Mwanza waongoza kwa ukuaji mkubwa wa mchango wake katika pato la Taifa (GDP) 2016

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Mkoa wa Mwanza, umekuwa wa kwanza kitaifa kwa ku-register ukuaji wa kasi wa pato lake kwa mwaka hadi kufikia asilimia 18.9% kwa mwaka 2016 huku ikifuatiwa na Mikoa ya Mtwara - 2.70%; Lindi- 1.96% na Rukwa - 3.60%.

Aidha, Mkoa wa Mwanza umeendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya Dar kwa kuchangia kiwango kikubwa kwenye pato la Taifa kwa kuingiza Trilioni 10 nyuma ya Dar yenye trilioni 17.6.

Hiyo ni dalili njema ya neema siku zijazo kwa Mwanza ambao baada ya kuzorota kwa kasi kubwa kwa sekta ya uvuvi, umekuwa ukipitia kipindi kigumu kiuchumi kwenye miaka ya 2010s.

Hata hivyo, kutokana na Mkoa huo kuwa "distributing centre" ya Mikoa nane (8) ya Kanda ya Ziwa na Magharib, imeendelea kufanya Mkoa kunawiri kutokana na biashara hiyo.
Kutokana na mazingira rafiki na shindani yanayojengwa sasa na Serikali, ni wazi Mkoa huo utaendelea kukua kiuchumi hasa baada ya kuwepo jitihada kubwa za Serikali kukuza sekta ya viwanda.

IMG_2620.JPG



IMG_2621.JPG
 
Mkoa wa Mwanza unayo nafasi kubwa zaidi ya kuinua pato la Taifa endapo miundombinu mikubwa itaimarishwa hasa Uwanja wa ndege na usafiri wa majini.
chuo kikuu cha umma hata kimoja tu na kuboresha bandari(mwanza south). I think itapendeza zaidi. Kwa sasa serikali ya mkoa ipo busy kuweka mazingira mazuri kuvutia watu wa kipato cha juu na kati kuishi na kuwekeza. Time will tell.....
 
Naona Mwanza imebeba Geita na 'mkoa' pendwa wa akina Gervas kule Chato.

In all Mwanza ina potential kubwa kuchangia pato la taifa. Lakini sasa inabidi tujengewe barabara na miundo mbinu mingine. Kila mkoa inabidi upewe kipaumbele kulingana na mchango wake kwenye pato la taifa (msinipige mawe especially wale mnaotoka mikoa inayochangia kidogo...hahahaha)
 
chuo kikuu cha umma hata kimoja tu na kuboresha bandari(mwanza south). I think itapendeza zaidi. Kwa sasa serikali ya mkoa ipo busy kuweka mazingira mazuri kuvutia watu wa kipato cha juu na kati kuishi na kuwekeza. Time will tell.....
Na kupata sana Laizerg, mojawapo ya jambo kubwa litakalothibitisha had his ya jiji, ni kuwa na chuo kikuu cha umma cha hadhi ya juu. Najua kuna vyuo vingi vya binafsi lakini hasa vikubwa vya Bugando na SAUT, but hivyo bado ni cha mtoto.
Tunataka kuwepo Chuo kikuu level ya Dar ama Dodoma, kikiwa na sifa za kudahili wanachuo wa kozi zote hasa wa uhandisi, sheria, siasa, biashara pamoja na elimu.
 
Hayakuhusu ka Raha P, nakuja zaidi ya Sister P, sijachuja sijavuja .... niite Mwanza Mwanza, mi majani ka P, Master ka J, Rasta ka Baba T ......

IMG_2623.JPG
 
Ukishakamilika UWANJA WA KIMATAIFA WA NDEGE MKOA WA MWANZA
Mwanza itakua haishikiki tena,,yaani ije DIRECT FLIGHT FROM DUBAI TO MWANZA EMARATES AIR LINE

au BRITISH AIRWAYS FRM LONDON TO MWANZA aisee sipati picha hapo kwanza wakazi wa singida watakuja mwanza kusafiri

Watu wa bukoba,kahama,shy,musoma simiyu na wilaya woote hao watakuja mwanza,kwa hivyo mzunguko wa kibiashara utakua kwa kasi mahoteli pia yatafanya biashara
Kikubwa zaidi ARUSHA kutazorota saana kwa watalii

Watalii watashukia direct mwanza kwasababu kutoka mwanza to serengeti national park ni km-110 tu

Tofauti ya Arusha kwenda Serengeti national park km-470
 
Nawachukia sana watawala wa CCM, haiwezekani Mwanza tuzidiwe na Dar kidogo hivyo kuchangia pato la taifa alafu bado serikali iwekeze Dar mara 10 zaidi. Yaani pesa ya Mwanza inaenda kujenga Dar!

Ifike mahari kila mkoa upambane na hari yake, haiwezekani watu wa Mwanza tuonekane wabaya alafu pesa yetu iwe tamu.

Bado watu wa Mwanza hatujapata mtetezi, mpaka sasa hakuna uwekezaji wa NHC wowote wa maana unaoendelea hapa. Mpaka sasa kinachokwamisha uwanja wetu wa ndege usiishe ni kutengewa vijipesa kidogo wakati miladi mingine kama hiyo pesa zinachotwa tu hadhina.

Nasisi Mwanza tunahitaji Hospitali kubwa ya Serikali, Bugando siyo yetu, si rahisi Bugando kununuliwa CT scan na MRI machine na serikali kwasababu si mali yetu. Iweje mpaka leo bado Mwanza tuwe na misafara ya kwenda kutibiwa saratani Ocean road wakati pesa yetu mngeiacha nasi tungejenga Lake road yetu.

Napinga vijana wenzangu kusafiri siku nzima kwenda kutafuta chuo kikuu kule Dom na Dar wakati pesa ya Mwanza inaweza wajengea chuo kikuu hapa!

Ninasiku nyingi sijaenda kule Dar lakini nasikia kuna mtu mmoja kajenga maghorofa 20 yenye floor 4 kila moja pale Mlimani, kama ni kweli ndio maana nasema Mwanza hatuna mtetezi kwakuwa majengo hayo yangeweza jengwa Mwanza kama mwanzo wa chuo kikuu.

Eti wanajenga uwanja wa kisasa wa michezo pale Dodoma, si bora wangejenga hata Arusha! hiyo Dodoma yenyewe ata wawajengee huo uwanja alafu watangaze mechi ya Simba na Yanga bule uwanja haujai.

Yaani wanatuachia Mwanza liuwanja la michezo CCM walilojimilikisha! ambalo halina hata taa na halina paa. CCM walaaniwe!
 
jiwe la maji Dah!! Naona umeona mbali kwenye vitu ambavyo nimekuwa nikiviamini muda wote, huwezi ukiwa na jiji la pili kwa ukubwa nchini tena kwa dunia hii ya kisasa halafu linazidiwa mbali na jiji kuu la nchi.

Haya mambo yalitakiwa kuisha Karne ya 20 ambako London, Tokyo na Paris vilikuwa vinazidi majiji ya pili Birmingham, Osaka na Marseilles kwa kila kitu.
Siyo dunia ya Karne ya 21.
 
Dah!! Naona umeona mbali kwenye vitu ambavyo nimekuwa nikiviamini muda wote, huwezi ukiwa na jiji la pili kwa ukubwa nchini tena kwa dunia hii ya kisasa halafu linazidiwa mbali na jiji kuu la nchi.
Haya mambo yalitakiwa kuisha Karne ya 20 ambako London, Tokyo na Paris vilikuwa vinazidi majiji ya pili Birmingham, Osaka na Marseilles kwa kila kitu.
Siyo dunia ya Karne ya 21.
Ukweli ndio huo, Takwimu za kuchangia pato la taifa zinaonyesha Mwanza tunazidiwa kidogo sana na Dar, yaani mpaka sasa Dar bado haija double juu ya Mwanza lakini katika uwekezaji wa serikali Dar kumependelewa mara 10 zaidi sasa kwanini kila mji usijijenge kwa pesa yake?
 
Back
Top Bottom