Mwanza: Wanne mbaroni utekaji, mauaji ya mfanyabiashara wa madini

Mwanza: Wanne mbaroni utekaji, mauaji ya mfanyabiashara wa madini

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumteka na kumuua mchimbaji wa madini ya dhahabu, Nestory Marcel Inda (61), mkazi wa mtaa wa Stamico-Katoro, Wilaya na Mkoa wa Geita, ambaye mwili wake ulitupwa katika Ziwa Victoria eneo la Mwalo wa Thale, Wilaya ya Ilemela.

Akizungumzia tukio hilo siku ya Jumatatu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na mgogoro wa ardhi uliotokea kwenye machimbo ya dhahabu ya Lwamgasa, mkoani Geita.

"Watuhumiwa waliokamatwa ni Jacob Othiambo (36), ambaye ni mchimbaji wa madini na pia mpwa wa marehemu; Erick Francis Olang (37), mfanyabiashara na mkazi wa Kishiri – Nyamagana; Abdul Nassir Dinisha (29), mfanyabiashara na mkazi wa Nyamhongolo-Taiwan – Ilemela, pamoja na Kulolwa Mbusu Muksen (46), mganga wa kienyeji mkazi wa Igoma – Nyamagana," amesema Mutafungwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, watuhumiwa walimnyonga marehemu kwa kutumia kamba ya katani, na baada ya kufariki walitupa mwili wake ziwani kwa lengo la kuficha ushahidi wa tukio hilo la kikatili.

“Inadaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, watuhumiwa walikwenda kwa mganga wa kienyeji kusafishwa kwa dawa za kienyeji ili kufuta ushahidi na kukwepa mkono wa sheria,” amesema Mutafungwa.

 
Eeehhh Mungu....
Nifundishe kunyamaza...😶
 
Wenye kuua watu na wasipakamatwe Wala kupatikani ni wasiojulikana pekee ukiwa si mmoja wa hao ukiua mtu utapatikana kivyovyote vile

Hawa mawasiliano yatakua yamewakamatisha
 
Back
Top Bottom