JANAURY JORDAN
Member
- Jan 4, 2016
- 6
- 4
MWANZA
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibanda iliyopo Kata ya Mkorani jijini Mwanza, Bahati Parapara, alisema ruzuku iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya elimu bure haikidhi mahitaji.
Alisema Desemba 30 mwaka jana alipokea Sh 647,000 na watoto walioandikishwa shule ya awali ni 210, darasa la kwanza 230 na darasa la pili hadi la saba 1,250 ambapo shule ina jumla ya wanafunzi 1,690.
Mwalimu Parapara alisema fedha iliyotolewa ni ndogo kulinganisha na idadi ya wanafunzi ambayo ni kubwa.
Alisema mbali na fedha hizo, pia amepokea Sh milioni 5 za ujenzi wa matundu ya vyoo kutoka kwa mkurugenzi.
Mwalimu Parapara alisema wanaiomba Serikali kuongeza fedha mara mbili ya hizo zilizotolewa kwa sababu zilizotolewa hazitoshi.
“Mgawanyo wa ruzuku hiyo ni kwa ajili ya ukarabati asilimia 30, vifaa asilimia 30, mitihani asilimia 20, michezo asilimia 10 na utawala asilimia 10,” alisema Parapara.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Msingi Buhongwa, Rehema Maruzuku, alisema amepokea ruzuku lakini hakuweka wazi kiasi ambacho amepelekewa.
Alisema fedha hizo zitasimamiwa na mwenyekiti wa mtaa, kamati ya shule, mratibu wa kata na ofisa wa halmashauri.
“Shule hii ina jumla ya wanafunzi 800, mgawanyo wa ruzuku hiyo ni kwa ajili ya ukarabati asilimia 30, vifaa asilimia 30, mitihani asilimia 20, michezo asilimia 10 na utawala asilimia 10,” alisema mwalimu Rehema.
Aidha ameitaka Serikali kutoa ruzuku hiyo kwa wakati ili kuepuka kulimbikiza deni kama yalivyo madeni ya walimu ambayo kila kukicha yanaongezeka kutokana na kutokulipwa kwa wakati.
SOURCE: MTANZANIA