Mwanza: Muandaaji wa Tamasha la Werrason amekula za uso baada ya mashabiki kuingia mitini

usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
13,901
13,870
Aliyeandaa tamasha la Werrason Mwanza ala za uso ‘sileti tena msanii Mwanza’

Weekend hii mkoani Mwanza muandaaji wa Tamasta la Werrason amekula za uso baada ya mashabiki kuingia mitini katika show yake hiyo.


Kwa mujibu wa Gazeli la Mwanaspoti, Mwandaaji huyo wa Shoo ya Werrason, Lengos VIP amesema kuwa amechukizwa na mashabiki wa Mkoa wa Mwanza kutojitokeza kwa wingi na kuapa hatarudia kupeleka wasanii mkoani humo.

Alisema kuwa alimgharamia Werrason na aliamini watapata watu ukumbini, lakini ilikuwa tofauti na matarajio yake hivyo naye kuamua kuondoka ukumbini.

“Sitarudia, nasema hivi sitarudia tena kuleta msaniii yeyote Mwanza. Nilitumia gharama kubwa takribani 30 milioni, lakini hata 2 milioni sikuiona” amesema VIP na kuongeza.

Lengos alisema, “Nilimwambia hata yeye ‘Werrason’ kwamba aachane na shughuli unajua wale wasanii wakubwa wanafanya kazi kwa kuona watu wametosha ukumbini, tofauti na hapo ni bure,” amesema.

Rais huyo wa Wakongo nchini, amebainisha kuwa amebaini sababu ya kutoitikia kwa mashabiki na kusababisha changamoto kwa msanii wake kufanya au kutokufanya shoo ni kutokana na kukosa matangazo.

Kuhusu utaratibu wa tiketi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwenye shoo la leo,VIP amesema kuwa watakagua hizo tiketi na wale watakaokuwa nazo zikiwa bora wataruhusiwa kuingia.

“Tutakagua tiketi kwa wale watakaokuwa nazo bora wataingia, lakini atakayekuja kwa kughushi tunamlaza polisi,” amesema mwandaaji huyo.

Source: Mwananchi
 
Kutoka Congo hadi Mwanza nauli bei gani? Hiyo milioni thelasini aliitumia kwenye nini?
Siku zingine ajifunze kupunguza costs. Msanii sio lazima aje na wanenguaji kumi, wawili wanatosha. Msanii sio lazima abebe vyombo vya mziki. Vya kukodi atavipata Mza. Pia sio lazima msanii akae Mwanza wiki, anakuja leo leo, anatumubuiza usiku kucha then kesho anaondoka.
 
Kutoka Congo hadi Mwanza nauli bei gani? Hiyo milioni thelasini aliitumia kwenye nini?
Siku zingine ajifunze kupunguza costs. Msanii sio lazima aje na wanenguaji kumi, wawili wanatosha. Msanii sio lazima abebe vyombo vya mziki. Vya kukodi atavipata Mza. Pia sio lazima msanii akae Mwanza wiki, anakuja leo leo, anatumubuiza usiku kucha then kesho anaondoka.
Anamleta msanii akae wik anategemea nn
 
Mara mia angemchukua rayvanny au harmonize, werrason kwa wakati huu?

Hajui biashara ya muziki aisee.

Dar napo ategemee hayo hayo.
 
Huku ni bongo Panya wewe. Muziki wa wakongo walikua wanaupenda mafisadi sasa vyuma vimekaza. Kama wewe unapenda huyo Wera bora ungemwita akuimbie kwako. Alafu wakongo kwa Mashauzi fara sana. Mil 30 Kwanini usileta team ya WCB kutoa mondi alafu uone hilo fiesta litavokua. Bora wasukuma wamekubaka shwine we. Mangosha yamekubikiri sijui hela ya Mkorogo utapata wapi.
 
Back
Top Bottom