MWANZA KWACHAFUKA: wadau wa sensa waandamana hadi kwa DC baada ya serikali kushindwa kuwalipa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MWANZA KWACHAFUKA: wadau wa sensa waandamana hadi kwa DC baada ya serikali kushindwa kuwalipa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Aug 20, 2012.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

  Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tunaiomba serikali ijipange vizuri kuhusu zoezi hilo muhimu..vinginevyo tutatia mashaka kuhusu usahihi wa takwimu zitakazopatikana.
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  hili zoezi limeshaingia doa toka zamani sana na halitakuwa na ufanisi wowote......zitatoka takwimu zikionyesha tanzania ina jumla ya watu mil.19..tuko hapa
   
 4. M

  Malata Junior JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 1,198
  Trophy Points: 280
  Kweli serikali ijipange upya wenyeviti wa mitaa na vijiji wamesema wanashangaa wao kuambiwa wahamasishe sensa bila malipo wakati wabunge walilipwa sh. milioni moja kila mmoja ili kuhasisha sensa na hawahamasishi!wamesema wao watakaa nyumbani wahesabiwe kama wananchi wengine.
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,090
  Likes Received: 10,448
  Trophy Points: 280
  Mpaka 26 ifike tutaona mengi wachia mbali 26 yenyewe.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kweli kikwete anaweza
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inawezekana serikali inafanya makusudi ili wapate sababu ya kusimamisha zoezi la sensa kwa kisingizio kuwa watendaji wao wamegoma kumbe wameshindwa kuwadhibiti wanaotaka kipengele cha dini kisiwepo na hata sasa wanatishia kukwama kwa zoezi hilo. Pia walifanya makosa makubwa sana kuwaacha waalimu na kuchukua magraduate waliomtaani ambao walishajijengea imani kuwa serikali haiwezi kutekeleza mambo yake mpaka kwa njia ya migomo. Wamekuwa wakigomea pesa zao za kujikimu wakiwa chuoni mara nyingi ndipo wanazipata, sasa wanaendeleza silaha hiyo hadi mtaani.
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  they better abscond the censor thing.
  walau itakuwa fundisho kwa dhaifu kikwete
   
 9. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hii sensa kama serikali inasoma ramani imeshachemka
   
 10. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  "hivi masuala ya sensa si yako mahakamani haya.. hairuhusiwi kuyajadili.. tutavuruga ushahidi jamani..by the way madai yao ni makuuuubwa sana serikali haina uwezo kuwalipa..." majiburahisikwamaswalimagumu@tzyaleo.com
   
 11. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali itajuta kuchukua graduate kwenye zoezi hili.
   
 12. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ikiwa fedha zilishatengwa, hii imekaaje?
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280
  Chonde chonde Rais wetu; chukua hatua kuhakikisha hili zoezi linafanikiwa japo limeshavurugika kwa kiasi cha kutisha. Nisingefurahi uwe Kiongozi wa kwanza kushindwa hata kuhesabu watu wako! Itakuwa ni failure na aibu ya mwaka kwa serikali yako.

  Serikali inayoshindwa kuhesabu wananchi wake itaweza nini sasa? Ni rai yangu tusifike huko; tumia kila uwezo na mamlaka uliyo nayo kufanikisha hili.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Serikali DHAIFU haina uwezo
   
 15. A

  ADK JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,149
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kiukweli serikali ya magamba imeshindwa kutawala
   
 16. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kumbe walimu walikuwa na hekima na uvumilivu mkubwa eee!
   
 17. m

  massai JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Bila kuweka wazungu au wachina hakuna DHAIFU aliwezalo.imesha ingia doa wala takwimu tutakayopewa sintoiamini hata kidogo.ingekua kwa hisani ya watu wa marekani hapo ningeamini
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo!!!
   
 19. H

  Hamuyu Senior Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  .
  M4C inaendelea huko Mwanza kwenye Semina ya walimu na Sensa habari zaidi tutawaletea live
   
 20. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata hili watasema M4C
   
Loading...