MWANZA KWACHAFUKA: wadau wa sensa waandamana hadi kwa DC baada ya serikali kushindwa kuwalipa.

Hii sensa kama serikali inasoma ramani imeshachemka

Mkuu, wanasema hivi "huhitaji kuwa kuku kujua kama yai ni bovu". tatizo la serikali ya ccm, hawataki kushauriwa. hii nchi ni yetu sote, tunahitaji kuwa na muafaka katika mambo fulanifulani ili sote twende kwa pamoja. sasa wao ni ubabe tuuuu, kisa eti wana mabunduki na mawasha washa. binadamu huwezi kumpelekapeleka kama kondoo. hili zoezi la sensa lina walakini, haya ngoja tuone, ila halitafanikiwa kwa kiasi kikubwa, labda wa-cook data.
 
Serikali itajuta kuchukua graduate kwenye zoezi hili.
Mbaya zaidi wasimamizi na watembeza dodoso wengi wamepewa hizo nafasi kiushkaji na wanarudisha 10 percent kwa waratibu wa sensa. Hii nimeishuhudia mwenyewe, kwa maana hiyo sensa inachukuliwa kama mradi wa wachache kufanya ufisadi. Kama walimu wangepewa kuendesha hili zoezi maadili waliyonayo yangefanikisha hili zoezi. Tegemeeni takwimu za ajabu sensa ya mwaka huu
 
...... Kama walimu wangepewa kuendesha hili zoezi maadili waliyonayo yangefanikisha hili zoezi. Tegemeeni takwimu za ajabu sensa ya mwaka huu
.
Hao walimu wanatumiwa na CDM ndo maana wameondolewa, pia hata haya malipo ya makarani huenda kuna mkono wa CDM; maana haiwezekani serikali iandae zoezi la sensa lenye dosari kibao namna hii...!
 
Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...

fedha zipo tena nyingi za kutosha. tatizo ni wahasibu wa HAZINA, na waratibu wa sensa wilaya husika, hawa ndio vimeo kabisa. wanachelewesha makusudi, mfano juzi walianza kugawa pesa saa 7 mchana wakati wanajua watu ni wengi 1500s. zoezi lingekuwa zuri kama wangeanza saa 2 asubuhi.

nasisitiza pesa zipo
 
ukweli nikiwa kama mdau wa sensa na nimoja ya watendaji,sensa imekuwa kama zima moto hali maandalizi ni miaka 10,hakuna vifaa,kama penseli,vitabu vya miongozo,na vingine vingi.sensa hh imetawaliwa na undugu na rushwa jambo ambalo linaweza kupelekea kutofanikisha zoezi hili.hebufikiri mtu anafundishwa kisha anapewa jaribio anapata 20% huyuni mke wa bosi mama wa nyumbani.Pinda na kikwete mmechemsha.
 
Hakuna sensa mwaka huu ni uhuni tu wa kugawana pesa zetu ndiyo unaofanyika.
 
Kazi za serikali huwa zinanipa wasiwasi kama waandaji wanakua serious! haiwezekani posho anayotakiwa mtu apewe kila siku aje apewe mwezi mmoja baada ya kufanya kazi! huyo mtu anaendaje huko kituoni? anakula nini?? sitaki kuamini kama bajeti ilikua haijapangwa na nina uhakika na hela zipo ila kwa vile nchi hii ilishakua ya 'Chukua Chako Mapema',watendaji wappo tayari kukwamisha malipo kwa kujinufaisha kwaNZA Wao wenyewe! Nchii hiii inaelekea kubaya sana tumwombe tu Mungu atujalie viongozi wenye busara 2015 kwani hawa waliopo hawana tena ubavu wa kuturudisha kwenye mstari!
 
.
Hao walimu wanatumiwa na CDM ndo maana wameondolewa, pia hata haya malipo ya makarani huenda kuna mkono wa CDM; maana haiwezekani serikali iandae zoezi la sensa lenye dosari kibao namna hii...!
Unaota ndoto za mchana au?
Kumbe haujui udhaifu wa Serikali ya magamba ndo maana unasema haiwezekani.

Mimi binafsi kama ningepewa nafasi ya kuishauri serikali kuendesha sensa, ningehusisha viongozi wa ngazi ya chini kama Wenyeviti wa Mitaa, na kila Kata ningepost mtaalam mmoja wa computer ambaye angefanya kaz ya ku-post data kutoka kwa wenyeviti wa mitaa. Kwisha habari,
lakini kwa serikali yetu yenye lundo la wazee wasiofikiri kisasa ndo wameanda vidodoso vya ajabu eti vitumike kwenye zoezi la sensa, ni ulaza mtupu tu!
 
Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...

Serikali ya wajanjawajanja,nasikia makarani wa sensa wanalazimishwa pia kufanya kazi ya vitambulisho vya uraia kwa malipo ya sensa,kazi ipo,nimeinyaka toka mikoani
 
Inawezekana serikali inafanya makusudi ili wapate sababu ya kusimamisha zoezi la sensa kwa kisingizio kuwa watendaji wao wamegoma kumbe wameshindwa kuwadhibiti wanaotaka kipengele cha dini kisiwepo na hata sasa wanatishia kukwama kwa zoezi hilo. Pia walifanya makosa makubwa sana kuwaacha waalimu na kuchukua magraduate waliomtaani ambao walishajijengea imani kuwa serikali haiwezi kutekeleza mambo yake mpaka kwa njia ya migomo. Wamekuwa wakigomea pesa zao za kujikimu wakiwa chuoni mara nyingi ndipo wanazipata, sasa wanaendeleza silaha hiyo hadi mtaani.

Tumeona tuwatumie wasomi waliopo mtaani ikiwa ni pamoja na ndugu zetu ili kuwawezesha kuichumi. Hili sio jambo baya ,tatizo ni hivyo walivyoanza kugoma tutakuja na hoja ya chama fulani cha upinzani kuwa nyuma yake utafikiri chama hicho ndio kilichowachagua,nasikitika kwamba tanzania ya leo hakuna watawala wanaotumia busara ktk mambo ya kitaifa,rejea baadhi ya kauli za viongozi kuhusiana na sensa ,wanatoa vitisho badala ya kuelimisha
 
Leo kuna Makarani wa Sensa Wilaya ya Kinondoni ilikuwa walipwe posho zao. Mkuu wa Wilaya mheshimiwa sana Jordan Rugimbana alipita kwenye baadhi ya vituo vya semina huku Mbezi Mwisho na kusema Posho watalipwa kuanzia kesho kwa kuwa BENKI HAKUNA HELA! Vijana walipomng'ang'ania na kutaka awaeleze ana maana gani hakuna pesa wakati shilingi BILIONI 140 ZILIISHA TENGWA kwa ajili ya Zoezi hilo akapanda gari lake na kutimua!
Jamani tukubaliane: Hapa hakuna Sensa. Mimi nawaunga mkono Vijana kugomea zoeizi hili mpaka wapate chao. Tatizo ni kuwa watendaji wa serikali DHAIFU wanajifanya wanajua sana pesa kuliko watu wengine na kila mtu hapo anapigia mahesabu cha Kuchukua Mapema!
 
JOSE na TUNDOSA ...hawa ni waratibu wa sensa nyamagana urasimu waliofanya inabidi wachunguzwe baada ya sensa kwani wamepokea sana rushwa za ngono na pesa....wameuza nafasi za waliokuwa wamechaguliwa na kuwapa wasiojua kusoma wala kuandika..hii ni aibu karani wa sensa kutokujua kusoma na kuandika
 
Kweli kikwete anaweza

Hili zoezi nahisi watu washakula 10% kabla ya zoezi lenyewe. sasa balance sheet zimegoma wanataka watu wafanye fujo makusudi ili wa-write off hela na zoezi lenyewe.

Hii ndo tanzania bana. kila kitu LEKA DUTIGITE
 
Hii ndo serikali ya ccm ni porojo tu, pesa ya sensa ilishatengwa lakini ni ufisadi kwa kwenda mbele kweli nimeamini ccm ni janga kwa taifa letu, yaani hata hili dogo la sensa malipo mpaka kuandamana hii ni zaidi ya Aibu!
 
Hivi hawa si waachane na hii sensa maana wanalazimisha sana ..kama imeshindikana basi waache...yasani hii nchi bana
 
Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...
.

Kuandamana kwa wana sensa ndio Mwanza kumechafuka? Wajameni Kiswahili chetu kinashitua sana.
 
Back
Top Bottom