Dah hapa nera karibia da kwa kina doi kichwa,kushoto kuna kina bi mkubwa walikuwa wanapika vitumbua hatari sana,kwenye kona ya kuingia nera toka makongoro kulikuwa na hospital ya dr chogo....wahenga wa mwanza tu ndio wanajua hii,si walioenda mwanza chuo!
Asante sana kwa ufahamu wako. Igogo na maeneo mengi jiji ni Dar yakiwemo Pasiansi, Nyamanoro na Mabatini na Kitangiri ni kama Miata ya Kilimanjaro ya Jiji la Rio de Janeiro Brazi
Haujitambui wewe. Usidhani watu wanaopost humu uzuri wa Mwanza hawajatembea ama wote wanaishi Mwanza. Wanapenda kwao na ndio furaha yao, we kama na inferiority complex sijui alishafika Dar so what? Ama unadhani Dar ni kila kitu? Mtu wa Dar akijisifia uzuri wa Dar kuna mburura mwingine atakubali hapa kudai ulishajiuliza Johannesburg? Wa Jo'burg naye ataulizwa ulishafika Dubai, Ndo unavyotaka?
Uwanja wa Kirumba na Rock City Mall na barabara ya Airport. Eneo linaloonekana ni pamoja na Mitaa ya Furahisha, Ghana, Nyamanoro, Kilimahewa, Pasiansi, Bwiru, Sabasaba, Ilemela na Airpot.
Rocky City Centre alongside Kenyatta Road, ni noma mzee. Kwa mbali ziwani meli inaonekana kwenye Bandari ya Mwanza North. Kilima kinachoonekana nyuma ni Kirumba.
Mwanza-Mwanza. Eneo linaloonekana ni Kilimahewa, Ghana, Kirumba, Isamilo, City Centre na Capri Point. Julia kwenye picha ni Kirumba stadium. Kipindi hicho hakujangwa Rock City Mall. Pembeni mwa Ziwa linaonekana soko maarufu la samaki Afrika Mashariki la Kirumba Mwaloni, ambapo biashara ya dagaa ni kubwa sana.