huyo masha ni mshkaji wake jk..si unajuwa ndio walimlipia karo ya masters ya riziwani university hapo uingereza...kwa hiyo baba mtu anataka kumlipia fadhila...KWANINI ASIMPE HATA U-HAUZI BOY HAPO IKULU awe anamsaidia kuchakachua
Watu wamepigwa mabomu hadi mitaaani kwao wanapoishi, ni moshi na muwasho watoto kwa watu wazima. Hivi demokrasia ndio hii??? Naona itafutee njia nyinigine ya kupata viongozi Tanzania hii ya kura itamaliza maisha ya watu wasio na hatia.
Habari kutoka Mwanza sasa ni Askari wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi kwahiyo Mwanza Ni vurugu mtindo mmoja. Hizi fujo zinaletetwa na CCM wenyewe badala ya kukubali na kutanga matokeo wao wanayeyusha watu ili waje wachakachue kazi ipo.
Kulingana na taarifa za ITV ni kuwa watu waliokuwa wanasubiri matokeo ya Ilemela na nyamagana wametawanywa na polisi kwa kutumia mabomu baada ya uvumilivu kuwashinda kusubiria matokeo na kuanza kurusha mawe.