figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Mtu mmoja ameuawa kwa kipigo na kuchomwa moto kwa tuhuma ya kupora simu ya mkononi aina ya Tecno.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema Juni 2, mtu huyo ambaye jina lake halikupatika anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, aliuawa baada ya kumpora simu mpitanjia eneo la Ngaza, Kata ya Nyegezi jijini hapa.
“Kabla ya kupora simu mtu aliyejulikana kwa jina la Aanicia Rwezaura alitishwa na yule aliyeuawa kwa panga, lakini wananchi wenye hasira kali walimwandama, kumpiga na hatimaye kumchoma moto hadi kufa,” alisema Kamanda Msangi.
Chanzo: Mwananchi