Mwanza: Auawa kwa kupora simu aina ya TECNO

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,701
Reaction score
59,214
Mtu mmoja ameuawa kwa kipigo na kuchomwa moto kwa tuhuma ya kupora simu ya mkononi aina ya Tecno.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema Juni 2, mtu huyo ambaye jina lake halikupatika anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, aliuawa baada ya kumpora simu mpitanjia eneo la Ngaza, Kata ya Nyegezi jijini hapa.

“Kabla ya kupora simu mtu aliyejulikana kwa jina la Aanicia Rwezaura alitishwa na yule aliyeuawa kwa panga, lakini wananchi wenye hasira kali walimwandama, kumpiga na hatimaye kumchoma moto hadi kufa,” alisema Kamanda Msangi.

Chanzo: Mwananchi
 
Daaah mkuu ukiwaza tar 16 inakaribia afu una simu feki lazima ukaibe
 
Simu yenyewe utakuta ni famba inasubiria kufungwa.
 
Mtu mmoja ameuawa kwa kipigo na kuchomwa moto kwa tuhuma ya kupora simu ya mkononi aina ya Tecno.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema Juni 2, mtu huyo ambaye jina lake halikupatika anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, aliuawa baada ya kumpora simu mpitanjia eneo la Ngaza, Kata ya Nyegezi jijini hapa.

“Kabla ya kupora simu mtu aliyejulikana kwa jina la Aanicia Rwezaura alitishwa na yule aliyeuawa kwa panga, lakini wananchi wenye hasira kali walimwandama, kumpiga na hatimaye kumchoma moto hadi kufa,” alisema Kamanda Msangi.

Chanzo: Mwananchi
 
Acheni kujichukulia hatua mikononi maana mara nyingi kunakuwa na uovu
 
Poleni wafiwa, leo takwimu za umaskini kimkoa zimewekwa hadahrani kumbe watu wa mwanza kele bure mitandaoni Mwanza ni kati ya mikoa sita inayo ongoza kwa umaskini nchini.. watu wa mwanza tafuteni hela acheni kuuana na kutukana watu wa Arusha.
 
Ukiona mtu anamtetea mwizi eti kwanini kauwawa basi ujue hajawahi kuibiwa
 
Mwanza? Mtu anakwambia kwetu sengerema lakini napenda nyegezi.
 
Back
Top Bottom