Dadiz
Member
- Jun 30, 2018
- 20
- 8
Ndugu wana jamvi, kwa kipindi kifupi nimekuwa nikifuatilia kinachoendela ktk mitandao ya kijamii! Awali tuliona andiko la Mwanjelwa ambaye amekuwa akilalamikia kuingiliwa na Naibu Spika Dkt Tulia kwa kuita wajumbe viongozi wanawake na kuwapatia semina yenye lengo la kuwapatia elimu ya kiuongozi jambo ambalo lilikuwa na manufaa makubwa kwa viongozi hao na si dhambi kufanya hivyo.
Pili jumbe zinazosambaa kuhusu tabia ya Dkt Tulia.
Kwa mtiririko wa mambo na kinachoendelea kinachopangwa kufanywa dhidi ya Dkt Tulia. Katika mchezo huu nawaona watu wawili ambao ndio “masters”.
Matukio yafuatayo yanaakisi hali ilivyo hadi Spika kupata hofu kubwa
1) Sote tunafahamu kuwa mwaka 2005-2010 Spika alkuwa Hayati Mzee Sitta na naibu akiwa Anne Makinda. Miaka 5 baadaye Naibu Spika Makinda akaja kwaa kiti cha Spika.
2) Mwaka 2010-2015 Aliyekuwa Spika Anne Makinda alkuwa anasaidiwa na Job Ndugai. Busara ilimwomgoza Makinda hakuchukua fomu ya kuendelea na Uspika kwa kusoma alama za nyakati hivyo kuamua kustaafu. Naibu Spika wake Job Ndugai akarithi mikoba kw kutwaa kiti cha Spika.
3) Mwaka 2015-2020 Job Ndugai akatwaa kiti na Naibu wake akiwa Mwanasheria Dkt Tulia Akson.
Hapa ndio mwanzo wa yote yanayoendelea. Job Ndugai anataman kuendelea na kiti chake hapo 2020-2025 lakini kila akipiga hesabu anaona tayari bundi ametua juu ya paa la jengo la bunge, akilala akiamka anaota Dkt Tulia.
Hofu yake kwa Dkt Tulia inasababishwa na mambo
Lakwanza ni historia na elimu ya Tulia. Tulia alisoma na kupata Shahda ya uzamivu mapema sana ktk Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika Kusini akiwa na miaka 31 tu! Na ndiye msichana pekee aliywahi kupewa dhamana ya kuongoza kitivo cha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa na miaka 33.
Mwaka 2015 Jk alimpandisha na kumteua awe Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. JPM alipoingia madarakani tu akaona atamfaa kwenye nafasi ya Naibu Spika. Kote huko hakuna mahala Dkt aligombea wala kuonyesha uchu wa kutaka kuongoza. Taarifa za ndani zinasema hata kugombea unaibu Spika ilikuwa ni mifumo kuelekeza kulingana na uhitaji! Ni kama ilivyoonekana JPM anafaa kuongoza.
Dalili zote zinaonyesha hizi si zama za siasa za iyena iyena ama zile za majungu na fitina. Ni siasa za hoja na proffession! Inatarajiwa kuwa robo tatu ya wabunge watakaoingia bungeni 2020 ni wale wa aina ya Kabudi, Ndalichako nk. Ndio maana hata Ndg yangu Kibajaji akisimama anajenga hoja iliyokwenda shule.
MBEYA
Mwanjelwa ni mwanasiasa aliyeingia bungen 2010 baada ya kuwa kwenye baraza kuu la wananwake kwa miaka 2 kuanzia 2008! Mwanjelwa alipata shahada ya heshima kutoka kwa Mch Lwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto.
Na kwa Miaka yote hiyo yeye anasimama kama ndiye alama ya akina mama wa Mbeya. Hata hivyo mambo yamebadilika ghafla kuanzia 2015 mara baada ya Dkt Tulia kuingia. Tangu aingie ktk siasa Dkt Tulia amejielekeza ktk kufanya siasa za maendeleo.
Amejitofautisha kabisa na siasa zilizoeleka na makada wa CCM za kutoa kanga, vitenge na 2,000 kwa akina mama. Yeye Dkt amejielekeza kupeleka maendeleo kila kona ya Nchi, utamsikia yuko Iringa, Mwanza na kwingineko! Leo unamsikia kapeleka misaada Kyela kwa wahanga wa mafuriko ili kuwasaidia.
Kwa Mbeya taarifa za ndani zinamtaja kama ndiye mtu pekee Chama kinamtegemea kukomboa Jimbo la Mbeya Mjini.
Hata hivyo nyota na mvuto wake unang’aa sio tu Mbeya bali kote Nchini. Karibu majimbo yote ya Mbeya yanamhitaji awe mwakilishi wao! Awali ilielezwa angegombea Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, kisha tukasikia anaenda jimbo la Rungwe baadae ikawa Busokelo kisha tukasikia tetesi anahitajika Kyela lakin saivi mwangwi wote ni Mbeya mjini!
Kimsimgi tukubali kuwa Mwanjelwa ni kiongozi anayefanya kazi zake za kiwaziri vizuri lakini si busara kumuweka katika mizania na Dkt Tulia! Ni kulinganisha kichuguu na Mlima Kilimanjaro kuanzia elimu, kazi walizowahi fanya, hata utulivu wanapozungumza!
MCHEZO ULIPO
Si mada yetu leo kuelezea mahusiano ya Ndugai na Mwanjelwa. Hilo kila mbunge anajua. Maudhui ya Makala hii ni kuchambua ndoa ya wawili hao kisiasa.
Sio siri tena juu ya uwepo wa vikundi ama movement zinazoratibiwa na boss huyo akimtumia Mwanjelwa kwa kumfinance kijana anayeitwa Mdau wa maendeleo ili kumzuia Dkt Tulia asiweze kushinda Ubunge endapo ataamua kufanya hivyo.
Mwanjelwa anaogopa kufunikwa na hatimaye kupotea katika siasa za Mbeya huku Ndugai akiwa anaogopa kuchukuliwa kiti chake cha uspika. Mwingine ameongezeka ni Sugu ambaye ameanza kuona uwakilishi wake unafika ukomo.
Hivyo kundi hili la “wanaoishi kwa matumaini” wamejikuta wakiunda ndoa inayoitwa utatu mtakatifu ikimhusisha Sugu, Mwanjelwa na Ndugai. Plan A ni kumsaidia Mwaselela ashinde kura za maoni na ikishindikana basi watumie Plan B ambayo ni kum-finance Sugu aendelee. Kwao agenda si Chama bali Dkt Tulia asivuke.
UGUMU WA POJECT NDUGAI/MWANJELWA.
Utekelezaji wa project Hii unachangiwa na mambo mengi, moja Dkt Tulia hajatangaza popote anagombea, hafanyi kampen wala kukutana na wajumbe wala wananachama zaidi ya kupeleka miradi na kuondoka.
Jambo hili linawafanya washindwe hata kumrekodi. Pili Mvuto wa Dkt Tulia mbele ya wana- Mbeya na watanzania. Ukifika Mbeya leo utakutana na jina la Dkt Tulia utadhan ana miaka 75 au utafkiri amekaa bungeni miaka 20 lakini binti huyu mwenye miaka 42 amehudumu bungeni kwa miaka 3 tu sasa.
Lakini mng’ao na mwangwi wake unawfunika wanasiasa waliokaa miaka 20.
NINI MPANGO WA BADAYE KUNDHOOFISHA DKT TULIA?
Mapacha wawili wamejipanga kutumia mbinu mbalimbali ili kunchafulia taswira mama huyu. Mbinu ya kwanza ni hiyo inayoendelea ya kunshutaki kwenye Chama ili wakati ukifika hoja ijengwe kuwa mtu huyu alianza kukiuka kanuni za Chama,
Mkakati namba mbili ni kumchafua kwenye mitandao ikiwemo kutumia vijana ili ionekana hana maadili hajiheshimu ili watu wenye busara wamwone hafai. Mkumbuke siasa za kuchafuana hazijaajza leo,
Dkt Salim aliambiwa alimuua Karume, Kikwete aliambiwa ni anashinda disco ni mhuni. Aidha wako wabunge wakike walioambiwa ni malaya, wengine wakaambiwa wasagaji nk!
Hivyo kikundi hiki kiendelee kupanga njama za kila aina lakini mwisho wa siku Chama hiki cha Magufuli si kama zamani.
MWISHO
Mchezo huu ukiendelea nitaleta hapa mawasiliano kamili ya njama zote zinazopangwa za kuchafuana. Najua kwa sasa liko jambo lingine wanapanga. Nafuatilia ili nije shusha kombora.