BULOLE BUKOMBE
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 488
- 109
Sijawahi ona machozi yangu mwenyewe takriban kwa miaka 30, hadi niliposhuhudia picha za rundo la nyama za Hayati Mwangosi, kidume mimi nimelia na kumwaga chozi hadharani,walau basi ingekua amechinjwa tu na majambazi ama vibaka nisingeumia hivi.Amechinjwa na Serikali tuliyoiweka wenyewe madarakani,siamini.Si kwamba mwangosi alikuwa kikaba,mwizi,ama aliyekuwa vitani dhidi ya serikali,alikua akiwajibika kwa taifa,kazi iliyompatia riziki yake halali na watoto wake.Kwa kutimiza wajibu wake,amefanywa rundo la nyama,alitenda dhambi ipi Mwangosi hata kustahili kufa kifo kilichomsahili Nduli Idd Amin! Askari aliyefanya hivyo Fimbo ya mungu ikatende kazi sasa na apate mateso makali ktk maisha yake hapa duniani na mwisho ahera.Na Serikali iliyo madarakani ikaadhibiwe vikali.Naomba mungu asinitoe duniani kabla sijashuhudia Serikali hii na Chama chake vikiadhibiwa vikali.
Imeandikwa apandaye uharibifu atavuna uharibifu hakika wote tulioona maiti ya Mwangosi hatutaitoka dunia hii kabla ya baadhi yetu hawajashuhudia kisasi cha MUNGU kwa waliomtoa roho mpendwa wetu Mwangosi