VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Daud Mwangosi,ulale salama,
Ulikupata mkosi,ukatuacha nyuma,
Wamekuua Polisi,tena bila huruma,
Mwangosi nakulilia.
Ukiwa kazini,unajitafutia kipato,
Umejawa umakini,ili kutunza watoto,
Polisi mahayawani,wakaleta habari nzito,
Mwangosi nakulilia.
Channel Ten,kituo chako cha kazi,
From then,umewaachia majonzi,
Yes we can,wataindeleza kazi,
Mwangosi nakulilia.
Ni nzima Tanzania,utaratibu unafahamika,
Polisi wafanya hima,kombe kufunika,
Wenyewe hawana bima,milele kufika,
Mwangosi nakulilia.
Tume imeshaundwa,uchunguzi kufanya,
Tayari imeshashindwa,ushahidi kukusanya,
Polisi wanapondwa,kwa wanayoyafanya,
Mwangosi nakulilia.
Sikia ahadi yangu,Hayati Mwangosi,
Polisi adui zangu,hata kwenye kadamnasi,
Nitamaliza hasira zangu,nikiamua kuasi,
Mwangosi nakulilia.
Raha ya milele umpe ee Bwana,na mwanga wa milele umwangazie.Apumzike kwa amani.Amina.
Ulikupata mkosi,ukatuacha nyuma,
Wamekuua Polisi,tena bila huruma,
Mwangosi nakulilia.
Ukiwa kazini,unajitafutia kipato,
Umejawa umakini,ili kutunza watoto,
Polisi mahayawani,wakaleta habari nzito,
Mwangosi nakulilia.
Channel Ten,kituo chako cha kazi,
From then,umewaachia majonzi,
Yes we can,wataindeleza kazi,
Mwangosi nakulilia.
Ni nzima Tanzania,utaratibu unafahamika,
Polisi wafanya hima,kombe kufunika,
Wenyewe hawana bima,milele kufika,
Mwangosi nakulilia.
Tume imeshaundwa,uchunguzi kufanya,
Tayari imeshashindwa,ushahidi kukusanya,
Polisi wanapondwa,kwa wanayoyafanya,
Mwangosi nakulilia.
Sikia ahadi yangu,Hayati Mwangosi,
Polisi adui zangu,hata kwenye kadamnasi,
Nitamaliza hasira zangu,nikiamua kuasi,
Mwangosi nakulilia.
Raha ya milele umpe ee Bwana,na mwanga wa milele umwangazie.Apumzike kwa amani.Amina.