armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
R. I. P
Hivi unajua connotation ya neno 'nigga'? Yaani wimbo una maneno machafuchafu wewe ndiyo umeona wa kumpa marehemu. Hata kama hujui kiingereza siyo kujipostia tu hata takataka. Ungetafuta hata jirani akusaidie kuufanya uendane na mazingira.
Mbona hao viongozi walitoa machozi ya furaha kuona kuwa wameongeza msukule mwingine tena nje ya waandamanaji. Weeeewe!! pipoz pawa at work
mkuu nakupongeza kwa kutoa muda wako na kutunga kazi nzuri kumuenzi marehemu, tupo pamoja katika kumuombea na kumkumbuka.Apumzike kwa amani mwangosi pamoja na marehemu wote waliouwawa na polisi kwenye mikutano ya ukombozi .
Hivi unajua connotation ya neno 'nigga'? Yaani wimbo una maneno machafuchafu wewe ndiyo umeona wa kumpa marehemu. Hata kama hujui kiingereza siyo kujipostia tu hata takataka. Ungetafuta hata jirani akusaidie kuufanya uendane na mazingira.
Hebu wewe tuletee wimbo wako hapa.. Au maneno ya kuonyesha huzuni yako tulinganishe... Manake bado sijakuelewa unachopenda kusikia juu ya Marehemu.
Eti kuna mtu anatoa pongezi kwa 'kutunga' kazi nzuri. Sijui hata anajua maana ya kutunga.
Hii ni thread ya mia moja ya kuhusiana na tukio hili. Halafu mnarudia maneno yale yale. Iko kazi
Hii ni thread ya mia moja ya kuhusiana na tukio hili. Halafu mnarudia maneno yale yale. Iko kazi
Daud Mwangosi,ulale salama,
Ulikupata mkosi,ukatuacha nyuma,
Wamekuua Polisi,tena bila huruma,
Mwangosi nakulilia.
Ukiwa kazini,unajitafutia kipato,
Umejawa umakini,ili kutunza watoto,
Polisi mahayawani,wakaleta habari nzito,
Mwangosi nakulilia.
Channel Ten,kituo chako cha kazi,
From then,umewaachia majonzi,
Yes we can,wataindeleza kazi,
Mwangosi nakulilia.
Ni nzima Tanzania,utaratibu unafahamika,
Polisi wafanya hima,kombe kufunika,
Wenyewe hawana bima,milele kufika,
Mwangosi nakulilia.
Tume imeshaundwa,uchunguzi kufanya,
Tayari imeshashindwa,ushahidi kukusanya,
Polisi wanapondwa,kwa wanayoyafanya,
Mwangosi nakulilia.
Sikia ahadi yangu,Hayati Mwangosi,
Polisi adui zangu,hata kwenye kadamnasi,
Nitamaliza hasira zangu,nikiamua kuasi,
Mwangosi nakulilia.
Raha ya milele umpe ee Bwana,na mwanga wa milele umwangazie.Apumzike kwa amani.Amina.