Mwangosi day wilaya ya Mufindi

Mwangosi day wilaya ya Mufindi

JUSTIN MPOTWA

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
16
Reaction score
11
Ndugu watanzania,

Zimebaki siku kadhaa kutimiza mwaka mmoja toka pale ndugu yetu Daudi Mwangosi alipouawa na polisi kwa bomu pale kijijini Nyololo.

Mwangosi aliuawa tar 02/09/2012 na hii ina maana tar 02/09/2013 ndio itakuwa ni siku ya kumkumbuka.

CHADEMA wilaya ya mufindi tumeandaa shughuli mbalimbali kumkumbuka ndugu yetu. Jimbo la Mufindi Kusini wanaratibu shughuli hizo.

Kutakuwa na matukio makubwa mawili

1. Uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya mwangosi ambao utasimikwa na katibu mkuu wa
CHADEMA taifa ndg dr. Wilbrod Slaa.

2. Harambee ya kuchangia familia ya Mwangosi mchango ambao utawasilishwa kwa mjane wa marehemu siku hiyo.

3. Mkutano wa hadhara utakao fanyika Nyololo na Igowole

Tunapenda kuwashirikisha wale wote ambao wangependa kuchangia shughuli zote hizo.

Tunatoa namba za simu za makamanda wanaohusika na uratibu wa shughuli hizo

a. Katibu jimbo, Emmanuel Ngwalanje 0787797950
b. Katibu mwenezi jimbo, Elisha Msemwa 0755733918
c. Mhazini jimbo, Carolina Kidenya 0768757447

Karibuni wote

============
Willbroad%20Slaa%281%29.jpg

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kimepanga kujenga mnara wa kumbukumbu katika kijiji cha Nyololo ili kumuenzi aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyeuwawa katika kijiji hicho.

Mwangosi aliuwawa katika kijiji hicho Septemba 2, mwaka jana kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa CHADEMA na polisi.

Katibu wa CHADEMA jimbo la MufindiKusini, Emmanuel Ngwalanje, akizungumza na NIPASHE jana alisema mnara huo ambao utagharimu kiasi cha Sh. 3,500,000 utaanza kujengwa Agosti 20 na kukamilika Agosti 28, mwaka huu na kuwaomba wadau kusaidia fedha kufanikisha ujenzi huo.

Ngwalanje alisema mmiliki wa eneoalipouwawa Mwangosi amekubali kutoa kibali cha kujengwa mnara huo, hivyo baada ya ujenzi kukamilika Septemba 2, mwaka huuambayo ni siku aliyouwawa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa,ataweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.

Alisema siku hiyo pia kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mjane wa Mwangosi na watoto wake.

Katibu huyo aliwataka wadau kusaidia kuchangia gharama za ujenzi wa mnara huo ili ujenzi uanzeharaka na kukamilika kwa wakati.

Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, anadaiwa kuwawa wakati polisi walipofyatua mabomu wakati CHADEMA wakiwa katika harakati zakufungua tawi la chama hicho katika kijiji cha Nyololo.

Kabla ya kuuawa kwa mwanahabarihuyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisiyao.

CHANZO: NIPASHE
 
Mwangosi atakumbukwa kwa vizazi na vizazi, ukombozi huu umekaa juu ya damu yake, tuko pamoja kimichango
 
Kabla ya Mwangosi day napenda kuuliza yule aliemlipua bomu Mwangosi ameshahukumiwa na sura yake inajulikana au ndo kininjaninja!?
 
Kuchangia familia yake ndio swala lenye manuufaa pamoja na shughuli zingine zitakazofanyika
Nitatuma mchango wangu kwa moja ya namba hizo mlizoweka
 
damu ya ndg yetu mwangosi haitopotea bure,itakuwa juu ya vichwa vyao wote waliotekeleza na waliowatuma.amen
 
asante kwa taarifa , ntaleta mchango bila shaka .
Pamoja sana Makamanda, Mungu awatangulie katika shughuli hiyo nzito ila damu ya Mwangisi iwe ni chachu ya ccm kulaaniwa na wale ambao bado wana i support.
 
TUko naye katika sala na siku moja mtoto wake atasoma na kufungua madai ya baba yake kuuwawa kinyemela
 
Khaa ivi mwangosi alikuwa na harakati gani za kuikomboa tz?
 
Willbroad%20Slaa(1).jpg

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kimepanga kujenga mnara wa kumbukumbu katika kijiji cha Nyololo ili kumuenzi aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyeuwawa katika kijiji hicho.

Mwangosi aliuwawa katika kijiji hicho Septemba 2, mwaka jana kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa CHADEMA na polisi.

Katibu wa CHADEMA jimbo la MufindiKusini, Emmanuel Ngwalanje, akizungumza na NIPASHE jana alisema mnara huo ambao utagharimu kiasi cha Sh. 3,500,000 utaanza kujengwa Agosti 20 na kukamilika Agosti 28, mwaka huu na kuwaomba wadau kusaidia fedha kufanikisha ujenzi huo.

Ngwalanje alisema mmiliki wa eneoalipouwawa Mwangosi amekubali kutoa kibali cha kujengwa mnara huo, hivyo baada ya ujenzi kukamilika Septemba 2, mwaka huuambayo ni siku aliyouwawa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa,ataweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.

Alisema siku hiyo pia kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mjane wa Mwangosi na watoto wake.

Katibu huyo aliwataka wadau kusaidia kuchangia gharama za ujenzi wa mnara huo ili ujenzi uanzeharaka na kukamilika kwa wakati.

Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, anadaiwa kuwawa wakati polisi walipofyatua mabomu wakati CHADEMA wakiwa katika harakati zakufungua tawi la chama hicho katika kijiji cha Nyololo.

Kabla ya kuuawa kwa mwanahabarihuyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisiyao.

CHANZO: NIPASHE
 
Tutamkumbuka daima mpendwa wetu Mwangosi,saa chache akiwa na ziraili kamhanda...
3833_261785427274451_780090219_n.jpg
 
Apumzike kwa amani Mwangosi. Utawala wa Kikwete utaondoka ukiacha kumbu kumbu mbaya sana kuwahi kutokea toka Tanganyika ilipopata uhuru wake. Ni katika utawala huu ndipo tumeshuhudia polisi wakiuwaua raia eti kwa sababu wamekusanyika au kuandamana kwa amani. Ni katika utawala huu ndipo tumeshuhudia aina mpya ya propaganda za kisiasa kupitia CCM za kutengeneza ugaidi na kufungua kesi za kigaidi. Ndipo tumeshuhudia watu waking'olewa kucha, meno, kutobolewa macho, kulipuliwa kwa mabomu kama ilivyotokea kwa Mwangosi, kulipua mabomu kwenye mikusanyiko ya maombolezo kama ilivyotokea kule Arusha, jeshi letu kuingia katika utekaji na utesaji wa raia kama inavyofanyika kule Mtwara eti kwasababu wananchi wanapinga gesi isiende Dar na maovu mengi ambayo yanahitaji kitabu kizima kuyaandika yote. Maneno kama ''kitu kizito chenye ncha kali ndipo tumeanza kuyazoea kila raia wanapouliwa au kujeruhiwa na vyombo vya dola. Kwa kifupi ni utawala unonuka damu za wananchi wasiokuwa na hatia!
 
R.I.P Mwangosi. Bwana alitoa serikali ya Kikwete ikatwaa. Walaaniwe wote waliosimamia na kutekeleza uovu huu. Damu ya mtu asiyekuwa na hatia itawatafuna kokote watakakoenda. Hata wakistaafu na kupewa marupu rupu yatokanayo na jasho letu hawatakuwa na amani vifuani mwao kutokana na damu isiyokuwa na hatia. Jinsi mwili wa Mwangosi ulivyosambaratishwa unamtia hasira mtu yeyote mwenye moyo wa nyama na utu wa binaadamu. Hakika wauaji na watesi wa familia ya Mwangosi watakufa vinywa wazi. Kamuhanda alisema anataka kustaafu vizuri. Akaratibu na kusimamia mauaji ya Mwangosi. Na kweli waliomtuma wakampandisha cheo kwa kazi nzuri waliyomtuma. Ni kwa muda gani yeye na waliomtuma watafurahia uzuri wa dunia hii? Wataishi hadi ukamilifu wa dahari? Pua zao zimeangalia chini kudhihirisha kuwa mavumbini walitoka na watarudi huko kwa laana kubwa. Ingekuwa ni heri hawa wasingelizaliwa.
 
Serikali ebu iwe sirias kitendo cha kuuwa watu ovyo kikomeshwe mara moja amani hii kidogo iliyobakia si muda mrefu itasambalatika. AMANI inaletwa kwa kutendea HAKI kwa mhitaji Polisi aliemuua mwangosi anyongwe Hadharani bila chenga.
 
Back
Top Bottom