Awali, Profesa Kitima alisema: "Tumefanya mikutano mingi maeneo mbalimbali ya nchi, kanda ya ziwa, Dar es Salaam..., lakini tatizo bado Mtanzania si mlalamikaji."
"Kazi ni kuchochea wajue haki zao, maana Watanzania wanaweza hata kupewa maji yenye tope lakini wakakaa kimya."
Hata hivyo, akijibu hoja hiyo Profesa Mwandosya, alisema: "Kuna hili la uelewa mdogo wa Watanzania, mmh... sijui."
"Ninavyojua, Watanzania wa sasa ni waelewa sana,...maana sisi wanasiasa tunawaogopa sana, unaweza kwenda sehemu wanakwambia kama huna maji safi hupati kura."
"Sasa, sijui kwamba hawana uelewa kudai haki zao vipi, nafikiri tatizo ni kwamba hawajajua uwepo wa hili baraza, wakijua watakuja tu, lakini Watanzania ni waelewa sana hili sisi wanasiasa tunalijua." .