Mwandosya akiri mwamko mpya kwa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandosya akiri mwamko mpya kwa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 4, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Date::4/4/2009
  Mwandosya akiri mwamko mpya kwa Watanzania

  Na Ramadhan Semtawa

  Mwananchi

  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ametoboa siri yake na wanasiasa wengine, akisema Watanzania siku hizi wameamka si wa kubeza.

  Kauli ya Profesa Mwandosya ambaye mwaka 2005 aligombea nafasi ya kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekuja wakati Watanzania wamekuwa wakionyesha mwamko mkubwa kutambua haki na wajibu wao katika nchi.


  Profesa Mwandosya akionekana dhahiri kusoma alama za nyakati, akizungumza kwa umakini na upole kama kawaida yake, alipinga madai kwamba Watanzania wa sasa hawafahamu haki zao.

  Kauli hiyo ya Profesa Mwandosya kutambua uelewa wa Watanzania, aliitoa jijini Dar es Salaam jana baada ya kutembelea kwa mara ya kwanza Ofisi za Mamlaka ya Huduma za Maji na Nishati (Ewura).

  Akiwa katika ziara hiyo ya kwanza, Profesa Mwandosya ambaye alianza mkutano na wakuu wa Baraza la Kuwalinda Watumiaji wa Huduma za Ewura (Ewura-CCC), alisema wanasiasa akiwemo yeye wanaogopa Watanzania.

  Katika kauli hiyo ambayo alikuwa akijibu hotuba ya Mwenyekiti wa Ewura CCC Profesa Jamidu Katima, ambaye alisema moja ya changamoto inayokabili baraza hilo ni mwamko mdogo wa Watanzania kujua haki zao.

  Awali, Profesa Kitima alisema: "Tumefanya mikutano mingi maeneo mbalimbali ya nchi, kanda ya ziwa, Dar es Salaam..., lakini tatizo bado Mtanzania si mlalamikaji."

  "Kazi ni kuchochea wajue haki zao, maana Watanzania wanaweza hata kupewa maji yenye tope lakini wakakaa kimya."


  Hata hivyo, akijibu hoja hiyo Profesa Mwandosya, alisema: "Kuna hili la uelewa mdogo wa Watanzania, mmh... sijui."

  "Ninavyojua, Watanzania wa sasa ni waelewa sana,...maana sisi wanasiasa tunawaogopa sana, unaweza kwenda sehemu wanakwambia kama huna maji safi hupati kura."

  "Sasa, sijui kwamba hawana uelewa kudai haki zao vipi, nafikiri tatizo ni kwamba hawajajua uwepo wa hili baraza, wakijua watakuja tu, lakini Watanzania ni waelewa sana hili sisi wanasiasa tunalijua."


  Mwandosya, katika hatua nyingine ametoa msimamo kwamba, mamlaka hiyo inapaswa kujiendesha kwa uhuru kwa mujibu wa sheria na endapo atatokea mtu kujaribu kuingilia ni vema akataarifiwa.

  Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema imekuwa ni bahati mbaya watu kudhani mamlaka hiyo ipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakati iko chini ya Wizara ya Maji.

  Masebu alisema, Waziri wa Maji na Umwagiliaji ndiye mwenye dhamana ya mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria ambayo imeunda Ewura.

  Ewura CCC inaundwa na wajumbe kutoka wizara sita ambazo ni Nishati na Madini, Maji, Viwanda na Biashara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (AG), Fedha na Uchumi na Miundombinu.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Inapofikia wana siasa kuelewa umuhimu wa wananchi ujue mambo yanaanza kwenda vizuri.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Naam nakubaliana nawe Mfumwa kwamba sasa wanasiasa wanaanza kuona tofauti ya Watanzania katika kufuatilia haki zao ikiwemo maslahi ya nchi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hili litasaidia sana katika kuleta mabadiliko ya uongozi katika nchi yetu kwa maslahi ya Watanzania wote.
   
 4. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  very diplomatic coded message directed to wanaojijua...(I see two things, a warning to those who think wananchi ni wajinga, and the other is a message for the people kuendelea kudai haki zao na wasibabaishwe na watu...) - thats just my view.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mfumwa,

  Prof. Mwandosya anajua hilo tokea miaka ya 90. Nafikiri amerudia tu kitu anachokiamini.

  Tatizo ni je wanasiasa wangapi wanaamini hivyo? Ukiwaona wananchi wajinga, kuna siku watakupiga chini tu.
   
 6. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  hii inaweza kupotosha msomaji.
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja mkuu, hapa kawaambia wananchi kijanja wasiogope kudai haki zao
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Watanzania sio mabwege tena.

  FMEs!
   
Loading...