mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 19,998
- 49,115
Leo katika kipindi cha sundown cha Magic FM mtangazaji Moses Mtete alikuwa akiripoti taarifa ya jeshi la polisi kumkamata kijana aliyemtukana Rais kupitia mtandao wa facebook
Cha ajabu mtangazaji huyo akasoma aya yote yenye hayo matusi yaliyoandikwa mtandaoni bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo na yeye anakuwa ameshiriki kumtukana Rais.
Maadili ya uandishi yanamtaka kusoma yale maneno ya staha na alipofika kwenye tusi husika alitakiwa kusema ........ au kuruka neno hilo.
Najua haikuwa nia yake kumtukana Rais bali kukosa maarifa kunakochangiwa na ukanjanja uliopitiliza.