Mwandishi wa habari atakayemhoji mbunge aliyesusia Bunge kunyang'anywa kitambulisho

Baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje ya BUNGE kupinga adhabu ya Lema spika ameagiza waandishi watakaohojiana na wabunge hao nje ya ukimbi wa Bunge watanyang'anywa vitambulisho vya kufanya kazi bungeni.
Uhuru wa habari.
Sent using Jamii Forums mobile app
Waandishi wanaojitambua wangekwisharudisha vitambulisho hivyo bila kusubiri kunyang'anywa.
 
Kwani hao waandishi wanategemea kuishi kwa kuandika habari za bunge tu? Huu ni kuingilia uhuru wa waandishi wa habari.

Mbaya zaidi na ambalo hawezi kuzuia ni kwamba siku hizi kila mtu ni mwandishi wa habari, hivyo habari zinapatikana hata kabla ya wahusika kuzitoa.
 
Baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje ya BUNGE kupinga adhabu ya Lema spika ameagiza waandishi watakaohojiana na wabunge hao nje ya ukimbi wa Bunge watanyang'anywa vitambulisho vya kufanya kazi bungeni.

Uhuru wa habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipo haja spika apewe mapumziko angalau ya miezi sita, kwani anayoyafanya bungeni sasa yanathibitisha kuwa hayupo sawa kabisa. Ni aibu tena ni aibu kubwa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom