Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Mwandishi wa habari wa channel ten Adam Malima amechukua form ya kuwania kuteuliwa na chama cha mapinduzi CCM kugombea ubunge wa jimbo la Mpwapwa mkoani Dodoma.
Adam Malima ambae ni mzaliwa katika jimbo hilo ameeleza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha kuwa anaifungua Mpwapwa ili iwe kubwa zaidi kimaendeleo.
Alisema Mpwapwa ina fursa nyingi za kukuza uchumi wa wakazi wa Mpwapwa pamoja na maendeleo ya wilaya kwa ujumla lakini hazitumiki wala kufikiwa na watu wengi jambo ambalo linafanya wakazi wa wilaya hiyo kutonufaika na fursa walizonazo.
“Tunaenda kuifanya Mpwapwa iwe kubwa zaidi”MAKE MPWAPWA GREAT kwa kufungua fursa za kukuza uchumi kwa wananchi na kuwezesha vyanzo vipya vya mapato kwa halmsahauri.” Alisema Adam Malima
“Mpwapwa kiasili ni kubwa na ina fursa za kutosha kusitawisha maisha ya wananchi, mfano kwenye kilimo wananchi wanazalisha sana lakini wanalanguliwa mazao yao kwa kuwa hakuna muunganiko kati yao na masoko ya uhakika, kama tukiweka mfumo rasmi wa masoko ya mazao wananchi watapata faida kubwa tofauti na sasa na halmashauri itakusanya mapato kwa wingi zaidi tofauti na sasa.
Alisema Adam Malima na kuongeza kuwa sekta hiyo ya kilimo pekee inatumiwa na mafisadi kujinufaisha wenyewe lakini kama kungekuwa na mpango mzuri wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato yatokanayo na mazao ya kilimo Mpwapwa ingekuwa na mapato makubwa ambayo yangeweza kutumika kwa kuboresha huduma za jamii kama afya na elimu lakini mapato yote wajanja wanapiga.
“Haiwezekani wananchi walime walipe kodi au ushuru wa mazao lakini fedha hizo zinaishia kwenye mifuko ya walaji, ni wakati sasa wa kupambana na kukomesha ufisadi unaofanyika kwa wananchi wa Mpwapwa”. Alisema Adam Malima
Chanzo: Chanel 10