The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Brighton Kinemo, leo amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi hiyo huku akiahidi kuwaletea wananchi wa Mvomero mabadiliko chanya yanayojengwa juu ya misingi ya uongozi bora, siasa safi na maendeleo jumuishi. Fomu hiyo imekabidhiwa kwake na Katibu wa CCM Wilaya ya Mvomero, Bi. Florence Machicho
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kinemo alisisitiza kuwa huu ni wakati wa kuanzisha zama mpya katika jimbo hilo kwa kutumia fursa zilizopo kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi. “Ninaingia katika kinyang’anyiro hiki nikiwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Mvomero kwa uaminifu, ushirikishwaji na uwazi. Mvomero ina kila sababu ya kuwa mfano wa maendeleo endelevu nchini, tunahitaji tu uongozi sahihi na maamuzi yenye tija kwa wananchi wote,” alisema Kinemo kwa msisitizo.
Kaulimbiu yake “Mvomero Kwanza: Uongozi Bora, Siasa Safi, Maendeleo kwa Wote” imeanza kushika kasi mitandaoni, ikitafsiriwa na wengi kama wito wa matumaini kwa vijana, wakulima, wanawake na wafanyabiashara wanaotaka kuona mageuzi ya kweli katika elimu, afya, miundombinu na fursa za ajira. Kinemo ameahidi kuwa akipewa ridhaa, atahakikisha kila kijiji kinaunganishwa na huduma muhimu kama barabara, maji, umeme na vituo vya afya vilivyo bora.