Mwandishi Moses Methew amtaka Dkt. Abbas ajitokeze hadharani kulijibu bunge la EU, adai Balozi hatoshi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,877
Akizungumza mubashara katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari kinachoongozwa na Nyanda " Mtozi" mwandishi mbobezi Moses Methew amemtaka msemaji mkuu wa serikali Dkt. Abbas atoke hadharani kuelezea sakata la bunge la EU na Tanzania.

Moses anasema hakuna sababu ya kulinyamazia swala hili kwani linagusa maisha ya watanzania wote na kwamba taarifa ya balozi wetu Ubelgiji haitoshi na haiwafikii wananchi wote.

Kipindi kinaendelea....

Ni Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Hakuna haja ya kuwajibu wahuni wachache wa bunge hilo. sioni tatizo lolote hapo hadi kumfikia kumsumbua msemaji mkuu wa serikali

Unawaita wahuni wakati mnawalamba miguu ili wasisiitishe kutoa mkopo...

Dr. akiwajibu tegemea na wao watagongelea msumari kulingana na tamko la Dr Abbas... Bora akae kimya asubiri wanaume watakacho amua...
 
Back
Top Bottom