Mwandishi bora ni FID Q,,,flow bora ni CHID BENZ

kanali mstaafu

JF-Expert Member
May 17, 2015
4,318
4,104
Ukisema uandishi wa mashairi adhimu katika HIP HOP Fid q ni Baba lao na ukizungumzia msanii wa HIP HOP mwnye flow nzuri kuliko yeyote ni CHID BENZI

Nipingwe kwa hoja kama kuna ulazima
 
Labda Chid Benz wa kipindi kileeee.kuhusu fid huwa namkubali sana huyu mtu lkn sijajua kashindanishwa na nani
 
Kwamba fid ni mwandishi bora...
Maoni ni kama USHUZI kila mtu anaweza utoa.
 
Mkuu,

Hapa ungepanua wigo...ungesema katika wabongo flava, nani mkali wa kuandika ili pengine wajuvi watupe mkali wao.....

Na hili jambo la kutofautisha HIPHOP na Bongoflava huwa sielewi wajuvi wanakuwa na maana gani hasa, natamani nipate jibu hapa. Binafsi, uimbe chochote kile, ilimradi ni kutokea hapa hapa, basi kina ile ladha ya hapa. Labda kama BONGO inayotamka inamaanisha AFRIKA MASHARIKI kama wakenya wanavyosema.
 
Ila lile besi la chidy wa ilala lafamilia kipindi kiiiileeeeee hatari....fid inabidi uwe na ubongo wa ziada kumwelewa ...wote wapo vizuri
 
Amani kwa Chachage na Makuadi wa Soko huria
Baba ahsante kwa utafiti na zawadi ya Almasi bandia...

Alinifanya nimchimbe zaidi Prof Chachage (Rest in Peace).Hiki kichwa ni hatari sana.

Anakwenda zaidi anakuambia,

Unataka kuchukiwa na mjinga, Mwambie akikosea
Ukweli siku zote unapigwa mawe, Uongo uzidi kuenea
Wenye nia hawana nguvu, Wenye nguvu hawana nia
Wanaridhika na moja, Wanaogopa kutafuta mia...

Shikamoo Fareed Kubanda.
 
Yeah umeongea kitu kikubwa sana....Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita nchi hii haijawahi kupata Rapper mzuri kama Chid Beenz.

Kwa flow Chid Beenz hakuna kama yeye pamoja na matatizo yote anayopitia ila bado Akishika kipaza anawafunika walio wazima.
 
Heko Chid benz
 
Nipinge kwa hoja mkuu
Unapo sema fulani ni mkali tena kwenye upande wa Hip Hop Lazima uguse mambo muhimu na nyeti ya utamaduni huo.
Unataka upingwe kwa hoja wakati wewe huna hoja zaidi ya kuweka hisia zako.
Ningekujibu kwa hoja kama mada yako ingekaa kitaalam.
 
Ukisema uandishi wa mashairi adhimu katika HIP HOP Fid q ni Baba lao na ukizungumzia msanii wa HIP HOP mwnye flow nzuri kuliko yeyote ni CHID BENZI

Nipingwe kwa hoja kama kuna ulazima
Unataka upingwe kwa hoja lkn wewe umekuja bila hoja
 
Nilikuwa nakubali sana flow ya mtu anaitwa NOORAH 'Babastyles'
 
Amani kwa Chachage na Makuadi wa Soko huria
Baba ahsante kwa utafiti na zawadi ya Almasi bandia...

Alinifanya nimchimbe zaidi Prof Chachage (Rest in Peace).Hiki kichwa ni hatari sana.

Anakwenda zaidi anakuambia,

Unataka kuchukiwa na mjinga, Mwambie akikosea
Ukweli siku zote unapigwa mawe, Uongo uzidi kuenea
Wenye nia hawana nguvu, Wenye nguvu hawana nia
Wanaridhika na moja, Wanaogopa kutafuta mia...

Shikamoo Fareed Kubanda.
sijawahi kujuta kumpenda fid q hata siku moja japo kuna wengine kama staminer, mwana fa, langa rest in peace ngwear rest in peace, pamoja na songa huwa napenda sana kuwasikiliza sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom