Mwanaume ni nani?

Mwanaume ni nani?

Hivi humu hakuna wanaume?
Au wanasoma na kujipima then wnasepa!!!!
Tupo, tumesoma, tumejipima na tumeona kwa kiwango kikubwa tunayatimiza hayo, tunaacha asilimia ndogo tu kwa sababu sisi ni binadamu.
 
Thats de BLAZE...MAN2MAN katika kuzisaka doo na kuamini anaweza yote...Kama umeiona leo yako that means kesho ni ya MAULANA., Men Hustle hard
 
Mwanaume
1.hamfokei mke
2. Hampigi mke
3. Hatumii vilevi Wala bangi
4. Havuti sigara
5. Mpole
 
MWANAUME NI NANI? (sio mvulana tafadhali)

Mwanaume ni sehemu ya uumbaji wa Mungu, ambae huanza majukumu katika umri mdogo kabisa.

Hutoa sadaka ndoto zake kwa ajili ya kuwafurahisha wazazi wake

Hutumia pesa yake aliyoipata kwa jasho kumnunulia zawadi mwanamke ampendae kwa ajili ya kumpa furaha

Hujitoa ujana wake wote kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mke wake na watoto wake bila kulalamika.

Hujenga future (kesho) ya watoto wake hata kwa kuchukua mikopo benki ambapo huilipa hata miaka yote.

Kamwe havai mlegezo, hasuki nywele, havai heleni wala kujinyonya nyonya midomo.

Kamwe hampigi mkewe, mkewe akikosea husuruhisha kwa njia za kidiplomasia na kwa akili. (kama maandiko matakatifu yalivyoagiza)

Mkewe akiwa katika majonzi na huzuni, humkumbatia na kumuangalia machoni, humwambia "mke wangu haya ni majaribu tu, nakupenda, usikate tamaa, mumeo nipo tutasonga mbele"

Mkewe na watu wengine hufikiria hivi juu yake;

Kama akienda out, basi si muangalifu

Kama akibaki nyumbani, yeye ni mvivu

Kama akiwagombeza wanae, ni mkali hajui kulea.

Kama asipowakaripia watoto, basi sio baba muwajibikaji

Kama akimzuia mkewe kufanya kazi, basi ni mwanaume asiejiamini

Kama asipomzuia mkewe kufanya kazi, basi ni mwanaume anaetegemea mshahara wa mkewe

Kama akimsikiliza mama yake, basi ni mtoto wa mama

Kama akimsikiliza mkewe, basi ni mtumwa wa mkewe au mume bwege
**********

Muheshimu kila mwanaume anaekupenda kwa dhati, huwezi jua ni mangapi anajitahidi kuyafanya ili tu akupe furaha wewe.

Pia nakupa pole kama umeumizwa, aliyekuumiza sio MWANAUME huyo ni MVULANA JOGOO, MWANAUME kamwe hadondoshi chozi la Mwanamke wake, kwake mwanamke wake ni tunu na johari ambayo inapaswa kutunzwa na kuthaminiwa kwa hali na mali!

"WANAUME" wa namna hii wapo, kama bahati mbaya haujawahi kukutana nae pole sana. Hiyo ilikuwa sample ndogo hivyo hauwezi ukathibitisha kuwa wote wako hivyo. Shuhuda ni nyingi mno.

Narudia tena pole sana, omba MUNGU, utakuja pata MWANAUME, au Omba Mungu ambadilishe huyo uliyefunga nae pingu au mtarajiwa wako kutoka Mvulana kuwa Mwanaume.

Share "WAVULANA" wote wasome, na "WANAUME" wafarijike kwa kazi wanayoifanya.
What a lovely Fairy tale!!
 
Back
Top Bottom