Nilikuwa msomaji na mpenzi mkubwa wa gazeti la Jitambue ambalo kwa muda mrefu sasa halipatikani mtaani.Katika gazeti hilo mambo mengi kuhusu saikolojia yalizungumzwa na kutolewa ufafanuzi.Moja ya jambo ambalo liliwahi kuniacha hoi katika moja ya makala ya gazeti hilo,ni ile iliyokuwa inazungumzia kuhusu wanaume kuingia kwenye mzunguko wa hedhi kama walivyo wanawake.Gazeti hilo lilitaja baadhi ya dalili za kumgundua mwanaume kuwa yuko katika siku zake ni pale anapokuwa na hasira kupita kiasi au anaonekana kubadilika kabisa tofauti na tabia yake halisi.
Wenzangu imekaaje hii?!