Mwanaume kutunzwa na mwanamke, hii imekaaje?

Bolivar

JF-Expert Member
Oct 23, 2010
229
103
Hili halizungumziwi sana lakini linakuwa kwa kasi. Kuna wanaume wa kutosha tu wanatunzwa na wanawake, wengine wako kwenye ndoa wengine mahusiano ya kawaida. The issue is wanaume hawa wameridhika, wanaona ni sawa na hawajishughulishi.

Kwa ushamba wangu wa uhafidhina mtizamo wangu ni kuwa na roles sawa kwenye mahusiano, kila mtu achangie kwa kutegemeana na kipato chake japo wengi wa kina dada wanaamini wanaume sharti wafanye kila kitu.

Kwa wanaume wanaotunzwa na wanawake, wanahisi vipi? Wanaona ni sawa tu? Hawa wanawake wanafikiri vipi? Ni aina gani ya wanawake hutunza wanaume? Na sababau ni zipi? Je hili ni sawa kijamii? Wanaume waliowahi kutunzwa na wanawake wanaweza kutupa uzoefu? Na wanawake wanaotunza wanaume, please give us your experience.

Ningefurahi kujua.
 
wengi wao wanaotunzwa ni wale wanaume wavivu,wapenda starehe 7bu hawajuigharama, hawana kazi. Na dizaini cku akipata mkwanja thubutu yako kama utapata mapendo yaleeeee. Ndo hayo tu
 
Beijing ndio imeleta haya, kwa hiyo usawa kwa wote! Halafu siku hizi wanaume wachache kule wanawake hivyo wanagombaniwa kweli kweli:pound:
 
Lady G, kwa hiyo hakuna mapenzi hapa, ni pesa tu? Lakini hawa jamaa wana kitu cha ziada, si bure mwanamke akakuhudumia kila kitu
 
Adam 'utakula kwa jasho' na wewe Eva utazaa kwa uchungu..... ikiwa vise versa akili kumkichwa
 
mnalilia haki sawa kwa wote, zamani wanawake walitunzwa na wanaume lakini siku hizi wameamua kuonyesha kuwa na wao wanaweza. Swali


je, we mwanamke unaemtunza mwanaume unajisikiaje, unamchukuliaje?



unahisi kama unaweza kumsikiliza na kumtii kama ambavyo ungefanya kwa anaekutunza?
 
Lakini kusema ukweli inapendeza mwanaume akijishughulisha! Kwa mtazamo wangu. A man ambaye analelewa na mwanamke anakuwa inferior, insecured na haijakaa sawa tu! Umekaa nyumbani kila siku unasubiri mwanamke arudi toka kazini jioni.. Mh! Hapana!!
 
Ukweli unatabaki palepale kuwa mwanaume atakula kwa jasho ila inapotokea mwanamke anamtunza mwanaume inategemea huyu mwanaume yukoje aidha anaumwa au ni mlemavu ila kama ni mzima jamani majukumu ni kusaidiana si kuachia mtu mmoja, tatizo la wanaume wengi siku hizi wanakimbia majukumu yao sio kisa una mke anatunza familia wewe unajiengua.
 
wanaume wengi wanaotunzwa huwa ni vidumu, hawataki kufanya kazi wala kujishughulisha, wengine masharobaro
 
iko poa tu kama vile mwanaume anavyomtunza mwanamke,si haki sawa jamani
 
Back
Top Bottom