Mwanaume kunyonya....!!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Eti mila potovu Tanzania zawanyima watoto haki ya kupata lishe ya maziwa ya mama, je wanaume wanapaswa kunyonya maziwa ya wake zao wakati wakiwanyonyesha watoto?? Mila za wanaume kunyonya maziwa zimepitwa na wakati

Kuna mjadala huu nimekutana nao kuleeee...ngambo ambao umejikita zaisi katika maandiko: Je ni ruksa??

Permalink Imejibiwa na IL-YA on April 5, 2009 at 8:31pmKUNYONYESHA MTU MZIMA:
Ndugu zangu wana Forodhani,nachukua nafasi hii nyembamba kuwashukuru kwa mawazo yenu kuhusiana na swali hili la mke kumnyonyesha mtu mzima hata kama itabainika kuwa mtu mzima yule ana ndevu kibao na mvi!!!
Kisheria kabisa ndugu wapendwa inajuzu,kama dada G.EYE alivyoweka bayana na wengine pia waliochangia kwa mawazo mazuri yalionenepa!!!

lakini ningelipenda kuweka wazi zaidi jambo hili kiriwaya ili ijulikane kuwa jambo hilo linaruhusiwa na ni vema kufanya hivyo hususan mke akiamua kumnyonyesha mumewe kwa maana ya kunyonyesha:

Kwanza kabisa aya tukufu ya 233 ya suuratul Baqarah inasema:
[Na wanawake waliozaa wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kukamilisha kunyonyehsa,na baba (wa huyo mtoto) yampasa chakula chao na nguo zao kama ada.Wala nafsi yoyote isikarifishwe ila kadiri ya uwezo wake.Mama asiwekwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake,wala baba kwa ajili ya mtoto wake,na mrithi yampasa kama hivyo.Na watakapopendelea(baba na mama)kumwachisha maziwa,kwa kuridhiana na kushauriana,basi hakuna lawama juu yao.Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha,basi hakuna lawama juu yenu kama mkitoa mliyoyaahidi kwa wema.Na mcheni Mwenyeezi Mungu na jueni kwamba Mwenyeezi Mungu anayaona mnayoyatenda.]

Hii ndio aya ndani ya Qur’an Tukufu inayozungumzia kuhusiana na suala la kunyonyesha.

KISA CHA KUNYONYESHWA MTU MZIMA:
Anasimulia mwana Aisha (mkewe Mtume) kuwa:Alikuja kwa Mtume SAHLA BINT SUHAYL akasema:
“Ewe Mtume wa Mwenyeezi Mungu!(kila) anapoingia kwangu SALIM, ninamuona ABU HUDHAYFA anachukia.Mtume akasema:Mnyonyeshe,SAHLA akasema:Yeye ana ndevu,(riwaya nyingine yasema:yeye ni mtu mzima) Mtume akajibu:Mnyonyeshe, mashaka ya ABU HUDHAYFA yatakwisha”

Ndugu mpendwa Mwana Forodhani tazama kisa hicho sehemu hizi:
• SAHIHI MUSLIM: JUZU YA 2, UKURASA WA 1078.
• SUNANUN NASAI: JUZU YA 6, UKURASA WA 104.
Kwa hiyo, Mwana aisha akawa akimwamuru dada yake UMMU KULTHUM kuwanyonyesha WANAUME mabalimbali anaowapenda waingie nyumbani mwake!!

Tazma: Al-Ummu, ya Shaafii:Juzu ya 5,ukurasa wa 28.
Tafsir Ibn Kathir: juzu ya 1, ukurasa wa 291.
Assunanul Kubra: Juzu ya 7, ukurasa wa 460.

The so called...IL-YA...


Permalink Imejibiwa na IL-YA on April 5, 2009 at 8:36pmILIPOSEMWA KUNYONYESHA,NI NENO TOFAUTI NA KUCHEZEA MATITI,KUCHEZEA MATITI KITU KINGINE NA KUNYONYESHA KITU KINGINE,LAKINI VYOTE VIWILI VINAJUZU KISHERIA,MUME KUMCHEZEA MATITI YALE MATAKATIFU NA MKE KUMNYONYESHA MUMEWE ,YAANI KUMNYONYESHA KAMA JINSI ANAVYONYONYESHWA MTOTO.KWA HIYO SIKU MUME AKITAKA KUNYONYA MAZIWA YA MKEWE HAKUNA NOMA NDUGU,UTANYONYA KWA RAHA ZAKO,NA HAYA NDIO MAPENZI YENYEWE!!!

THE SO CALLED ..IL-YA..


Permalink Imejibiwa na Al Mabrouk on April 5, 2009 at 10:56pmIL-YA alisema:
KUNYONYESHA MTU MZIMA:
Kwanza kabisa aya tukufu ya 233 ya suuratul Baqarah inasema:
[Na wanawake waliozaa wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kukamilisha kunyonyehsa,na baba (wa huyo mtoto) yampasa chakula chao na nguo zao kama ada.Wala nafsi yoyote isikarifishwe ila kadiri ya uwezo wake.Mama asiwekwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake,wala baba kwa ajili ya mtoto wake,na mrithi yampasa kama hivyo.Na watakapopendelea(baba na mama)kumwachisha maziwa,kwa kuridhiana na kushauriana,basi hakuna lawama juu yao.Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha,basi hakuna lawama juu yenu kama mkitoa mliyoyaahidi kwa wema.Na mcheni Mwenyeezi Mungu na jueni kwamba Mwenyeezi Mungu anayaona mnayoyatenda.]

The so called...IL-YA...
Hiyo aya haijaruhusu MTU MZIMA KUNYONYA wala hakuna pahala ndani ya KURAAN paliporuhusu mtu mzima kunyonya maziwa ya chakula cha watoto wake.

Ila ipo aya inasema Mwanamke aliekunyonyesha huruhusiwi kumuoa na mtu ambae mumenyonya ziwa moja hata kama hilo ziwa si la mama yako mzazi basi ni haramu kwako kuoa au kuolewa nae.

Jamani hapo kunyonya kumetengeneza haramu ya ndoa kwa watu walinyonya ziwa moja hata kama sio ndugu.

Kama hiyo hekima haionekani hapo basi lakini mimi sikubali uhalali wa MTU MZIMA kunyonya maziwa ya mwanawe wala sioni sababu.

4_23.gif



KURAAN 4:23
"Mmeharimishiwa kuoa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na wanawake walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa kuoa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika ALLAH ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu."

hivyo KURAAN ndivyo inavyosema.



Permalink Imejibiwa na IL-YA on April 5, 2009 at 11:31pmKWA HIYO UNAPINGA RIWAYA NA KISA HIKI KILICHOSIMULIWA NA AISHA (A.S)?/

NA UNAPINGA KAULI ZA MAULAMAA WOTE WALIOSEMA INAJUZU?WE VIPI/
KWANI MAULAMAA HAO WALIKUWA HAWAONI AYA HIYO,HIYO AYA IKO NA MADHUMU YAKE NA MAKUSUDIO YAKE AMBAYO WEWE UKACHANGANYA KATIKA VITU HIVI VIWIWLI,WAMEHARAMISWA KWENU MAMA ZENU,HAIAMAANISHI KUWA MKEO AKIKUPA MAZIWA UTUMIE BASI AMEKUWA MAMA YAKO!!!


USIDHANI MTU AKIKUNYONYESHA NDIO ANAKUWA MAMA YAKO,KAMA NDIO HIVYO BASI MTUME (S.A.W) ASINGELISEMA INAJUZUMKE KUMNYONYESHA MUMEWE!!!!

KISHA MAZIWA KATIKA CHUCHU ZA MKEO NANI ALIKWAMBIA KUWA MAZIWA HAYO NI MTOTO TU,HIVYO MTU MWINGINE HARUHUSIWI KUNYONYA? MAZIWA YALE NI MUME NIYE MMILIKI WA KWANZA KISHERIA KWA SABAU CHAKULA KILICHOTUMIKA KURUTUBISHA AU KUONGEZA MAZIWA YALE,NICHAKULA ALICHOKICHUMA MUME,NDIO MAANA SHERAIA IKASEMA HAIRUHUSI MKE KUMNYONYOSHA MTOTO ASIYEKUWA WA MUMEWE PASINA RIDHAA YA MUME KUFANYA HIVYO!!!


KWANINI,KWA SABABU MAZIWA NI YA MUME!! YEYE NDIYE MWENYE MADARAKA KATIKA MAZIWA YALE,AKIAMUA KUNYONYA POATU,SHERIA INAMLIDA,NA SI LAZIMA SHERAIA IWE NDANI YA QUR'AN !!1
KWANI KUNA MABO MANGAPI NI SHERIA LAKINI HAYOPO NDANI YA QUR'AN TUKUFU BALI TUNAYAPATA KUTOKA KATIKA HADITHI ZA MTUME (S.A.W)? LUKMAN VIPI NDUGU,HUJASOMA NINI???/


HEBU REJEA JIBU LA DADA G.ILI UJUE NI JINSI GANI MAULAMAA WALIVYOJIBU SWALI HILO,TATIZO LAKO HUTAKI HADITHI UNATAKA KUTOSHEKA NA QUR'AN TU,NILIKUULIZA KAMA MSIMAMO WAKO NI SAHIHI KUTOSHEKA NA QUR'AN TU,BASI TWAMBIE ULIJUAJE KUWA UNATAKIWA KUSWALI SWALA TANO,SUBHI RAKAA MBILI,MAGHARIBI TATU,NA ZILIZOBAKI NNE???????HAYO YOTE YAMO NDANI YA QUR'ANI???????




THE SO CALLED ..IL-YA...



Permalink Imejibiwa na IL-YA on April 5, 2009 at 11:32pmQUR’AN NA HADITHI ZA MTUME (S.A.W):

NDUGU LUKMAN:
We unasema kuwa Mtume (s.a.w) chochote ila QUR’AN tu.Kwahiyo mtu atakaye kuja na hadithi au riwaya,wewe kama wewe hutambui kitu mambo!!

Katika site tukufu ya kwa jina “ZANZIBARWEBSITE” wewe ndiye ulikuja na maajabu zaidi,maana yaonekana hata Qur’an huijui japo kuwa unatembea nayo au inapatikana home kwenu.

NGOJA NIKWAMBIE QUR’AN INAKUTAKA UFANYE NINI,
Qur’an tukufu inasema,
“mkizozana au (kutofautiana) katika jambo basi lirudisheni jambo hilo kwa MWENYEEZI MUNGU NA{ MTUME WAKE}”
Hapa Allah (s.w) hakusema lirudisheni jambo hilo kwangu tu,bali kasema kwangu na kwa Mjumbe wangu kwenu ,yaani Mtume Muhammad (s.a.w),na huwezi kulirudisha jambo hilo kwa Mtume (s.a.w) bila kupitia hadithi za Mtume (s.a.w) au Riwaya mbali mbali.Hivyo basi ukitaka aya upate RIWAYA AU HADITHI za Mtume (s.a.w) ni lazima urejee katika vitabu vilivyokusanya hadithi hizo na riwaya hizo,kitendo cha kukataa hadithi na au riwaya zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) na ukasema kuwa hakuna hadithi za Mtume (s.a.w) wala riwaya bali Qur’an tu!!!
Kauli hii,itaonesha kuwa wewe PUNDA,yaani kivipi?
kinamna hii bwana lukman:
Hebu tazama katika suuratul Jumua,aya ya 5,Allah (s.w) amesema:
{MFANO WA WALE WALIOPEWA TAURATI KISHA HAWAKUICHUKUA, NI KAMA MFANO WA “PUNDA” ANAYEBEBA VITABU VIKUBWA VIKUBWA,MFANO MBAYA MNO WA WATU WALIOZIKADHIBISHA AYA ZA MWENYEEZI MUNGU,MWENYEEZI MUNGU HAWAONGOZI WATU MADHALIMU.}

Hii ndio aya inatwambia kwamba kuibeba Qur’an bila kujua au kufuata yaliyokuwepo ndani yake,ni sawa na na PUNDA aliyebeba vitabu vikubwa vikubwa,lakini punda yule ukimuuliza umebeba nini,hajui alichokibeba,ukimuuliza yaliyoandikwa katika vitabu hivyo ulivyovibeba unaelewa nini maana yake?punda atakwambia sielewi?hivyo tukakatazwa tunaposhika kitabu hiki yaani QUR’AN tusiwe kama punda bali tuelewe kilichoandikwa ndani yake na tufuate tuliyoelekezwa kufuata.

sasa wewe leo hii unaambiwa hadithi za mtume kutoka katika vitabu mbali mbali kama vile vitabu vya kishia na kissuni,unasema hakuna vitabu vya kishia wala kisunni mbele ya Qur’an,na kwamba Mtume (s.a.w) hajatuachia hadithi,bali kitabu tu.!!!We vipi!!!! Hivi hujishangai kweli!!!

tena unakuja na aya usizozielewa makusudio yake,ili kuzitumia kupinga hilo,shauri yako ,ukionekana kama kituko Fulani hivi,usimlaumu mtu!!!!

THE SO CALLED ..IL-YA..

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom