Mwanaume kufa mapema

Mwanaume kufa mapema

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,933
Reaction score
34,912
Hivi ni kwann wanaume wengi hutangulia mbele za haki kuliko wanawake?
 
Shauri wana zambi nyingi sana.........wanawake wana dhambi chache ambazo nazo zinasababishwa na wanaume.......
Zambi......
Dhambi........
 
Wanaume hufa mapema kutokana na kufanya kazi nyingi za hatari kama bodaboda,ushimbaji madini ujambazi na kazi za ufundi zinachangia vifo vingi vya wanaume uvutaji wa sigara bangi unga na matumizi ya pombe Kali kupita kiasi msongo wa mawazo wa kuendesha familia.
 
Wanaume wanafanya kazi nzito jamani...
Wengine wanateseka wanalea familia huko mke hamjali mume wake ikiwa kumpikia vizuri.. kumpeti peti... sasa kwa kazi wanazofanya wakikosa faraja mwili unadhoofika sana huku sisi tunanenepeana tuu..mwanaume anaumwa mwanamke hajali wala nini ndio kwanza anadai hela..mwanaume anakosa pa kupumzikia kila siku mawazo majukumu yote ya mke na watoto juu yake ya wazazi wake juu yake huku mwanamke unamdharau mume wako.. hamna siku hata moja inapita hujamkwaza. Anawaza hadi damu za pua bado hatujali...
KUNA BAADHI YA WANAWAKE NI WAUWAJI.. nimekumbuka kisa kimoja acha kabisa.
MWANAMKE UNAYETAKA MUME WAKO AISHI MUDA MREFU MLEE WATOTO WENU PAMOJA...
..shirikiana nae kila jambo ..mfariji pale anapokata tamaa mpikie vizuri ale ashibe mpe haki yake...usimruhusu mume wako awaze mawazo tofauti ya kumuumiza..SASA WEW MTESE AFE NJAA NA MAWAZO HALAFU ULIE LIE
 
wanaume wanakufa mapema kutokana na sababu zifuatazo
1.Wengi ni Malaya sana nikiwemo na mimi pia
2.wengi ni wanywaji wa pombe kali na wanakula chipsi
3. wanashinda wana stress za.kutafuta hela ili walishe familia
4. wengi hawana mda wa kwenda ibadani unaweza kukuta mtu amekaa miezi sita hajawahi kutokea church na hapigii hata maombi kwake
5.wengi ni vibaka na wanafany kazi haramu na mbaya. mfano wew ni boda boda, dereva tax, maloli yani ukifanya kazi hizi lazima ufe mapema na kama wew ni jambazi au kibaka siku ukikamatwa lazima ufe kwa kichapo
6.wengi tunatembea na wake.za watu kuowa hatutaki tunakwepa majukumu na kubanwa na mkeo
7. taendelea baadaye kwanza nimalizie mzinga wangu huu
 
Ni takwimu gani zinaonyesha wanaume hufariki mapema kuliko wanawake?
 
Kwa mantiki hiyo wanawake ni sababu mojawapo ya janga hilo?
 
Manyanyaso wanayowapa wenza/wake zao tuu inatosha kuwafanya watangulie mbele za haki.
Kuna wanaume ni wanyama jamani. Unakuta mwanaume mtu mzima ana vototo vidogo kadhaa huku mkewe hamjali hata kidogo. Eti anarudisha damu mwilini.
Ndio maana mwanaume anaweza kupata ukimwi mke wake asipate coz wao wametulia
 
Labda tuanze kujua kwanza hao wanaume wanaokufa sana ni zipi chanzo cha vifo kwa sana?
Ajal?
Maradh?
 
wanaume wanakufa mapema kutokana na sababu zifuatazo
1.Wengi ni Malaya sana nikiwemo na mimi pia
2.wengi ni wanywaji wa pombe kali na wanakula chipsi
3. wanashinda wana stress za.kutafuta hela ili walishe familia
4. wengi hawana mda wa kwenda ibadani unaweza kukuta mtu amekaa miezi sita hajawahi kutokea church na hapigii hata maombi kwake
5.wengi ni vibaka na wanafany kazi haramu na mbaya. mfano wew ni boda boda, dereva tax, maloli yani ukifanya kazi hizi lazima ufe mapema na kama wew ni jambazi au kibaka siku ukikamatwa lazima ufe kwa kichapo
6.wengi tunatembea na wake.za watu kuowa hatutaki tunakwepa majukumu na kubanwa na mkeo
7. taendelea baadaye kwanza nimalizie mzinga wangu huu

sired clozid
 
Hivi ni kwann wanaume wengi hutangulia mbele za haki kuliko wanawake?

Kwa sababu Wanawake wana akili klk Wanaume hali inayowapelekea Wanawake kuwa waangalifu na maisha yao, kwa mfano huwezi kuona Msichana anafanya michezo ya hatari kama kupanda miti au kudandia malori au ni mara chache kukuta Mwanamke amelewa mpaka anajikojolea na asubuhi tayari yuko anatoa lock!

Kiumri pia wanaume hu oa wanawake wenye umri mdogo kwa mfano Mugabe is 44 yearsolder than his wife Grace. Biologically mugabe atatangulia mbele ya haki kabla ya grace
 
Back
Top Bottom