Mwanaume kiuno chako kinatakiwa kiwe chepesi kwa ajili ya kumridhisha mkeo

Mwanaume kiuno chako kinatakiwa kiwe chepesi kwa ajili ya kumridhisha mkeo

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
3,712
Reaction score
11,611
Ameandika James Gn,
JUKUMU LA KIUNO KUWA LAINI NA CHEPESI NI LA MWANAUME NA SI MWANAMKE.

Kama wewe ni Mwanaume na Umekaza fuvu eti kwa kudhania Mwanamke ndiye mwenye jukumu la kukishitua kiuno au kukatika wakati tendo likiendelea unapote sana.

Mbali na ukweli kwamba Wanawake ndiyo hujilegeza na kuwa na kiuno chepesi kinachompa urahisi yeye kuifikia jimai kimsingi Mwanaume ndiye mtu mwenye jukumu hili la kukitumia kiuno chake kama Weapon kwa ajili ya kuziibua na kuzimaliza hisia za Mwanamke.

Leo nakupa sababu za kwanini Mwanaume unapaswa kuwajibika nyakati za kupeana mdinyo na Mke wako au Mwanamke wako.

Ipo hivi👇

Mtazamo wa Kisaikolojia, Ki-Afya na Kiuhusiano. Mwanaume anapaswa kuwa na "kiuno chepesi" (yaani kuwa na uwezo mzuri wa kushiriki kikamilifu na kwa ufanisi katika tendo la ndoa) kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Kutimiza Mahitaji ya Mwenza Wake.

Tendo la ndoa siyo kwa ajili ya Mwanaume pekee, bali ni ushirikiano wa pande mbili. Mwanamke anapohitaji kupokea upendo wa kimwili, anatarajia Mwanaume wake awe tayari, mwenye juhudi na aweze kumridhisha kihisia na kimwili.

Mwanamke huhitaji Mwanaume mwenye ushirikiano, siyo mwenye uvivu au asiyejali kuhusu hisia zake na kwa namna anajisikia pale anapo hemkwa.

Kiuno chepesi humaanisha Mwanaume yuko tayari kujituma kwa upendo katika tendo hilo na kuhakikisha Mwenza wake ana deliver kwenye swala la hisia.

2. Kudumisha Furaha ya Mahusiano.

Kwenye mahusiano ya muda mrefu, tendo la ndoa lina nafasi kubwa ya kudumisha ukaribu wa kihisia, matokeo ya Mwanaume kuwa na Stamina na mwenye kiuno chepesi:

👉 Hupunguza kwa kiasi kikubwa sana matatizo ya migogoro ya ndani katika ndoa au uhusiano wao wa Kimapenzi au familia.

👉 Husaidia mwenza wake kuhisi anapendwa, kuthaminiwa na kuridhika ama kulidhishwa kihisia zaidi.

3. Kujenga Afya ya Kihisia na Kimwili.

Mwanaume mwenye uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa juhudi (kiuno chepesi) pia hunufaika Ki-Afya kwanini hunufaika Ki-Afya?.

👉 Huimarisha mzunguko wa damu.
👉 Husaidia kuondoa msongo wa mawazo.
👉 Huongeza uwezo wa kumudu mwenza Kihisia.

4. Kuepuka Kukataliwa au Mwenza Kutafuta Mbadala.

Mara nyingi, ukosefu wa bidii katika tendo la ndoa unaweza kumfanya mwenza kuhisi anapunjwa au kutopata haki yake ya msingi ya ndoa, hali hii huongeza hatari ya penzi kuisha.

Mfano...

👉 Mpenzi kuwa na hisia za kutosheka nje ya ndoa (kama halidhishwi) ndani kutamfanya kutafuta mbadala.

👉 Uvivu wa Mwanaume kutasababisha kupungua kwa Mapenzi ya ndani ya ndoa au uhusiano hivyo Mwanaume unapaswa kuwa imara.

5. Chachu ya Asili ya Mvuto wa Kimaumbile.

Mwanaume ndiye aliyepewa jukumu la uongozi katika tendo la ndoa kwa kawaida ya maumbile, hivyo basi..

Kiuno chepesi humaanisha Mwanaume yuko tayari kuchukua nafasi ya uongozi wa tendo hilo bila kumchosha mwenza wake.

Fuata notes hii 👇

Mwanaume kuwa na kiuno chepesi sio suala la mzaha bali ni sehemu ya kumjali, kumridhisha na kumheshimu mwenza wake.

Ni njia ya kudumisha furaha, ukaribu, na Afya ya kimapenzi katika uhusiano wowote wa ndoa zingatia sana maelekezo haya.

Asalamalekhum
Bwana wetu Yesu Asifiweee
Hi my follower

5E909E50-0027-4990-AD91-5243018DA024.jpeg
 
Back
Top Bottom