chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,369
- 27,786
Habari wanaMMU.
Wanaume wamekuwa na tabia ambayo huenda hawajajua madhara yake au hawajafahamu nini matokeo ya kile wanachokuwa wanakifanya kwa wakati husika huko mbeleni.
Inatokea anakuwa na mahusiano na mwanamke/msichana na katika hayo mahusiano wakati mwingine anakuta amemdhalilisha mwanamke kiasi kwamba thamani ya huyo mwanamke inakuwa imepotea katika jamii yake.
Kwa mfano, unampiga mwanamke picha za uchi na kuzisambaza mitandaoni.
Wakati mwingine unamuingilia kinyume na maumbile na baadaye unaamua kumuanika mitandaoni kwa sababu ya kutofautiana kwenu.
Huyu mwanamke uliyofanyia huu uchafu sasa inafikia wakati anapaswa kuwa mke wa mtu na kuzaa watoto,
Jiulize hii laana ya kumtia doa mwanamke ambaye hukuwa na mpango nae kimaisha anaibeba nani maana ni kwamba mwanaume mwenzako unakuwa umemtwisha msalaba usiomuhusu.
Hakika hii LAANA itakufikia.