Bado hujaumizwa!
Wenzio tulishapita huko,
Usidhani mtu anapenda kuwa na relationship mbili au tatu,
Inafika kipindi Moyo huna Majibu kila unayeonana naye, huelewi unampenda au anakupenda upo upo tu,
wapo waliosomesha wakaachwa wakajiua,
wapo waliozalishwa wakatemwa kama Big G,
Wapo waliong'ang'ania miaka na miaka baadaye kaolewa mwingine,
wapo waliotunza sana mademu zao kumbe demu anamchuna anakwenda tumia na wengine halafu nje anasema lile liboya nalilia pesa zake,
Mapenzi hakuna Bongo,
Mapenzi Ulaya, Afrika Biashara.
Kama siyo Biashara haiwezekani Msichana akienda kutambulisha kwao cha kwanza bwana anafanya kazi gani, amejenga au amepanga?? Maswali haya yamekaa kama fursa.
So Usiumize sana kichwa juu ya Mapenzi,
Tunza Sana Afya yako Maana ndiyo hukufanya utabasamu kila unapoiona asubuhi mpya,
Mengine yachukulie poa tu.