Mwanaume halisi hatukutegemei uyafanye haya

Mwanaume halisi hatukutegemei uyafanye haya

Tanganyikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
1,160
Reaction score
364
Kama tittle inavyojieleza Mwanaume kufanya yafuatayo haipendezi:-

1) Kuwa mbeya au kushiriki umbea kwa namna yoyote aidha kwa kukusudia au kwa kutokusudia.

2) Kutumia maneno haya:-

Shosti/Shostito, My, Mie, Mwaya, Nimekumisije, Msyuuuu...,My Maa, Ptuuuuu...., Utantaka,haalooo, jamaani n.k

3) Kutumia hela na Mwanamke yeyote au Mpenzi wako au Kumhonga kisha kulalamika mbele ya Wanaume wenzio. Sasa si ulienjoy naye,sisi tukusaidiaje? (Hapo Unajichoresha)

4) Kutamka neno "Nimeshindwa" au "Siwezi" mbele ya mwanamke...ni bora useme "Nitalishuhulikia" haijalishi unaweza au huwezi hilo suala.

5) Kulalamika kupita kiasi au kuweka kitu rohoni muda mrefu, (haipendezi pia kwa dume). Kama umekerwa Tunasemaga tu kavukavu.

6) Kuomba ushauri wa kitoto toto. Mfano,kitu kidogo unachoweza kushuhulikia ukiomba ushauri ni kujishusha na kujidharau.

7) Kuwa Mnafiki, mfano unajua kabisa chama flan kina unyonyaji na maovu na unashabikia kisa una maslahi bila kusimamia ukweli.
 
No. 7 umenena. Kuna watu wanajitoa fikra utafikiri wanawake. Jinga sana
 
7) Kuwa Mnafiki, mfano unajua kabisa chama flan kina unyonyaji na maovu na unashabikia kisa una maslahi bila kusimamia ukweli.

aisee!, kwaiyo, chama kile kuna kina mama zaidi wakipiga umbea.
inakuaje kwenye mzania huu mtu anaposhabikia prof. muongo, chenge au asiye muadilifu yoyote hata kama kahama chama kwenye macho ya watanzania?
 
Bora umewakumbushe.....maana wenginee khaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom