Mwanaume epuka haya makosa uishi maisha marefu

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Ni kawaida yangu kushauri wanaume wenzangu kuhusu mambo yanayohusu mahusiano na mapenzi.

Hua nasikitika sana kuona mwanaume mwenzangu anateseka au nasikia amejiua kwa sababu ya mapenzi. Najihisi mwenye hatia labda sikutimiza wajibu wangu wa kushauri, labda ushauri wangu ungeweza kumfikia akachukua maamuzi tofauti.

Ushauri wangu kwa wanaume wenzangu.

1. Usiwe na mwanamke mmoja. Huu hua nauita ukweli mweusi au ukweli mchungu. Watu wengi wanafiki hawawezi kulisema hili, sisi tusio wanafiki hulisema hili kila mara. Ni kosa kubwa sana mwanaume kua na mwanamke mmoja na mmoja pekee. Huyu mwanamke siku akifanya tofauti na matarajio yako unaweza kujiua. Acha ajinga wa mke/mpenzi mmoja, utakufa kabla ya muda wako.

2. Usimuamini mwanamke. Kosa lingine kubwa wanaume tunafanya ni kumuamini mwanamke, mwanamke pekee unaetakiwa kumuamini ni mama yako, wengine wote usiwaamini 100% kumuamini mwanamke ni sawa na kuamini utashinda kwenye kamali, ikitokea umeshinda haina shida ila usiposhinda utajuta. Usicheze kamali na mwanamke.

3. Usimpe mwanamke moyo wako. Kosa kubwa ambalo wanaume wengi hufanya ni kumwamini mwanamke na kumpatia mioyo yao. Hili ni kosa kubwa. Mwanamke mpe hela kadri uwezavyo ila usimpe moyo wako. Moyo wako usiuchezee bahati masibu, utakuja kujiua au kuua mtu ukateseke jela. Kitu pekee cha kumpa mwanamke ni hela sio moyo. Linda moyo wako kwa gharama yoyote. Moyo wako ndio maisha yako. Kumpa mtu mwingine maisha yako ni utaahira.

4. Usisomeshe mchumba. Kosa kubwa wanaume wanafanya ni kumuamini mwanamke hadi kufikia hatua ya kumsomesha. Kazi ya kumsomesha ni ya wazazi wake sio yako, usibebe jukumu la wazazi wa mwanamke. Labda kama unafanya hivyo bila kutegemea chochote toka kwake. Usijifanye mbadala wa wazazi wake, wewe ni mume au mpenzi tu na hakuna zaidi ya hapo.

5. Usiache mwanamke. Vijana wengi hudhani kuacha mwanamke ni sifa. Unakuta mtu anajisifu mimi sijawahi kuachwa, naacha tu, ujue huyo hana akili kabisa. Mwanaume hupaswi kuacha mwanamke. Hata kama hupendi na humtaki usimtamkie live sikupendi na sikutaki, wewe muache kwenye dormant state au sleep mode, ipo siku utapata dharula utaenda kuamsha. Ila ukimuacha jua umeformat disk, siku ukipata dharula hupati kitu. Usije kuthubutu kuacha mwanamke. Muache akuache yeye. Na hata ikitokea ukaenda kumuhitaji inakua ni rahisi kwako maana alikuacha yeye wewe hujamuacha.

Mada itaendelea.
 
Mada kuhusu wanawake kuwa na tabia za kuwaumiza wanaume zitakwisha pale tu watakapobadilisha hizo tabia tajwa.
 
kwenye uziii huu hawatokuja wamenyuti sana ila waache tabia za ovyooo
 
Umenena mkuu, ikiwezekana tuwasiliane na Ndalichako hii Mada iingizwe kwenye mitaala ya secondary school Kama somo ili kuokoa roho za wanaume tulio wengi.
Kwa Id Yako mkuu ww uko salama kabsa
 
Back
Top Bottom