Ingawa haikuzoeleka, hakuna cha ajabu. Mara nyingi ikiwa mwanamke kakutongoza ni kuwa mnafahamiana kabla, ingawaje zipo kesi za "love at first sight". Mwanamke anapokutongoza atakuwa amejiamini hata kukukabili, na zaidi kwa kukuhisi kuwa unaona haya kiasi huwezi kuanza wewe. Na ikiwa huna majukumu (unaye wako tayari), kubali bila ya kusita, sio kwa sababu ya kumhurumia au kwa sababu umejiona umepata cha bure na ukaanza kujipandisha chati. Ikiwa humtaki kwa dhati bora urudishe majeshi nyuma. Dhambi itakuwa kumkubalia kutaka kutumia fursa baadaye ukamwacha. Hili sikushauri.