Mwanaume amemng'ata mke wake sehemu za siri

Mwanaume amemng'ata mke wake sehemu za siri

Kuna Jirani yangu kafanya jambo ambalo sijawahi kutarajia. Ni mtu tunakaa karibu hatujazoeana lakini salamu za haste haste huwa tunapeana halafu kila mtu na time zake. Leo nimegongewa mlango asubuhi mno, kuamka na kutoka nje, nikakutana na vitoto viwili vifupi, I guess, aged 4 - 5 years. Vikanisalimia shikamoo! Marahaba, nikaitikia.

Mmetumwa nini watoto wazuri? Mama anakuita, vikaitikia! Nyie ni watoto wa nani? Mnaishi wapi? Watoto wa Baba, tunakaa pale, kimoja kikanionyesha kwa mkono. Nikawauliza mama yupo na nani? Mwenyewe, kimoja kikaitikia. Na baba? Hayupo, wakaitikia wote.

Ndipo nilipowaambia tangulieni mwambieni nakuja.

Nilipofika kwenye hiyo nyumba sikuingia ndani. Muda si muda nikaona msichana mmoja anatoka (nahisi ni hg), halafu nikamwambia nimeambiwa naitwa na mama wa hii nyumba, naomba umwambie aje hapa nje. Akaniambia karibu tu ndani. Nikamwambia samahani, naomba umwite namsubiri hapa (niingie ndani sijui lolote wala kinachoendelea huko, thubutu).

Yule mama akawa amekuja, akanisalimia. "Kaka samahani, mtu unapopata shida jirani yako ndio msaada namba moja, nimepata shida kakangu". Nikamwuuliza shida gani dada! Pole. Ni aibu hata kukuambia, huku akilia na kuinama (karibu nichomoke, maana niliona kama ni so huku asubuhi sana).

Alivyoona nina wasiwasi na naweza kusepa muda wowote, akaniambia "nimeng'atwa sehemu za siri na mme wangu kufuatia ugomvi uliotokea usiku na nimeumia vibaya, sasa naomba ushauri, niende polisi kuchukua Police Form 3 (PF3 kwa ajili ya matibabu au nifanyeje?". Ebo, kusikia hivyo nikamwambia ngoja nije nimeacha mlango wazi!

Nilijiuliza maswali kadhaa bila majibu. Ndipo nikamwendea mama mmoja naye ni jirani, anaonekana ni mtu mwenye busara. Nikamwambia mama nakuomba nenda ile nyumba, maana kama vile mama mwenye nyumba ana shida ukamsikilize. Mama huyo alinihoji maswali mengi, lakini sikumwambia kuhusu shida, isipokuwa nilimwambia watoto wamekuja hapa kwangu kutoka hiyo nyumba, wameniambia mama anakuita, nahisi alikuwa anahitaji mtu mwanamke ndio maana nakuomba ukamsikilize.

Baada ya hapo, nilijiandaa na kutoka kwenda kazini, kurudi ni mpaka jioni. Kwa kweli sijaweza kumpa wala sikuwa katika mood ya kumshauri maana niliogopa kwa sababu ushauri ambao ningeutoa ilikuwa ni kumsaka yule jamaa na kumweka ndani kwanza. Nimejaribu kuwaza hatma yao na ya watoto nikaona bora tu nisepe.

Ndugu zangu, hivi ni ugomvi gani huo mpaka mwanaume umng'ate mwanamke sehemu za siri? Hivi kuna uwezekano kwamba wanawake wanafanyiwa mambo mabaya sana na wanaume lakini hawawezi kuyasema.

Nikashauri nini iwapo nitahitajika tena? Ingawa nitajitahidi kukwepa nisionane naye wala yule mama mwingine niliyemwambia aende kadri nitakavyoweza? Sitaki kujiingiza kutoa ushauri, maana akili zangu zinanipa alert kwamba nitavunja hiyo ndoa!

Watu wenye tabia kama hizi acheni uharamia aisee. This is the most ridiculous scenario ever I have ever encountered! Ni kitu cha ajabu sana kama 7-1!

Please guys, stop doing this!

mmmmh hizi fiksi balaa yaani mtu awe na ugomvi na mkewe hafu amng'ate sehemu za siri mbona haiji kijana
 
najiuliza mengi hapa
  1. huyo jirani alikufahamu kiasi gani hadi athubutu kuomba msaada kwako
  2. jirani yako huyo hakufahamu uwepo wa huyo mama mwingine hadi afikie maamuzi ya kukuita wewe (mwanaume)?
#MlikuwNaYenu #
 
sasa wewe unakimbia badala umwambie akuoneshe alivyoumia? na je vp kile kimboga chenye chumvi na maji kilitoka au kipo? maana kile muhimu kweli.
 
Back
Top Bottom