CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,828
- 1,862
Habari za Jumapili wana JF?
Ni story ya kusogeza weekend.
Sio Tanzania ni huko Zimbabwe.
Mwanaume mmoja alifiwa na rafiki yake kipenzi ambaye pia ni jirani yake. Walikuwa na urafiki wa karibu sana lakini hata hivyo kumbe huyo rafiki yake alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa huyu jamaa.
Hata hivyo lakini hakuweza kujua kwa kuwa walijitahidi kuficha siri hadi kifo kilipompata huyu swahiba wa jamaa. Sasa aligunduaje wakati mgoni wake tayari kaishakufa? Mapenzi yaache tu yaani.
Wakiwa msibani na mkewe, uchungu wa moyo aliokuwa nao mke kwa kufiwa na mpenzi wake ulikuwa hauvumiliki. Mke alilia sana kwa uchungu hadi jamaa akatilia shaka kuwa hiki kilio sio cha kumpoteza shem kuna jambo nyuma yake.
Basi mme akamchukua mke chemba akaanza kumuuliza sababu ya kuumizwa kiasi kile na kifo cha shem wake. Mke akasema ameumia sana lakini jamaa akambana zaidi ndio akakiri kuwa alikuwa mpenzi wake.
Basi mume akafura kwa hasira akaelekea msibani na kurusha matusi kwa wanandugu wote na kutaka aone maiti. Alipata hasira kuwa kagundua jambo hilo wakati mgoni ameishakufa alitamani angepambana naye ana kwa ana lakini ndio hivyo kwa hiyo alipoifikia maiti akatembeza kichapo kwa maiti ile hadi aliporidhika.
Kwa matusi yake na kitendo cha kudhalilisha maiti alikalishwa na mahakama ya kimila. Akawaeleza yote yaliyojiri lakini wakampiga faini ya ng'ombe 3 kwa kutukana watu wasio na hatia.
Man assaults wife lover’s corpse