Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,504
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imelalamikiwa kuwa inaendekeza vitendo vya rushwa katika utoaji haki.
Akizungumza baada ya kuachiliwa huru Williamu Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Leornaed Swai Mwanasheria wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) amesema kuwa rushwa katika mahakama ya Kisutu inatisha.
Swai ametoa tuhuma hizo baada ya Hakim Hellen Liwa kusoma hukumu kwa niaba ya Kyey Rusema ambapo iliamriwa kuwa mahakama imemuona Mhando hana hatia.
Mahakamaa imeeleza kuwa hakuna ushahidi ilionyesha kuwa Mhando alitumia madaraka yake vibaya kutokana na mkataba wa TANESCO kuipa zabuni ya mkewe kampuni ya Santa Clara, na pia yeye hakuhusika kwenye kutoa zabuni kwa kuwa zabuni hutelewa na bodi ya zabuni.
Source: Mwanahalisi