Mwanasheria wa CCM achukua fomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanasheria wa CCM achukua fomu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 27, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Amon Mtega,

  Songea


  MWANASHERIA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka makao makuu Dodoma, Glorious Luoga, amejitosa kuchukua fomu ya kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC).

  Luoga anawania nafasi hiyo kupitia Wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, huku akiwataka wananchi mkoani hapa kuona umuhimu wa kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo.

  Hayo aliyasema juzi wakati akichukuwa fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Ofisi ya Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini.

  Luoga alisema, kila mwananchi ana wajibu wa kimsingi kuhakikisha kuwa, anachangia shughuli za maendeleo katika eneo analoishi na kuachana na tabia ya kupenda kuchangia harusi.

  Alisema wilaya hiyo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo shule za sekondari za kata ambazo nyingi zimekuwa hazina maabara, walimu, vitabu pamoja na madawati.

  "Lengo langu la kuchukuwa fomu nikuja kuunga mkono jitihada zilizofanywa na wezee wangu pamoja na Serikali ukizingatia wilaya yetu inachangamoto nyingi.

  "Hizi changamoto utatuzi wake sio lazima zikasemewe bungeni kwani mkongojo wa wazee hupokelewa na vijana," alisema Luoga.

  Luoga alisema CCM bado inanguvu kubwa na mfumo wake ni mzuri wa kupambana na vyama vingine vya siasa ambavyo vimekuwa vikijitahidi kujaribu kutaka kukichafua lakini watu wengi wenye uelewa wamekuwa wakikiamini.

  Luoga alisema mfumo wa kujivua gamba katika chama hicho ulikuwa na lengo la kukisafisha chama na si vinginevyo, kama baadhi ya vyama vya upinzani vinavyodai kuwa kumejaa mafisadi.

  Toa Maoni yako kwa habari hii


   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Haisaidii kitu
   
 3. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Amefundishwa na PalaMAGAMBA Kabudi!

  Jamani, si kila aliyesoma sheria ni mwanasheria. Wengine wana LLB na hawajawahi kukanyaga kwenye mlango wa mahakama. Kuna rafiki yangu ana LLB lakini ni mfugaji mzuri wa kuku huko Kitunda, na hakumbuki kifungu hata kimoja cha sheria.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tehe tehe tehehe hehehe heeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Kashaijabutege ni kweli hilo ulisemalo, huyo Luoga alikuwa anafanya kazi BRELA baada ya kutumiwa na mafisadi kuregister vikampuni uchwara ndio wamempa kazi hapo CCM, huyo hata mlango wa Mahakama hajui unafafanaje na hata hiko cheti cha sheria ni yale masomo yetu ya jioni ndio aliyopitia yeye.

  2010 Aliujaribu moto wa Makangoro Mahanga kwenye kura za maoni za CCM ubunge wa Segerea akamsambaratishia mbali ndio maana hata hii NEC kakimbilia Songea ndio labda Mama yake mzazi anaweza kumsaidia maana mama yake ni Gamba zoefu linalojulikana kule Songea.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Wanasheria tumbo hawa, wangekuwa real wasingekuwa sehemu ya magamba
   
Loading...