Mwanasheria Mkuu wa TBS kortini kwa mashtaka ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kibali

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
court.jpg

Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali.

Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay amemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hati ya mashtaka, Mlay alidai kuwa Mei 19, 2017 huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Marco akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.

Marco katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.

Katika shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).

Wakili Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa hadi Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: Mpekuzi
 
Kuna raia mmoja wa nchi jirani anatumia passport ya Tanzania! Uhamiaji ina tatizo sana, tena huyo wa TBS amejulikana kwa sababu alikuwa kwenye nafasi ya juu. Raia wa kigeni ni wengi nchini kwa kuwa ufuatiliaji ni hafifu, kuna raia wa kigeni wanafanya udalali wa kuuza viwanja na hilo lilibainishwa na mdau mmoja hapa jf.
 
Hakika maajabu hayaishi Tanzania! Aliwezaje kupata ajira serikalini na kupanda ngazi mpaka kufikia level ya kuwa "Mwanasheria mkuu" wa taasisi ya serikali???
Maajabu hayaishi
Ina maana vetting haikufanyika kuhakikisha kuwa ana kila kitu kinachomruhusu kuajiriwa
Issue za shule alikosoma au alitokea wapi kabla
Mpaka kuwa mwanasheria waa taasisi ya umma kubwa kama TBS na sio raia
Je ni mangapi ameyavujisha nje akiwa mwajiriwa wa taasisi
 
Kuna raia mmoja wa nchi jirani anatumia passport ya Tanzania! Uhamiaji ina tatizo sana, tena huyo amejulikana kwa sababu alikuwa kwenye nafasi ya juu. Raia wa kigeni ni wengi nchini kwa kuwa ufuatiliaji ni hafifu, kuna raia wa kigeni wanafanya udalali wa kuuza viwanja na hilo lilibainishwa na mdau mmoja hapa jf.
Mkuu niliwahi kutoa taarifa polisi kwa ishu kama hiyo walinijibu vibaya sana nilitamani niwafanye mbaya ila nikawapotezea police,uhamiaji,ccm ni matatizo tupu
 
Wakati NIDA ilipopanguliwa kwa nguvu na watu kupewa kesi nikajua sasa vitambulisho vitatoka kwa kasi,lakini tangu jamaa wapigwe na kesi kimyaaaa,hakuna cha vitambulisho wala nini!

Mwanasheria Mkuu wa shirika la viwango Tanzania kapandishwa mahakamani akidaiwa kuwa mrundi!

Wako waCongo,waganda,wakenya,Wanyarwanda wangapi wanakula bata ngazi za juu?

Vitambulisho vimekwama wapi? NIDA ya wale tulioambiwa wameiba walau walishaanza kutoa vitambulisho,hawa mbona hawatoi
IMG_20170607_183417.png
 
Back
Top Bottom