Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Rais Magufuli hana mamlaka ya kuingilia mambo ya Zanzibar

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema Rais John Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar ukiwamo uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20.

Hii ni kauli ya pili kutolewa ndani ya wiki moja ikieleza hali hiyo, baada ya ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Luvuba aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam.

Amesema: “Katiba ya Zanzibar si ya Muungano, masuala ya ulinzi na usalama ndiyo ya Muungano na ndiyo sababu ulinzi umeimarishwa visiwani humo kuhakikisha nchi hiyo inakuwa salama."

Alitoa kauli hiyo wakati akifafanua mambo mbalimbali yaliyozungumzwa na wabunge wakati wa mjadala Bungeni.

Tangu kuibuka kwa mgogoro Zanzibar watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakisema mwarobaini wa mgogoro huo kwa kutumia jitihada za ndani, ufanywe na Rais Magufuli baada ya jitihada za viongozi wa kisiasa visiwani kukwama.

Mgogoro huo, ambao umekuwa kawaida kuibuka kila baada ya Uchaguzi Mkuu, uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo Oktoba 28 na baadaye kuuitisha upya, kitendo ambacho CUF inakipinga.

Tangu wakati huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na marais wa zamani wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume wamekuwa kwenye mazungumzo ambayo hayakuzaa muafaka.

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua uwepo wa Serikali mbili. Hizi Serikali uwepo wake ni Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar. Ukisoma Ibara ya nne ya Katiba si tu kwamba inaweka mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu ya Dola, bali inaweka mgawanyo wa madaraka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.”

Ibara ya 4 ya Katiba inasema (1) Shughuli zote za Mamlaka ya nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na mambo ya Muungano kama alivyoorodheshwa katika nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.

(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

Masaju alisema Katiba ya Zanzibar ndio inayozaa ZEC.

“Kile ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga Serikali moja,” alisema.

Alisema kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Muungano na ya Zanzibar na Serikali haiwezi kufanya hivyo.
 
Rais wa JMT ana mamlaka ya kikatiba kudhibiti mambo yote au dalili zote zinazoweza kuhatarisha amani sehemu yoyote ya Muungano. Kufuta na kurudia uchaguzi bila sababu za msingi ni kuhatarisha amani!
Hata hivyo, kwa watu wenye busara, hoja siyo kukosa mamlaka bali ni uhalali wa kinachofanyika!
Ni ujinga kusema Rais hana mamlaka hata kama amani itatoweka.
Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu hayana mipaka ndani ya nchi yake.
Ifike wakati sasa, wasemaji wa serikali wachaguliwe watu wenye uwezo wa kufikiri kiujumla na siyo usomi wa vyeti!
 
Naona povu linakutoka kijana...ndiyo maana hukuchaguliwa wewe hiyo post... pole sana kapange foleni ya uchaguzi march 20 au Maalim ameshasema..hahahahaa
 
Hii nchi haieleweki ni kasa jike au shoga ?
Kwani ZEC inawajibika kwa nani ? Kibaraka Sheni..
Kibaraka Sheni kinawajibika kwa nani ?
Kwa rais wa nchi..
ni sawa tu na halmashauri..
mtumishi aliekabidhiwa dhamana hawajibiki kwa rais anawajibika kwa mkurugenzi au katibu mkuu,ambae ndie huwajibika kwa rais..
na maagizo ya rais hayaendi moja kwa moja kwa mtendaji au mtumishi,yanaenda kwa yule anaewajibika kwake,ambae yeye ndio hushusha rungu.
 
Yaani huu Muungano ni kama Pilau kwenye bunge la katiba Tanzania ni nchi moja kwenye Jecha na Zec Bara hawana mamlaka ya kuingilia ya Zanzibar na lolote likitokea Zanzibar aendelee kukaa kimya ,tusisikie amepeleka JWTZ huko
 
Mkapa alipotumia jeshi kufanya mauaji ya wanzanzibar waliokuwa wanaandamana kuhusiana na uchaguzi wa 2010 alikuwa anatumia katiba gani?
Maps kama Rais wa JMT anawajibika kwa mambo ya Muungano. Fuji na vita na mambo ya Muungano.
 
AG Masaju ana kazi ngumu sana ya kutetea profession yake katikati ya wanasiasa. Vipengele vya katiba alivyovinukuu ni sahihi hususan kwa minajili ya kumtoa Magu kwenye kimeo hicho, zigo kwa CCM.
 
Rais wa JMT ana mamlaka ya kikatiba kudhibiti mambo yote au dalili zote zinazoweza kuhatarisha amani sehemu yoyote ya Muungano. Kufuta na kurudia uchaguzi bila sababu za msingi ni kuhatarisha amani!
Hata hivyo, kwa watu wenye busara, hoja siyo kukosa mamlaka bali ni uhalali wa kinachofanyika!
Ni ujinga kusema Rais hana mamlaka hata kama amani itatoweka.
Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu hayana mipaka ndani ya nchi yake.
Ifike wakati sasa, wasemaji wa serikali wachaguliwe watu wenye uwezo wa kufikiri kiujumla na siyo usomi wa vyeti!
Wewe ndio uwe nanuwezo wa kufikiri.
Unachokisema wewe cha uvunjifu wa amani nintofauti na kutoa maamuzi kuhusu uchaguzi.
Iwapo kama kutakuwa na uvunjifu wa amani, basi hapo atakuwa na mamlaka ya kutunza amani. Na ndio maaana kuna majeshi na polisi kibao kule ili kuhakikisha kuna amani ambayo labda wewe na wenzio mna mpango wa kuivunja.
Yeye hawezi kuingilia uchaguzi, hivyo wenyewe watu wa zazibar ndio wanaotakiwa kumalizana, tena kwa amani kabisa. Bila kujali, kama kurudiamuchaguzi, au kuhesabu upya, au kumtangaza wanayeona alishinda au vyovyote vile, watajuwa wazanzibar wenyewe.
Ila kama mtashindwa kufika muhafaka kwa amani, na kukaonekana kuna dalili ya uvunjifu wa amani, hapo sasa Raisi ana mamlaka ya kuhakikisha kuwa amani inalindwa kwa either majeshi aunpolisi.
Think objectively but not subjectively kijana. Taifa hili letu, na linatuhitaji wote. Kuna maisha ya kesho kaka.....
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema Rais John Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar ukiwamo uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20.

Hii ni kauli ya pili kutolewa ndani ya wiki moja ikieleza hali hiyo, baada ya ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Luvuba aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam.

Amesema: “Katiba ya Zanzibar si ya Muungano, masuala ya ulinzi na usalama ndiyo ya Muungano na ndiyo sababu ulinzi umeimarishwa visiwani humo kuhakikisha nchi hiyo inakuwa salama."

Alitoa kauli hiyo wakati akifafanua mambo mbalimbali yaliyozungumzwa na wabunge wakati wa mjadala Bungeni.

Tangu kuibuka kwa mgogoro Zanzibar watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakisema mwarobaini wa mgogoro huo kwa kutumia jitihada za ndani, ufanywe na Rais Magufuli baada ya jitihada za viongozi wa kisiasa visiwani kukwama.

Mgogoro huo, ambao umekuwa kawaida kuibuka kila baada ya Uchaguzi Mkuu, uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo Oktoba 28 na baadaye kuuitisha upya, kitendo ambacho CUF inakipinga.

Tangu wakati huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na marais wa zamani wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume wamekuwa kwenye mazungumzo ambayo hayakuzaa muafaka.

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua uwepo wa Serikali mbili. Hizi Serikali uwepo wake ni Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar. Ukisoma Ibara ya nne ya Katiba si tu kwamba inaweka mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu ya Dola, bali inaweka mgawanyo wa madaraka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.”

Ibara ya 4 ya Katiba inasema (1) Shughuli zote za Mamlaka ya nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na mambo ya Muungano kama alivyoorodheshwa katika nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.

(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

Masaju alisema Katiba ya Zanzibar ndio inayozaa ZEC.

“Kile ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga Serikali moja,” alisema.

Alisema kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Muungano na ya Zanzibar na Serikali haiwezi kufanya hivyo.

Huyu Ni Mwanasheria Mkuu au Mwanapropaganda Mkuu, Rais Ni Amirijeshi Mkuu na aliapa kulinda Katiba ya Nchi, Taifa Zima la Tanzania na Pia aliapa Kulinda amani ya Nchi, Iweje Amnyamazie "Mtu mmoja" Jecha aliyetumwa na Kikwete na Mkapa Kufuta "Matokeo ya Uchaguzi" wa Zanzibar? Maana uliofutwa sio Uchaguzi, Uchaguzi Ulishafanyika matokeo yashabandikwa kwenye Kuta za Vituo.
 
Ina maana hivi vyuo vyetu vinazalisha wasomi sampuli hii....naona tumekwisha...kwa hali hii bora nikose hiyo elimu..
 
Sasa kama Magufuli hana mamlaka na huo uchaguzi wa Zanzibar Maalim Seif na Shein walikuwa wanapishana kule ikulu kumpa taarifa gani Magufuli kuhusu maongezi waliyokua wanaongea?
 
Wewe ndio uwe nanuwezo wa kufikiri.
Unachokisema wewe cha uvunjifu wa amani nintofauti na kutoa maamuzi kuhusu uchaguzi.
Iwapo kama kutakuwa na uvunjifu wa amani, basi hapo atakuwa na mamlaka ya kutunza amani. Na ndio maaana kuna majeshi na polisi kibao kule ili kuhakikisha kuna amani ambayo labda wewe na wenzio mna mpango wa kuivunja.
Yeye hawezi kuingilia uchaguzi, hivyo wenyewe watu wa zazibar ndio wanaotakiwa kumalizana, tena kwa amani kabisa. Bila kujali, kama kurudiamuchaguzi, au kuhesabu upya, au kumtangaza wanayeona alishinda au vyovyote vile, watajuwa wazanzibar wenyewe.
Ila kama mtashindwa kufika muhafaka kwa amani, na kukaonekana kuna dalili ya uvunjifu wa amani, hapo sasa Raisi ana mamlaka ya kuhakikisha kuwa amani inalindwa kwa either majeshi aunpolisi.
Think objectively but not subjectively kijana. Taifa hili letu, na linatuhitaji wote. Kuna maisha ya kesho kaka.....

Kitendo cha kufuta na kurudia uchaguzi bila sababu za msingi ni kuhatarisha amani!
Narudia tena, kwa mwenye uwezo mzuri wa kufikiri, huwezi kusema Rais ana mamlaka tu ya kuingilia hatari itakatokea na hawezi kupambana na kisababishi!
Hoja ingekuwa kwamba, kinachofanyika ni halali kwa mtazamo wa Rais na hivyo hana sababu ya kuingilia kwa sasa!
Kujificha kwenye kichaka cha kutunga tu kuwa hana mamlaka hata kama kinachofanyika hakina uhalali ni makosa makubwa!
 
AnO uwezo wa katiba kuhakikisha hatumii majeshi y muungano kuwaweka ccm zanzibar kwa nguvu.....yeye ndie mwanye majeshi na askari na ndio waloharibu kila kitu.
Kama ni kikwete au nani lakini wao ndio waloleta matatizo kwa kulea mafisadi znz na kuuweka utawal wa kiimla usokubalika.
Watu wanajaribu kumtoa ili ionekane hilo tatizo si la muungano ili kujivua na a chill na kimataifa.
Lakini hili ni lake kama mwanasheria mkuu halitaki basi bora tugawane mbao..nini faida ya huu muungano kama kazi kuu ni kuwalinda vibaka wa democrasia znz?

Hili linamhusu kwa sabBu ndio chimbuko la tatizo.
Siku ile ya matangazo askari wa muungano wangefanya kazi yao kwa haki leo tusingefika hapa....ila ni vyombo vya muungano ndio vimeleta vurugu kulazimisha lazima ccm itawale milele znz.....huu ni mwiba wa samaki mpevu hauwezi kutoka dunia imeona ubakaji ile wa democrasia kujinasua ni kumpa uhuru jecha aamue kwa hiari sio under siege
 
Jifupa hili ni la Magu na limesababishwa na Mzee wa Msoga. Halikwepeki.

Huu uongo hata shetani haukubali
 
Ninavyo Mimi magufuli hana washauri wazuri baadae atakuja juta wanamdanganya sasa kule Congo Ana mamlaka kupeleka jeshi au Burundi wanasheria wengine hata sijui wamesoma wapi inamaana hana uwezo wa kusuluhisha mgogoro wa Zanzibar lakini wa Burundi anao uwezo kweli huu muungano bora uvunjwe
 
Back
Top Bottom