VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kutokana na sakata la kikatiba lililopata tiba ya tabu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Mcheche Masaju; Waziri wa Sheria na Katiba Dr. Harrison Mwakyembe; Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kisheria na timu nzima ya washauri wa Rais wanapaswa kujiuzulu.
Rais hakupaswa kuucheza mchezo alioucheza wa kumteuwa Dr. Possi kuwa Balozi. Rais hakupaswa 'kusimangwa' na kuzungumzwa vile ikiwa amezungukwa na wasomi wengi tu wa Sheria, tena wenye jukumu la kumshauri na kumuongoza Rais kwenye mambo ya kisheria.
Pamoja na kwamba Dr. Possi, kwa kuteuliwa Ubalozi, ameshapoteza sifa za kuwa Mbunge hata kama hatajiuzulu rais hakupaswa kushiriki kwenye mchezo mgumu kama ule kama angeshauriwa vyema. Masaju, Mwakyembe na wengineo wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri mkuu wa mambo ya kisheria kwa Serikali inayoongozwa na Rais. Alikuwa wapi? Waziri Mwakyembe,mbobezi wa sheria, na Waziri mwenye dhamana ya kulinda Katiba na Sheria alikuwa wapi? Washauri wa pale Ikulu walikuwa wapi?
Lazima wajiuzulu au waondolewe. Hakuna namna nyingine.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)