Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Waziri wa Sheria na hawa wajiuzulu mara moja

Kutokana na sakata la kikatiba lililopata tiba ya tabu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Mcheche Masaju; Waziri wa Sheria na Katiba Dr. Harrison Mwakyembe; Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kisheria na timu nzima ya washauri wa Rais wanapaswa kujiuzulu.

Rais hakupaswa kuucheza mchezo alioucheza wa kumteuwa Dr. Possi kuwa Balozi. Rais hakupaswa 'kusimangwa' na kuzungumzwa vile ikiwa amezungukwa na wasomi wengi tu wa Sheria, tena wenye jukumu la kumshauri na kumuongoza Rais kwenye mambo ya kisheria.

Pamoja na kwamba Dr. Possi, kwa kuteuliwa Ubalozi, ameshapoteza sifa za kuwa Mbunge hata kama hatajiuzulu rais hakupaswa kushiriki kwenye mchezo mgumu kama ule kama angeshauriwa vyema. Masaju, Mwakyembe na wengineo wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri mkuu wa mambo ya kisheria kwa Serikali inayoongozwa na Rais. Alikuwa wapi? Waziri Mwakyembe,mbobezi wa sheria, na Waziri mwenye dhamana ya kulinda Katiba na Sheria alikuwa wapi? Washauri wa pale Ikulu walikuwa wapi?

Lazima wajiuzulu au waondolewe. Hakuna namna nyingine.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Unatamani na wewe ungekuwa Rais na maumuzi yako ya ki obvious uliyoyazoea. Urais haunogi kama unaamua amua ki obvious. lazima ufanye maamuzi magumu. Wengine muna utamaniiii, mara muigize eti mna wananchi wenu wanaowaita rais, mara mtangaze baa la njaa, kipindi kile kabla hamjahamia eti mlitangaza vita na Malawi. Kuna Rais mmoja tu mwacheni afanye kazi yake. Akikosea si ndio raha ili ninyi mje kushinda kirahisi? Vipi leo mnataka apatie ili iweje?
 
..Mtu sahihi wa kuwajibika ni mwanasheria mkuu wa serikali(AG).

Kuna siku bwana huyu alikwama bungeni mpaka January maropes akaokoa jahazi. Unapoona mwanasheria mkuu anaokolewa na layman tu, ndo utaelewa why mambo yanajiendea ndivyo sivyo
 
Ukweli ni kwamba Raisi anawashauri wake wanaomshauri juu ya nani amteue na nani asimteua sasa hao wanapaswa kuwajibika mara moja kwa aibu waliyomsababishia mtukufu wetu,AG na Waziri wa sheria watamshauri raisi tu pale wanaposhilikishwa juu ya teuzi ambazo raisi anakusudia kuzifanya hivyo sio sawa kuwaattack hawa watu wawili kabla hujaattack timu inayomshauri mh raisi

Kwa mfano huyo msemaji wake alipoletewa taarifa ya huo uteuzi angeweza kuangalia sheria zikoje kwenye suala lenyewe na kumshauri raisi badala ya kupeleka kila kitu hewani hata ambavyo havikidhi matakwa ya kisheria.

KIUKWELI HII IMEKUWA AIBU AMBAYO MTUKUFU ANAANZA NAYO MWANZONI MWA MWAKA 2017,TUNASEMAGA BUNDI KATUA MAGOGONI
 
LUMUMBA WAKO WAPI JAMA WAOKOE HILI JAHAZI?

Wamejificha wanasubiri upepo upite...kuna mmoja Jana kasema eti magufuli kama Pele kawanyamazisha wapinzani kwa kuteuwa Possi kuwa balozi....niliishia kucheka tu..
 
Ukweli ni kwamba Raisi anawashauri wake wanaomshauri juu ya nani amteue na nani asimteua sasa hao wanapaswa kuwajibika mara moja kwa aibu waliyomsababishia mtukufu wetu,AG na Waziri wa sheria watamshauri raisi tu pale wanaposhilikishwa juu ya teuzi ambazo raisi anakusudia kuzifanya hivyo sio sawa kuwaattack hawa watu wawili kabla hujaattack timu inayomshauri mh raisi

Kwa mfano huyo msemaji wake alipoletewa taarifa ya huo uteuzi angeweza kuangalia sheria zikoje kwenye suala lenyewe na kumshauri raisi badala ya kupeleka kila kitu hewani hata ambavyo havikidhi matakwa ya kisheria.

KIUKWELI HII IMEKUWA AIBU AMBAYO MTUKUFU ANAANZA NAYO MWANZONI MWA MWAKA 2017,TUNASEMAGA BUNDI KATUA MAGOGONI

Mkuu umeongea kitu nilikuwa najiukiza tangia jana...hv msigwa Kazi yake ni kutoa taarifa tu kama anavopewa na mkulu au na yeye huwa ana nafasi ya kuipima taarifa kabla hajaitoa??? Au hata kutafuta kidogo Ushauri kabla hajatoa taarifa nimekuwa najiuliza tu.
 
Inaonekana huyu mtu yeye anakumbuka kwenda hewani tu,atumii muda kuumiza hiki kitu kimekaaje, na yeye anawajibu wa kumshauri raisi japo sio jukumu lake rasmi, sema hawa jamaa wote wa awamu hii huwa hawasumbui kichwa kufikilia beyond the scope wao mkulu akisema wanafuata kama ilivyo
 
Ikiwa tunatakiwa kuelezea ukweli itatupasa tusema hivi "Rais ameteua wabunge nane, sita kati yao ni wanaume"

Haijalishi kama mmoja kajiuzulu au la. Waliteuliwa na wakatumikia position ya Ubunge.

Au mnataka kusema sasa anaweza kuteua hadi wakafika 11?

Na akiamua kumshinikiza mwengine ajiuzulu, atachagua mwengine wawe 12?

Ulichoandika ndo nimekuwa nikiamini hvo hamna jinsi inaweza badilisha ambacho ameshakifanya...akijidai anateua wanawake watano eti ili kutimiza matakwa ya katiba basi atakuwa ameteuwa 11 na sio 10 kama ambavo katiba inamtaka..

Nilisema Jana hapa mukulu "Karuka mkojo kakanyaga mavi" alichotakiwa kufanya ni kutengua uteuzi wa mmoja kati ya Bulembo au Kabudi maana kimsingi bado sio wabunge kwani hawajaapishwa..
 
Usikute Mwakyembe alikuwa anatafutiwa sababu ya kutolewa hapo kwenye sheria ,ngoja reshuffle ya baraza lije

Mwakyembe amepwaya kwenye hiyo wizara ya sheria na katiba na nitashangaa kama atabaki kwenye cabinet ; pengine kwasababu hakuna marupurupu kama yale aliyokokotoa kwenye wizara ya mabehewa ya treni!!
 
Kutokana na sakata la kikatiba lililopata tiba ya tabu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Mcheche Masaju; Waziri wa Sheria na Katiba Dr. Harrison Mwakyembe; Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kisheria na timu nzima ya washauri wa Rais wanapaswa kujiuzulu.

Rais hakupaswa kuucheza mchezo alioucheza wa kumteuwa Dr. Possi kuwa Balozi. Rais hakupaswa 'kusimangwa' na kuzungumzwa vile ikiwa amezungukwa na wasomi wengi tu wa Sheria, tena wenye jukumu la kumshauri na kumuongoza Rais kwenye mambo ya kisheria.

Pamoja na kwamba Dr. Possi, kwa kuteuliwa Ubalozi, ameshapoteza sifa za kuwa Mbunge hata kama hatajiuzulu rais hakupaswa kushiriki kwenye mchezo mgumu kama ule kama angeshauriwa vyema. Masaju, Mwakyembe na wengineo wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri mkuu wa mambo ya kisheria kwa Serikali inayoongozwa na Rais. Alikuwa wapi? Waziri Mwakyembe,mbobezi wa sheria, na Waziri mwenye dhamana ya kulinda Katiba na Sheria alikuwa wapi? Washauri wa pale Ikulu walikuwa wapi?

Lazima wajiuzulu au waondolewe. Hakuna namna nyingine.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Kama boss wao ni haambiliki, hashauriki wajiuzuru vipi? Pia yeye ndio anatakiwa aulize kabla ya kufanya chochote kile. sasa kama anakurupuka?
 
Inaonekana huyu mtu yeye anakumbuka kwenda hewani tu,atumii muda kuumiza hiki kitu kimekaaje, na yeye anawajibu wa kumshauri raisi japo sio jukumu lake rasmi, sema hawa jamaa wote wa awamu hii huwa hawasumbui kichwa kufikilia beyond the scope wao mkulu akisema wanafuata kama ilivyo

Wanasema eti mukulu ni mukali muno..
 
Kutokana na sakata la kikatiba lililopata tiba ya tabu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Mcheche Masaju; Waziri wa Sheria na Katiba Dr. Harrison Mwakyembe; Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kisheria na timu nzima ya washauri wa Rais wanapaswa kujiuzulu.

Rais hakupaswa kuucheza mchezo alioucheza wa kumteuwa Dr. Possi kuwa Balozi. Rais hakupaswa 'kusimangwa' na kuzungumzwa vile ikiwa amezungukwa na wasomi wengi tu wa Sheria, tena wenye jukumu la kumshauri na kumuongoza Rais kwenye mambo ya kisheria.

Pamoja na kwamba Dr. Possi, kwa kuteuliwa Ubalozi, ameshapoteza sifa za kuwa Mbunge hata kama hatajiuzulu rais hakupaswa kushiriki kwenye mchezo mgumu kama ule kama angeshauriwa vyema. Masaju, Mwakyembe na wengineo wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri mkuu wa mambo ya kisheria kwa Serikali inayoongozwa na Rais. Alikuwa wapi? Waziri Mwakyembe,mbobezi wa sheria, na Waziri mwenye dhamana ya kulinda Katiba na Sheria alikuwa wapi? Washauri wa pale Ikulu walikuwa wapi?

Lazima wajiuzulu au waondolewe. Hakuna namna nyingine.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Kila mtu angekuwa akiamka analopoka Fulani na Fulani wajiudhuru nchi ingekuwa haina dira.

Anyway mleta mada kajipange tena
 
Wataanzia wapi kujiuzulu wakati hawataki kitumbua chao kuingia mchanga, kama kawaida watu wengi waliopo kwenye serikali wapo kwa ajili ya kumfurahisha mkuu badala ya kutenda kazi kwa weledi,wameruhusu mtu mmoja avunje katiba huku wakimwangalia tu na kumshangilia, mbaya zaidi wanamsaidia dhambi hiyo.Kuna mambo mengi yanayopaswa kukemewa kutokana na kwamba yanavunja katiba lakini watu hao wanasindwa,wanaangalia maisha yao na si kumuudhi mkuu, yaani kwa kifupi wapo kama mkia wa mbuzi,haufukuzi nzi wala hauzibi sehemu za siri.
 
Kutokana na sakata la kikatiba lililopata tiba ya tabu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Mcheche Masaju; Waziri wa Sheria na Katiba Dr. Harrison Mwakyembe; Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kisheria na timu nzima ya washauri wa Rais wanapaswa kujiuzulu.

Rais hakupaswa kuucheza mchezo alioucheza wa kumteuwa Dr. Possi kuwa Balozi. Rais hakupaswa 'kusimangwa' na kuzungumzwa vile ikiwa amezungukwa na wasomi wengi tu wa Sheria, tena wenye jukumu la kumshauri na kumuongoza Rais kwenye mambo ya kisheria.

Pamoja na kwamba Dr. Possi, kwa kuteuliwa Ubalozi, ameshapoteza sifa za kuwa Mbunge hata kama hatajiuzulu rais hakupaswa kushiriki kwenye mchezo mgumu kama ule kama angeshauriwa vyema. Masaju, Mwakyembe na wengineo wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri mkuu wa mambo ya kisheria kwa Serikali inayoongozwa na Rais. Alikuwa wapi? Waziri Mwakyembe,mbobezi wa sheria, na Waziri mwenye dhamana ya kulinda Katiba na Sheria alikuwa wapi? Washauri wa pale Ikulu walikuwa wapi?

Lazima wajiuzulu au waondolewe. Hakuna namna nyingine.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Acha mihemuko mkuu, Rais angechukuliwa kuwa amevunja katiba iwapo angewaapisha bila kupunguza jina la mbunge mmoja.
Kwa kuwa hajafanya hivyo rais hawezi hesabika kuwa kavunja katiba.
Ndiyo maana kilichofuata baada ya uteuzi huo ni kutengua uteuzi wa mbunge mmoja(Possi) ambaye bila shaka ataandika barua ya kujiuzulu ili ubunge wake ukome kwa mujibu wa katiba kutokana na kupangiwa majukumu mengine na Rais.
 
Back
Top Bottom