Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amshauri Freeman Mbowe kutokwenda Polisi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
WANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamesema wamemshauri Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe, asiende kuripoti polisi leo.

Akizungumza jana Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, alisema Mbowe hatakwenda kuripoti polisi leo kwa sababu amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na inaanza kusikilizwa Februari 21 mwaka huu.

“Mbowe haendi polisi, tumemshauri asiende kwa sababu kesi yake inaanza kusikilizwa Jumanne (kesho).

“Kama wanamhitaji, waje keshokutwa (kesho) Mahakama Kuu, watampata hapo,”alisema Mallya.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema yuko Mwanza na hajawasiliana na Mbowe.

“Hapa niko Mwanza sijawasiliana na mwenyekiti, lakini kama nikiwasiliana naye, nitamshauri asiende huko polisi.

“Kwa hiyo, naweza kusema kilichofanywa na Kamishna Sirro si wito wa kipolisi bali ni siasa kama ambavyo alifanya Makonda kwa kutangaza majina ya watu hadharani.

“Wito wa polisi huwa ni wa kimaandishi, hawajamwandikia barua, hawajampigia simu.

“Hawa maafande wana namba zetu za simu sisi kama mawakili wa chama, kama wanamhitaji Mbowe kwanini wasitupigie simu mpaka watangaze kwenye vyombo vya habari,”alihoji Lissu.

Alipoulizwa kama Mbowe atakamatwa wakati wowote kuanzia sasa, Lissu alisema watalazimika kulishtaki mahakamani Jeshi la Polisi kwa kitendo hicho.

“Hatuwezi kukubali utaratibu huu, waache kufanya siasa, wakimhitaji mwenyekiti wetu wamwandikie barua,”alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.
BAVICHA nao wamtaka Kamanda Sirro kufuata sheria na Misingi ya Utawala bora kwa kumuita Kiongozi huyo ambaye pia ni kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni.
 
huu ni ushenzi kwanini kinamjibia huyu mtu,kwani chama ndo kimetuhumiwa au ni mtu binafsi??ni kama kipindi kile walivokua wanamtuhumu lowassa na kumng'ang'aniza lowassa mwenyewe aseme ukweli na sio chama kimsemee,kwanini na leo hii wasimwache mwenyewe ajisemeee??hili ni jambo binafsi na sio jambo la chama,chadema mmefirisika busara za kutambua hata jambo hili...???
 
Mwache amshauri tu simnasema nchi haina sheria sijui atamtetea vipi siku akidabwa msiangaike na vifungu
 
huu ni ushenzi kwanini kinamjibia huyu mtu,kwani chama ndo kimetuhumiwa au ni mtu binafsi??ni kama kipindi kile walivokua wanamtuhumu lowassa na kumng'ang'aniza lowassa mwenyewe aseme ukweli na sio chama kimsemee,kwanini na leo hii wasimwache mwenyewe ajisemeee??hili ni jambo binafsi na sio jambo la chama,chadema mmefirisika busara za kutambua hata jambo hili...???
We huoni wewe ndo umefilisika ? We kilaza
 
Huo ni ushauri au anampeleka mwenzie macho kumchuzi huu yeye mkono kwa ubwabwa... Utii bila shuruti..
 
Hawa jamaa swala la kutii sheria bila ya shuruti ni jambo gumu sana kwao

Hii ni kawaida ya waharifu duniani kwao kutii sheria na taratibu ni jambo gumu sana
 
Back
Top Bottom