Mwanasheria Mkuu: Ripoti ya mabilioni ya Uswisi ipo tayari

Mwanasheria Mkuu: Ripoti ya mabilioni ya Uswisi ipo tayari

Majina yawekwe wazi na kwajinsi serikali yetu ilivyozoea ni kwamba hatua hazitachukuliwa,ni wakati wetu

watanzania tuungane tukatae uovu katika serikali yetu tutaendelea hivi mpaka lini? tusikumbatie mafisadi,ile

demokrasia tuliyonayo tuitumie vyema,sisi ndo serikali tunaweza tukaamua nini kiwepo na nini kisiwepo,The former

US President Abraham Licoln defined Democracy is a government of the people by the people and for the

people.Shime watanzania tubadilike tuchukue hatua stahiki na hasa kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi

tufanye maamuzi sahihi ya kuchagua watu walio sahihi,bila kusahau swala la Katiba tufanye maamuzi sahihi si ya

chama fulani.
 
washahamisha kimya kimyaJK atacheka cheka tu
 
Unaambiwa danadana zinazopigwa nchi hii hata maradona hajawahi kuzipiga !
 
sina imani na serikali katika kushughulikia kesi kama hizi.sitegemei kuona maamuzi ya kizalendo

Hivi hatuwezi enda Cuba tukamuomba Fidel aje kutusaidia kuwanyoosha hawa viongozi. Na uzee wake he will do a great job. A better job than all of us TZdians put together. This is just too much na haiishi hapa kuna list zitakuja nyingi tu na hakuna kitakachofanyika zaidi ya maamuzi ya kubebana.
 
Hapa naona hadi sarikali tubinasishe ili kieleweke,sisi tumeshindwa
 
Mkapa, Mwinyi ‘waguswa’ na mabilioni ya Uswisi

Mwandishi Wetu

Toleo la 302
10 Jul 2013



Ben%20Mkapa.jpg



UTARATIBU wa Watanzania kwenda kuhifadhi fedha katika mabenki ya Uswisi ulikithiri wakati wa utawala wa marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, imefahamika. Picha za grafu na zilizotolewa na mtandao wa Umoja wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Duniani (CIJ) na ambazo Raia Mwema imefanikiwa kuziona zinaonyesha kwamba wateja wengi kutoka Tanzania walipeleka fedha zao Uswisi katika kipindi cha kati ya mwaka 1988 na 2007. Mwinyi alianza kuwa Rais wa Tanzania mwaka 1985 na kumaliza muda wake mwaka 1995 na Mkapa alianza mwaka huo na kumaliza awamu yake mwaka 2005. Mtandao huo, kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya duniani, vimeibua taarifa hizo kutoka katika benki maarufu ya HSBC iliyoko Uswisi na habari hizi ni sehemu ya kampeni kali ya kupambana na ufisadi.

Mtandao huo tayari umeibuka na taarifa kwamba Watanzania 99 wamehifadhi kiasi cha dola za Marekani milioni 114 katika benki hiyo, huku wakiwa na jumla ya akaunti 286. Hadi kufikia juzi usiku, ni Mtanzania mmoja tu, Sailesh Vithlani, ndiye ambaye anajulikana kuwemo katika orodha hiyo ya watu 99. Lakini Raia Mwema limeahidiwa na vyanzo vyake kwamba litapatiwa majina ya Watanzania wengine 98 waliobaki. Taarifa hizo za uchunguzi ambazo zimepachikwa jina la “SwissLeaks” zinaonyesha kwamba katika kipindi cha kati ya mwaka 1982 ambapo ndipo taarifa hizi zimeanza kuvujishwa hadi mwaka 2006, wateja 91 kati ya 99 waliokuwa na akaunti Uswisi ndiyo walifungua kiasi hicho. Kwa maana hiyo, wateja wengine wanane walifungua akaunti zao katika kipindi cha kati ya mwaka 2006 na 2007.

Mwezi Juni mwaka 2012, Benki Kuu ya Uswisi ilitoa taarifa iliyoeleza kwamba Watanzania wanahifadhi kiasi cha dola milioni 197 (zaidi ya Sh bilioni 313) katika akaunti mbalimbali nchini humo. Kwa taarifa za sasa za SwissLeaks, ina maana kwamba ukiondoa dola hizi zilizopo HSBC, kuna takribani dola nyingine milioni 83 katika benki nyingine tofauti nchini Uswisi. Hii ni kama walioziweka hawajaziongeza au kuziondoa kwenye akaunti zao tangu Juni 2012. Hata hivyo, mwaka juzi, gazeti hili lilibaini kwamba pamoja na ukweli kwamba Uswisi ndiko kunakosifiwa, Watanzania wamehifadhi fedha nyingi zaidi katika Visiwa vya Jersey vilivyo chini ya Himaya ya Waingereza kuliko za Uswisi. Gazeti liliwahi kuripoti kwamba fedha za Watanzania pekee zilizoko katika visiwa hivyo zinakadiriwa kufikia kiasi cha pauni za Uingereza milioni 413 (sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.06). Fedha hizo zinatosha kuhudumia bajeti za wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Afrika Mashariki kwa mwaka mzima bila ya kuomba fedha kutoka kwa wafadhili na bado ‘chenji’ ikabaki.

Gazeti hili haliwezi kutaja chanzo cha habari hizi kwa vile taarifa hii ilipatikana katika mkutano uliofanyika Uingereza wiki iliyopita chini ya kanuni za Chatham (Chatham Rules) ambazo zinakataza kutaja vyanzo vya habari zilizopatikana kutoka katika mikutano inayotawaliwa na kanuni hizo. Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zilizopatikana, Raia Mwema limeelezwa kwamba zaidi ya Jersey, kuna fedha nyingine nyingi katika visiwa vingine kama Cayman na Isle of Man ingawa pia kuna fedha zilizohifadhiwa jijini London, mji mkuu wa Uingereza. “Kuna watu binafsi ambao wamehifadhi fedha zao. Kuna fedha za kampuni kadhaa na kuna fedha za inayoitwa mifuko ya hisani. Naweza nikashindwa kuwapa majina haswa ya wenye fedha hizo lakini nadhani inawezekana kuwapa majina ya kampuni na mifuko hiyo ya hisani (trusts), kilieleza chanzo hicho. Kisiwa hicho ni miongoni mwa nchi zinazopendwa na watu, kampuni au taasisi zinazokwepa kulipa kodi au zinazopata mapato yake kwa njia ya kifisadi kwa vile zinatoza kodi kidogo na zina sheria zinazolinda usiri wa walioweka mali zao. Mkutano huo ulielezwa kwamba visiwa hivyo vilivyo chini ya Uingereza lakini vinavyojitawala vyenyewe vimehifadhi kiasi cha pauni bilioni 40 kutoka Afrika na katika hizo, pauni milioni 413 zinatoka Tanzania. Visiwa vya Jersey vilijipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania miaka michache iliyopita baada ya kubainika kwamba aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge, alikuwa na akaunti katika visiwa hivyo ambayo ndiyo iliyotumika kumwekea fedha (dola milioni moja) zinazodaiwa kutokana na mauzo ya rada ya kampuni ya BAE Systems kwa serikali ya Tanzania.










- See more at: Raia Mwema - Mkapa, Mwinyi ‘waguswa’ na mabilioni ya Uswisi
 
Hawana aibu Mkuu Mani Hawa wahuni. Wanakomba hazina kila kitu kasha kwenda kukinga mikono kwa wafadhili watusaidie. Nchi tajiri kama yetu haihitaji msaada hata wa senti mbili kutoka nchi yoyote ile ila hawa wahuni ndiyo wanaoiangamiza nchi yetu. Bora wafadhili wamestuka na hawatatoa tena senti yao hata moja ili hawa mafisadi waweze kuondolewa madarakani kirahisi kwani maisha kwa Wananchi wengi yatazidi kuwa magumu sana na hatimaye kujua kwamba adui mkubwa wa Tanzania na Watanzania ni hawa MACCM bin Mainterahamwe.

Halafu bila aibu tunaomba wajapan watununulie ambulance ya muhumbili!
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu ndiye yuleyule aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakimwaga mboga yeye anamwaga ugali?

Ndiye Mwanasheria aliyesema kuwa,sharti la kupeleka mswada wa mabadiliko ya Tume huru,kuhoji matokeo ya urais na upuuzi mwingine eti hadi hapo wanaukawa watakapoipigania rasimu pendekezwa ya maccm,vinginevyoUkawa watajiju?

Huyu ni mwanasheria mkuu,au Naibu Katibu Mkuu wa itikadi na uenezi wa ccm?, nchi hii wanasheria tunao,bado kweli tupo kwenye kujaribu kuhama kutoka Agrian society kuitafuta industrial revolution wakati wazingu wako kwenye post modernity jamaani!!!!
 
Kashfa zote ziwekwe hadharani kabla ya uchaguzi mkuu..ili CCM tuanze kujua tuna hasara kiasi gani, na kama mali zote za CCM zinatosha kulipa hasara hizo. UKAWA hawatakubali makabidhiano ya nchi bila fidia ya hasara
 
Hahahahaahahaaa saa kwanini asingesubiri hadi Bunge lifike ndio aseme kuwa iko tayari? Kulikua na haraka gani? anataka apooze kitu gani? No No No something is not okay here, changa la macho hili aisee
Sawa kabisa ni changa la macho na Ripoti yenyewe itasema hivi "Si kosa kuwa na fedha katika akaunti ye yote ya nje, na serikali imejiridhisha kuwa hela za watuhumiwa ni za halali. Hata hivyo serikali haitasita kuchukuwa hatua stahiki endapo ushahidi utaletwa kwamba hela hilo si za halali". End of the story
 
Hivi endapo itabainika kuwa kuna watumishi wa umma ktk orodha hiyo na ambao hawakui taarifu tume ya maadili ya viongozi wa umma kuhusu pesa hizo wanazomiliki huko nje. Je, serikali itawachukulia hatua? Maana kuna wengine tayari ni wastaafu.
 
Kwani na yeye hajaweka huko?Hizi za ESCROW kazifichia wapi?

Yeye zake kazichimbia kwenye SAFE yake kule shambani kwake MSOGA na zingine kampa mkewe akazigawe huko Lindi anakowania kuwa mbunge wao!!
 
Sawa kabisa ni changa la macho na Ripoti yenyewe itasema hivi "Si kosa kuwa na fedha katika akaunti ye yote ya nje, na serikali imejiridhisha kuwa hela za watuhumiwa ni za halali. Hata hivyo serikali haitasita kuchukuwa hatua stahiki endapo ushahidi utaletwa kwamba hela hilo si za halali". End of the story


Tukumbuke kuwa katika katiba ambayo inapendekezwa na hawa wezi ni pamoja na kuruhusu watu kuwa na account za fedha nje ya nchi!!! Kumbukeni kuwa CHENGE ndio alisimamamia uandishi wa hii katiba pendekezwa.!! Nchi hii ina mazingaombwe kweli.
 
Yeye zake kazichimbia kwenye SAFE yake kule shambani kwake MSOGA na zingine kampa mkewe akazigawe huko Lindi anakowania kuwa mbunge wao!!

Duh!Inaelekwa unajua mengi angalia KUCHA na MENO yako tu
 
masaju.jpg

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akizungumza kwenye mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, Dar es Salaam jana.

Picha na Abuu Kimario
Na Lilian Timbuka, Mwananchi

Posted Alhamisi,Februari12 2015 saa 9:6 AM
Kwa ufupi
Hayo yalisemwa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali


Dar es Salaam. Kamati iliyoundwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kuchunguza mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi, imekamilisha uchunguzi na inasubiri kukabidhi ripoti ya kazi hiyo kwa Spika wa Bunge.


Hayo yalisemwa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Dar es Salaam.

Masaju alisema kamati hiyo ilikamilisha kazi yake baada ya kuwahoji watu mbalimbali na kukamilisha kazi hiyo kama walivyoagizwa na Bunge na kinachosubiriwa ni kuikabidhi kwa chombo hicho cha kutunga sheria.

“Ofisi yangu kupitia kamati iliyoundwa tulikwishamaliza kazi hii, lakini hatuwezi kutoa taarifa kupitia sehemu nyingine zaidi ya ofisi iliyotupatia kazi kama utaratibu unavyoelekeza.

“Sasa wananchi na nyie waandishi wa habari msubiri taarifa hiyo itolewe kule bungeni ambako tuhuma hizi zilianzia,” alisema Masaju.



Watuhumiwa


Vigogo 10 wametajwa kuhusika katika kashfa hiyo. Inadaiwa kuwa katika orodha hiyo, yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).


Kamati ilivyoundwa


Kamati hiyo maalumu iliundwa kwa Azimio la Bunge baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuibua tena tuhuma hizo bungeni mapema mwaka jana, akidai kuna vigogo walioficha Sh323.4 bilioni katika benki mbalimbali za Uswisi.

Kiasi hicho cha fedha kinaweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 300 ambao ni sawa na kutoka Morogoro hadi Iringa.

Kwa mara ya kwanza, tuhuma hizo zilitolewa bungeni na Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), mwaka 2012.

Katika kikao cha Tisa cha Bunge, Zitto aliwasilisha hoja binafsi kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza Serikali kuchukua hatua dhidi ya Watanzania aliowaita vigogo walioficha fedha na mali haramu nje ya nchi.

Kutokana na hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne Makinda, liliipa Serikali muda wa mwaka mmoja ambao ulimalizika Oktoba mwaka jana iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake bungeni.

Wakati sakata hilo lilipokuwa limepamba moto, Serikali ya Uswisi kupitia kwa Balozi wake nchini, Olivier Chave iliwahi kusema Serikali ya Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguza na kurejesha mabilioni ya fedha hizo.

Balozi Chave alikaririwa wakati huo akisema hawajaona jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka kuzipatia ufumbuzi tuhuma hizo.

Chave alisema nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kujua uhalali wa fedha hizo na endapo zitagundulika ni chafu watakuwa tayari kuzirejesha nchini.


Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya fedha hizo zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi zilizopo nchini.

Hata hivyo, Machi mwaka jana ilielezwa kuwa mabilioni ya shilingi yaliyowekwa na Watanzania katika benki za Uswisi yalikuwa yameanza kuhamishwa kimyakimya.


Ripoti ya Benki za Uswisi ya 2012 ilionyesha kuwa fedha zinazotoka Tanzania zilipungua kwa karibu Sh36.4 bilioni ikilinganishwa na zilizokuwapo 2011 nchini humo, lakini haielezi sababu ya kupungua kwake.



Watanzania 99

Hivi karibuni, Timu ya Wanahabari wa Kimataifa wanaoandika Habari za Uchunguzi (ICIJ) ilitoa ripoti ikisema Watanzania 99 wanamiliki Dola za Marekani 114 milioni (Sh193bilioni) kwenye akaunti za benki nchini Uswisi.

Ripoti hiyo inayoitwa SwissLeaks iliyotolewa Marekani, imesheheni taarifa za Benki ya HSBC ya Uswisi na namna watu maarufu wakiwamo wanasiasa, wachezaji, viongozi wa dini na wafanyabiashara walivyoficha mamilioni ya fedha na kufanikiwa kuzikwepa mamlaka za mapato katika nchi zao.

Katika orodha hiyo, Tanzania inashika nafasi ya 100 duniani na nafasi ya pili Afrika Mashariki ikiwa nyuma ya Kenya inayoshika nafasi ya 58 duniani kwa kuweka zaidi ya Sh950 bilioni nchini Uswisi.

Ingawa taarifa hiyo haikutaja majina ya watu wote walioweka fedha Uswisi, imemtaja mfanyabiashara Shailesh Vithlani ambaye anadaiwa kuwa dalali wakati Tanzania iliponunua rada kutoka kwa kampuni ya BAE system kuwa ni miongoni mwao.

Hivi karibuni, Waziri wa Fedha Saada Mkuya alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akitahadharisha kwamba si kila aliyeweka fedha Uswisi amezipata kwa njia haramu.

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Kill 3, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi

tunaitaka orodha hiyo fasta
 
Hii ripoti ambayo Mwanasheria Mkuu mpya George Masaju alidai itafikishwa Bungeni kujadiliwa, mbona hatujasikia mjadala wowote kuhusu mabilioni haya yaliyofichwa Uswiss? Kulikoni?
 
Back
Top Bottom