Mwanasheria Mkuu awakaanga mawaziri

Mwanasheria Mkuu awakaanga mawaziri

Huyu Warema anaongea pumba sana sasa nimesoma hapo eti hata yeye anatakiwa afuate sheria hii ina maana gani? kwamba yeye ni mkubwa sana ama vipi?

Halafu eti “tunatakiwa kuiga msemo wa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema kuwa ‘tii sheria bila shuruti’, sasa huyu Said Mwema si ndo ameliamrisha jeshi la Polisi kwnda huko kuibia watu na kunyanyasa watu na kuwanajis watu? hiyo kutii sheria bila shuruti mbona yeye ameivunja., ilikuwa ashauri kwamba huyu Said Mwema na yeye awajibishwe.,

Halafu izo issue za kimahakama kama yeye ni mwanasheria mkuu wa Serikali kwanini yeye binafsi asihusike katika hili? nadhan hawa wote walikuwa wawajibishwe akiwemo na huyu Warema pia sio kuwakaanga wenzake kwa sababu wapo nje sasa.,

CCM ni wanafiki kuna baadhi ya wabunge wa CCM mule bungeni ambao walipata nafasi kuchangia kwenye ile ripoti ya kamati mbona tayari walishaanza kuwakingia kifua hawa mawaziri? na kina Warema walikuwa wanagonga meza ku-support? yule mama Assumpter aliposema ni wapinzani ndio waliouwa, sasa baada ya hapo wakasimama wabunge wengine wa CCM kusema hawa mawaziri waondoke na ilipobidi kuondolewa sasa wanaanza kuwakaanga me nadhan ni unafiki mtupu.,
 
Jaji Werema, ukiukwaji wa sheria na kudhalau ushauri kutoka kwa Mwana Sheria Mkuu sio kwa baadhi ya Mawaziri tu, hata baadhi ya Viongozi wa vyama vya Upinzani na Chama Tawala wanajiona sana na kufikiri wako juu ya sheria - wanafanya wapendalo!! Tusipo kuwa makini hawa ndio watalisambaratisha TAIFA letu kutokana na vitendo vyao na kauli zao hatarishi, wengi wao hawaoni mbali zaidi majivuno tu na ujeuri - wanafikiri Nchi hii ni ya kwao, raia wengine ni wapangaji - tusipokuwa makini na kuwakemea mapema kwa nguvu zetu zote watatufikisha pabaya!
 
Back
Top Bottom