Mwanasheria Mkuu awakaanga mawaziri

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,281
2,000
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema baadhi ya mawaziri wamekuwa wakaidi kufuata ushauri wa kisheria ambao amekuwa akiutoa na kwamba hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayotokea katika utendaji wa Serikali, yakiwamo yale yaliyobainika katika Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

Wakati Jaji Werema akiwananga mawaziri, kwa upande mwingine amemsifia Rais Jakaya Kikwete akisema kuwa yeye si kama mawaziri wake kwani ni msikivu na anayeshaurika. Akizungumza na mwandishi wetu jana, Jaji Werema alisema endapo ushauri ambao amekuwa akiutoa mara kadhaa kwa mawaziri ungezingatiwa, kilichotokea bungeni mwishoni mwa wiki cha mawaziri kung’oka kisingekuwapo.

“Tunatakiwa kuiga msemo wa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema kuwa ‘tii sheria bila shuruti’, Rais tunamshauri na anashaurika kwa nini mawaziri wakatae kuzingatia ushauri?” alisema Werema na kuongeza:

“Mawaziri hawatakiwi kujifanyia tu mambo yao. Tunawaandikia barua lakini zinakwenda na yanafanyika yaleyale... Hata mimi nikionekana kukiuka sheria na kanuni naweza kuwajibishwa kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.”

Jaji Werema alisema watu wanaweza kutofautiana kisiasa lakini katika mambo yanayohusu haki za binadamu lazima kuunganisha nguvu pamoja ili kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa bila kupindishwa.

Alikuwa akizungumzia kuhusu kung’oka kwa mawaziri wanne kutokana na matokeo ya uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili ambao ulifanywa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira.

Ripoti ya Kamati hiyo ilisababisha Rais Kikwete kutengua uteuzi wa Mawaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Tume ya Kimahakama

Kadhalika, Jaji Werema alisema Tume ya Kimahakama itakayochunguza kwa kina madhara yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili iliyosababisha vifo, majeraha, utesaji wa kinyama, uharibifu wa mali na upotevu wa mifugo, itaundwa na Rais Kikwete.

“Tume hii itakwenda mbali zaidi ya taarifa ya kamati, itachunguza waliohusika, waliosemwa katika ripoti kwa juujuu watatafutwa, kuangalia matumizi ya nguvu kiasi hicho na mwisho mapendekezo ya tume hiyo juu ya kipi kifanyike kwa wahusika itazingatiwa,” alisema na kuongeza:

“Hawa Mawakili wa Serikali waliokuwa katika operesheni hiyo, DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) atatakiwa kutoa maelezo, hao mawakili wake walikwenda huko kwa misingi gani pamoja na mahakimu waliokuwa huko.”

Hata hivyo, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo alisema hakuna haja ya kuundwa kwa tume hiyo na kinachotakiwa ni kutumika kwa sheria ya kutafiti sababu za vifo.
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,535
2,000
Hakuna haja ya kuwa na tume tena! Mauaji, mateso, unyanyasaji na unyang'anyi nk vyote vimefanyika na wahusika wanafahamika!

Kinachotakiwa wote wapelekwe mahakamani wakajitetee huko vinginevyo ni kupoteza fedha na muda bure!!

Kadri tunavyotumia muda mrefu kuchukua hatua ndivyo kadri tunavyoongeza maumivu kwa waliodhulumiwa haki yao ya misingi ya kibinadamu na kuishi!
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,613
2,000
sasa kama mwanasheria mkuu anaishia kuwananga mawaziri wasiofuata sheria nani hasa aliyebaki anayeweza kuwachukulia hatua??

this country bwana!
 

mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,390
1,250
Acha wawajibike kwa nini wafanye uzembe wa kizembe wacha watimuliwe ili wengine wakija washike adabu.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,215
2,000
dawa pekee na ambayo ndiyo wanastahili watuhumiwa hao ni kuburuzwa mahakamani tu , hayo manenomaneno tumechoka nayo .
 

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,385
2,000
mawaziri wamejikaanga wenyewe kwa uzembe wao mwanasheria hahusiki hapo
Sasa hivi kinacholalamikiwa ni mfumo kuwa ni mbovu kwani waziri anateuliwa na Rais, katibu wa wizara anateuliwa na Rais n.k. lakini uwajibikaji anatakiwa waziri awajibike peke yake hii si sahihi. Rais Kikwete aliishasema kuwa kama kuwajibika ni wote lakini anasita kuwawajibisha wateule wake wengine.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,215
2,000
Acha wawajibike kwa nini wafanye uzembe wa kizembe wacha watimuliwe ili wengine wakija washike adabu.

siyo kutimuliwa tu , lazima waswekwe jela , sipati picha kwa NCHIMBI kusokomezwa kwenye gereza la keko halafu awe chini ya NYAMPALA NGUZA VICKING !
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,619
2,000
Huyu mzee aache unafiki, yeye ndiye amekuwa akiwatetea mawaziri bungeni kila mara wapinzani wanaposema mapungufu yao. leo anajifanya kuwa hawakusikiliza ushauri wake. na yeye anatakiwa kuachia ngazi mara moja
 

ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
What if yeye ndiyo chanzo cha haya yote?... USA walimtumia Chenge wakatuletea sera za hovyo za madini na uwekezaji! Huyu Werema nae ametengenezwa na hao hao! Inaingia akilini kuendelea kugawa vitalu vya gesi wakati hatuna sera husika?... inaingia akilini kugawa vitalu vyote kwa wageni? kwanini sheria na mikataba ya kimataifa tuyoingia inatugharimu sana? inakuwaje tunakamata vipusa kasha tunavitia moto badala ya kuuza ili kuwapata fedha za kuwalinda Tembo waliosalia?.... AG huyu si mzalendo na hatufai ...yuko kwa maslahi ya SYMBION et al... Mwisho wa siku utasikia TANESCO wameingia mkataba wa miaka 100 wa uendeshaji na uzalishaji wa Umeme Tanzania... RIP Julius Kambarage Nyerere, Ulituachia nchi yenye nidhamu na maadali, ulituachia nchi yenye wanyama wa kila aina, ulituachia nchi yenye madini mengi, uliwaadaa na kuwasomesha bure hawa MAFISADI wenye kudhulumu mali za Watanzania! Tunakulilia Mwalimu...
 

Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
673
195
Ndugu yangu Kibo 10 na kubaliana nawewe kwamba Mawaziri wengi ni wakaidi na hawapendi Ushauri wa Kisheria hasa kwenye Mawizara kwani wamekuwa wakiona ushauri huo mara nyingi umekuwa ukienda kinyume na Matarajio yao. Lakini vile vile kuna jambo kubwa la kikatiba limetokea hapa ambalo tuliangalie wote kwa makini;

1: " Hawa Mawakili wa Serikali waliokuwa katika operesheni hiyo,DPP(MKURUGENZI WA MASHTAKA) ATATAKIWA KUTOA MAELEZO,HAO MAWAKILI WAKE WALIKWENDA HUKO KWA MISINGI GANI PAMOJA NA MAHAKIMU WALIOKUWA HUKO:Natumaini watatueleza na kufafanua yafuatayo:
1. Nani alikuwa akiwalipa posho kwa kipindi chote walichokuwa huko?
2.Je kuna mashtaka yeyote waliyo yafungua kama sehemu ya kuwako kwao katika Taskforce hiyo?
3.Je katika uendeshaji wao au uwepo wao katika Kamati kumeathiri vipi Misingi ya Haki asilia " PRINCIPLE OF NATURAL JUSTICE, Kwamba;Mtu asiwe Hakimu,Mpelelezi na Mwendesha mashtaka yeye mwenyewe KATIKA SHAURI HILOHILO na pia mtu hawezi kuwa Hakimu katika Jmabo linalo Muhusu kitaalamu wanazungumza kama
"NEMO JUDES IN CAUSA SUE "
4. Je hao Mahakimu waliteuliwa kuingia katika Kamati hizo kwa misingi gani? Jaji Mkuu aliidhinisha?je walikuwa wanakazi gani haswa katika Kikosi kazi hicho?

Msingi wa Pili ni Hoja ya Mheshimiwa Jaji Mstaafu ,Thomas Mihayo kwamba itumike sheria ya Kutafiti sababu ya Vifo. na dhani hapa anazungumzia The Inquest Act Sura ya 21 iliyorejewa mwaka 2002 ....Kimsingi sheria hii ipo na ninzuri kabisa na hata ingetumika kutafuta sababu na wahusika wa vifo kama vilivyotokea Morogopro,Soweto Arusha na Nyololo Iringa ingekuwa Rahisi sana na Sijui kwanini wanasheria na wadau wa Haki za Binadamu hawapendi kuitumia labda wana wasiwasi na uwezo wa Mahakimu.

Na Uzuri wa Sheria hii ni kwamba anybody can move the Corona`s Court " Ili kuchunguza Kifo chochote chenye Utata.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 12(1) ambacho kinaeleza kwamba
When any body is found ,or a person has died,in circumstances which make the holding of an inquest necessary or desirable,the person finding the body or becoming aware of the death shall as soon as practicable inform the Coroner,or a police officer or any appropriate authority and upon receiving that information the police officer or the appropriate authority shall notify a coroner having jurisdiction to hold an inquest.

Katika mazingira yanayozunguka Tukio hili , Tume ya Kimahakama siyo chaguo sahihi wala Inquest Act haita toa suluhisho sahihi la tatizo hili kwani hapa tayari Mahakama Imeguswa na lazima Mahakimu walioingia huko waliteuliwa kwa mujibu wa taratibu za Kiutawala za Mahakama kwahiyo Mahakama tayari inakuwa "subjudice" Mahakama nayo ni mtuhumiwa tayari wa vitendo hivyo.

Iwapo ningeulizwa ushauri basi kwa maoni yangu ningependekeza iundwe Tume huru na Rais nje ya mfumo wa sasa wa vyombo vya utawala itakayoundwa na Majaji wastaafu na ikiwezekana Majaji wawili kutoka Nje ya Tanzania katiaka nchi mojawapo mwanachama wa Jumuiya ya Madola ili waweze kuchunguza na watoe maoni yao iwapo kunawatu wanatakiwa kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria mbali na hatua za kiutawala kama kufukuzwa kazi au kujiuzuru.
 

marshal

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
353
225
Ki msingi nakubaliana na hoja ya AG kuwa mawaziri hawasikilizi ushauri wa kisherai waliopewa. Lakini zaidi ya hapo kuna tatizo kubwa serikalini kati ya watendaji,wataalamu, na wanasiasa. Siku Zote watendaji na wanasiasa wanahisi wana nguvu kuliko wataalamu na ndio maana vitu vingi havipo sawa. Tatizo kubwa ni kuwa nchi haieshimu usahuli wa kitaalamu iwe wa ki sherai, kihandisi,kisayansi ama kisiasa.

Nchi hii itendelea kuwa na matokeo mabovu ya maamuzi kwa sababu ya msingi mbaya tuliojiwekea. mifumo yetu ya maauzi haiko sahihi...
 

Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,412
2,000
tatizo serikali ya mapinduzi inaamini nguvu kulioko vingine ndo mazara yake hayo
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Analinda kitumbua chake kisiingie mchanga huyu!!! Madudu yote haya Serikalini miaka yote alikuwa wapi kuwananga Mawaziri hadi asubiri shinikizo la pili toka kwa Wabunge ndio aanze kubwabwaja!!!! Huyu naye ni tatizo kubwa sana ndani ya Serikali kama walivyo Mawaziri wote ndani ya Baraza la Mawaziri.


sasa kama mwanasheria mkuu anaishia kuwananga mawaziri wasiofuata sheria nani hasa aliyebaki anayeweza kuwachukulia hatua??

this country bwana!
 

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
1,195
Aweke bayana pia wakati Waziri Mkuu Mhe. Pinda alipotoa ruhusa kwa polisi na vyombo vingine vya dola kuwapiga raia yeye kama Mwanasheria Mkuu alimshauri nini hadi kupelekea PM kupelekwa mahakamani. Ama ndiyo staili ya kujitoa kwenye tatizo kila jambo linapoharibika. Inawezekana pia kwamba hata huo ushauri anaojinasibu kuutoa kwa mawaziri hajawahi kufanya hivyo bali ni njia ya kujikosha tu.

Mbona kwenye suala la kurushwa mabomu huko Arusha na kuuawa kwa akina Mwangosi suala la kuundwa Tume ya Kimahakama kuchunguza matukio hayo limepigiwa kelele sana lakini Serikali imeamua kulipuuzia. Werema kwa nafasi yake amemshauri nini Rais juu ya jambo hilo hadi sasa anajidai kumsifia rais kuwa ni msikivu na anashaurika.

Kamwe CCM na watawala wake hawajawahi kuwa na utamaduni wa kujali haki za binadamu na katika hilo Werema hawezi kukwepa dhambi hiyo asilani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom