Mwanangu; watakuja watalia lakini mwisho atabaki mkeo na wanao!

Loki

Senior Member
Feb 12, 2019
174
290
Baba alinisisitizia kuchukua likizo, kazini nilikua na mambo mengi sana lakini aliniambia kuwa mwezi mmoja wa kutokua kazini naweza ujutia maisha yangu yote kwani yeye hatavuka mwezi atakufa. Kwa namna alivyokua anaongea mpaka niliogopa, Baba yangu hakua mtu wa kudekadeka mara nyingii alijifanya mgumu hata alipokua anaumia sana, nilipomsikia anaongea vile nilijua kuwa kuna kitu na nahitajika kwenda kumuona.

Nilichukua likizo na kwenda nyumbani, kweli alikua anaumwa, alikua kaisha, alikua kakonda afya imedhoofu na alikua hawezi hata kunyanyuka. Alikua mple anaongea taratibu mnyonge sana, kwa mtu aliyekua anamfahamu Baba yangu angemuonea huruma na hata kutoa machozi kwa kumuona vile. Nilimuangalia kwa huruma lakini alilazimisha tabasamu, hakutaka kuonekana mnyonge.

Aliniambia kuwa wewe ndiyo mtoto wangu wakwanza, una wadogo zako sita na wakike wawili na wanaume wanne, kuna kitu nataka nikufundishe kabla sijafa ili uje kuwa Bora na si kuwa kama mimi. Nilimuitikia nikidhani kuwa kuna kitu ataniambia, lakini mpaka likizo inaisha hakuniambia kitu chochote, nilishangaa na kumuuliza mbona kaniahidi kuniambia kitu lakini hajaniambia na likizo inaisha natakiwa kurudi kazini.

Alitabasmau na kuniambia kuwa ameshaniambia. Nilifikiria sana nikijaribu kukumbuka kama kuna kitu labda aliniambia nikakisahau lakini sikukumbuka, nilifikiri sana na sana sikukumbuka chochote, nilishindwa nikamuambia Baba mbona sikumbuki chochote. Alitabasmau tena, huku akiongea kwa shida aliniuliza nimeka pale siku ngapi, nilimuambia siku 23, akaniuliza wewe una Shangazi wa ngapi nikamuambia wawili na Baba wadogo nikamuambia watatu.

Akaniuliza tangu nikae hapo walishakuja mara ngapi, nilimuambia Shangazi mmoja alikuja mara tatu, kuna mwingine kila baada ya siku mbili anakuja, Baba wado aliyekuja ni mmoja mara moja kwani wote wapo mjini na familia zao. Alitabasamu tena na kuniuliza vipi Mama yako tangu uje hapa yeye kaja mara ngapi? Nikashanga ana nikidhani labda Baba kachanganyikiwa nilimuambia.

“Baba Mama mbona kila siku yuko hapa, ndiyo anakupikia, anakusafisha, anakufanyia kila kitu? Inamaana umesahau?” Nilidhani Baba akili zimanza kupotea lakinia litabasamu na kuniambia “Hapana mwanangu, sikusahau leo kuwa Mama yako hayupo, nilisahau kipindi namuoa kuwa hayupo. Niliendekeza ndugu na kuwajali, niliwapa kila kitu huku Mama yako nikifungia ndani, nilikua nikimpiga kwa maneno tu ya ndugu zangu.

Alivumilia kila kitu kwakua hakua na pakwenda lakini leo yeye ndiyo yuko na mimi na ananihudumia kwa kila kitu wakati mimi sina pakwenda. Ndugu zangu wana maisha mazuri lakini wapo na familia zao wanakuja kunisalimia wakati Mama yako ananiogesha na kunilisha. Nyie wanangu mpo huko mna maisha yenu, siwalaumu lakini ukweli nikuwa mimi si jukumu lenu hata kuja kunisalimia mnapangiana zamu.

Lakini Mama yako hana cha zamu, akilala akiamka yuko na mimi, akigeuka ni mimi, akila ni mimi, akipumua ni mimi, nikijisaidia ni yeye, nikitapika niyeye, nikidondoka ni yeye. Wakati zamani nilikua namuambia kama umenichoka bado ondoka lakini leo siwezi hata kujisaidia bila yeye. Mwanangu wapende ndugu zako lakini kama hutaki kufa kwa unyonge kama mimi basi Mpende mke wako zaidi, huyo ndiyo Mungu akipanga utazeeka naye.

Ndugu watakuja kukusalimia tu na kukupa pole lakini wakubeba kinyesi chako ni mkeo. Mfanye abebe huku akikumbuka mema uliyomfanyia na si mateso uliyompa, mwanangu ukimnyanyasa mwanamke lazima utateseka tu, akitangulia kufa yeye utabaki na watoto wanaokuchukiaa kwakua ulimtesa Mama yao, hata kama hawakuona lakini utakua unaumia kila siku ukiwaona na ukitangulia wewe basi yeye ndiyo atakua karibu kukuhudumia, mheshimu sana mke wako.”

Baba alimaliza kuongea, akaniambia nimuache apumzike. Siku iliyofuata niliondoka kurudi mjini lakini sikufika, nilipigiwa simu kuwa Baba yangu kafariki dunia. Nilirudi kwenye msiba, ndugu zake walikuja na kulia tena sana. Lakini baada ya siku mbili wote walirudi kwao na familia zao, alibaki Mama tu, nilijikuta badala ya kulia natabasamu kwani Baba alinifundisha kuwa watakuja watalia na mwisho wa siku atabaki mkeo na wanao.

Comment, Shea uwezavyo

R.I.P WOTE WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kizazi hicho cha wanawake kinatoweka......ni endangered species hao..............hawa wa siku hizi kwanza atakusema wee kwa wenzie alfu utasikia "mmmh...hapana...mimi nimechoka....mtu ni kuumwa tuu hata haponi....usikute ni ma uhuni yake ndio yamemletea hayo magonjwa ya ajabu ajabu...sijui ana ngwengweeee.....kalelewe na wanawake zako huko mimi usiniletee magonjwa humu|"...alafu unakua umegeuziwa kesi na habari yako inaishia hapo hapo....anapata mtu mwengine instagraaammm....
 
Mkuu una ushuhuda kabisaa
 
Baba alinisisitizia kuchukua likizo, kazini nilikua na mambo mengi sana lakini aliniambia kuwa mwezi mmoja wa kutokua kazini naweza ujutia maisha yangu yote kwani yeye hatavuka mwezi atakufa. Kwa namna alivyokua anaongea mpaka niliogopa, Baba yangu hakua mtu wa kudekadeka mara nyingii alijifanya mgumu hata alipokua anaumia sana, nilipomsikia anaongea vile nilijua kuwa kuna kitu na nahitajika kwenda kumuona.

Nilichukua likizo na kwenda nyumbani, kweli alikua anaumwa, alikua kaisha, alikua kakonda afya imedhoofu na alikua hawezi hata kunyanyuka. Alikua mple anaongea taratibu mnyonge sana, kwa mtu aliyekua anamfahamu Baba yangu angemuonea huruma na hata kutoa machozi kwa kumuona vile. Nilimuangalia kwa huruma lakini alilazimisha tabasamu, hakutaka kuonekana mnyonge.

Aliniambia kuwa wewe ndiyo mtoto wangu wakwanza, una wadogo zako sita na wakike wawili na wanaume wanne, kuna kitu nataka nikufundishe kabla sijafa ili uje kuwa Bora na si kuwa kama mimi. Nilimuitikia nikidhani kuwa kuna kitu ataniambia, lakini mpaka likizo inaisha hakuniambia kitu chochote, nilishangaa na kumuuliza mbona kaniahidi kuniambia kitu lakini hajaniambia na likizo inaisha natakiwa kurudi kazini.

Alitabasmau na kuniambia kuwa ameshaniambia. Nilifikiria sana nikijaribu kukumbuka kama kuna kitu labda aliniambia nikakisahau lakini sikukumbuka, nilifikiri sana na sana sikukumbuka chochote, nilishindwa nikamuambia Baba mbona sikumbuki chochote. Alitabasmau tena, huku akiongea kwa shida aliniuliza nimeka pale siku ngapi, nilimuambia siku 23, akaniuliza wewe una Shangazi wa ngapi nikamuambia wawili na Baba wadogo nikamuambia watatu.

Akaniuliza tangu nikae hapo walishakuja mara ngapi, nilimuambia Shangazi mmoja alikuja mara tatu, kuna mwingine kila baada ya siku mbili anakuja, Baba wado aliyekuja ni mmoja mara moja kwani wote wapo mjini na familia zao. Alitabasamu tena na kuniuliza vipi Mama yako tangu uje hapa yeye kaja mara ngapi? Nikashanga ana nikidhani labda Baba kachanganyikiwa nilimuambia.

“Baba Mama mbona kila siku yuko hapa, ndiyo anakupikia, anakusafisha, anakufanyia kila kitu? Inamaana umesahau?” Nilidhani Baba akili zimanza kupotea lakinia litabasamu na kuniambia “Hapana mwanangu, sikusahau leo kuwa Mama yako hayupo, nilisahau kipindi namuoa kuwa hayupo. Niliendekeza ndugu na kuwajali, niliwapa kila kitu huku Mama yako nikifungia ndani, nilikua nikimpiga kwa maneno tu ya ndugu zangu.

Alivumilia kila kitu kwakua hakua na pakwenda lakini leo yeye ndiyo yuko na mimi na ananihudumia kwa kila kitu wakati mimi sina pakwenda. Ndugu zangu wana maisha mazuri lakini wapo na familia zao wanakuja kunisalimia wakati Mama yako ananiogesha na kunilisha. Nyie wanangu mpo huko mna maisha yenu, siwalaumu lakini ukweli nikuwa mimi si jukumu lenu hata kuja kunisalimia mnapangiana zamu.

Lakini Mama yako hana cha zamu, akilala akiamka yuko na mimi, akigeuka ni mimi, akila ni mimi, akipumua ni mimi, nikijisaidia ni yeye, nikitapika niyeye, nikidondoka ni yeye. Wakati zamani nilikua namuambia kama umenichoka bado ondoka lakini leo siwezi hata kujisaidia bila yeye. Mwanangu wapende ndugu zako lakini kama hutaki kufa kwa unyonge kama mimi basi Mpende mke wako zaidi, huyo ndiyo Mungu akipanga utazeeka naye.

Ndugu watakuja kukusalimia tu na kukupa pole lakini wakubeba kinyesi chako ni mkeo. Mfanye abebe huku akikumbuka mema uliyomfanyia na si mateso uliyompa, mwanangu ukimnyanyasa mwanamke lazima utateseka tu, akitangulia kufa yeye utabaki na watoto wanaokuchukiaa kwakua ulimtesa Mama yao, hata kama hawakuona lakini utakua unaumia kila siku ukiwaona na ukitangulia wewe basi yeye ndiyo atakua karibu kukuhudumia, mheshimu sana mke wako.”

Baba alimaliza kuongea, akaniambia nimuache apumzike. Siku iliyofuata niliondoka kurudi mjini lakini sikufika, nilipigiwa simu kuwa Baba yangu kafariki dunia. Nilirudi kwenye msiba, ndugu zake walikuja na kulia tena sana. Lakini baada ya siku mbili wote walirudi kwao na familia zao, alibaki Mama tu, nilijikuta badala ya kulia natabasamu kwani Baba alinifundisha kuwa watakuja watalia na mwisho wa siku atabaki mkeo na wanao.

Comment, Shea uwezavyo

R.I.P WOTE WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maisha hayana formula kuna waliowafanyia wema wake zao lakini wakati wa matatizo na uzee cha moto walikipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ilitokea na itatokea....Lakini lA Msingi ni kufahamu kila mwanafamilia ana umuhimu wake kwako..... mfano ikitokea sehemu ya Mama/Baba atasimama Mama/Baba na si mwingine.....Vilevile ikitokea unataka kuvua Nguo wote watatoka lakini Mkeo/Mumeo hatatoka.......

MAISHA NDIVYO YALIVYO........
 
Mkuu maisha hayana formula kuna waliowafanyia wema wake zao lakini wakati wa matatizo na uzee cha moto walikipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nilichojifunza mimi kikubwa kutoka kwenye hiki kisa ni kwamba mzee wake na mleta mada alikuwa anaumia nafsini mwake kuona kuwa alimtendea vibaya mke wake lakini mwisho wa siku akamprove wrong na kuwa msaada mkubwa kwake

So ni heri umtendee Wema mtu hata akija kubadilika wewe usononeke tu kuwa amekuheuka ila siyo kwamba wewe ulimtendea vibaya

A Big Lesson Brother

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba alinisisitizia kuchukua likizo, kazini nilikua na mambo mengi sana lakini aliniambia kuwa mwezi mmoja wa kutokua kazini naweza ujutia maisha yangu yote kwani yeye hatavuka mwezi atakufa. Kwa namna alivyokua anaongea mpaka niliogopa, Baba yangu hakua mtu wa kudekadeka mara nyingii alijifanya mgumu hata alipokua anaumia sana, nilipomsikia anaongea vile nilijua kuwa kuna kitu na nahitajika kwenda kumuona.

Nilichukua likizo na kwenda nyumbani, kweli alikua anaumwa, alikua kaisha, alikua kakonda afya imedhoofu na alikua hawezi hata kunyanyuka. Alikua mple anaongea taratibu mnyonge sana, kwa mtu aliyekua anamfahamu Baba yangu angemuonea huruma na hata kutoa machozi kwa kumuona vile. Nilimuangalia kwa huruma lakini alilazimisha tabasamu, hakutaka kuonekana mnyonge.

Aliniambia kuwa wewe ndiyo mtoto wangu wakwanza, una wadogo zako sita na wakike wawili na wanaume wanne, kuna kitu nataka nikufundishe kabla sijafa ili uje kuwa Bora na si kuwa kama mimi. Nilimuitikia nikidhani kuwa kuna kitu ataniambia, lakini mpaka likizo inaisha hakuniambia kitu chochote, nilishangaa na kumuuliza mbona kaniahidi kuniambia kitu lakini hajaniambia na likizo inaisha natakiwa kurudi kazini.

Alitabasmau na kuniambia kuwa ameshaniambia. Nilifikiria sana nikijaribu kukumbuka kama kuna kitu labda aliniambia nikakisahau lakini sikukumbuka, nilifikiri sana na sana sikukumbuka chochote, nilishindwa nikamuambia Baba mbona sikumbuki chochote. Alitabasmau tena, huku akiongea kwa shida aliniuliza nimeka pale siku ngapi, nilimuambia siku 23, akaniuliza wewe una Shangazi wa ngapi nikamuambia wawili na Baba wadogo nikamuambia watatu.

Akaniuliza tangu nikae hapo walishakuja mara ngapi, nilimuambia Shangazi mmoja alikuja mara tatu, kuna mwingine kila baada ya siku mbili anakuja, Baba wado aliyekuja ni mmoja mara moja kwani wote wapo mjini na familia zao. Alitabasamu tena na kuniuliza vipi Mama yako tangu uje hapa yeye kaja mara ngapi? Nikashanga ana nikidhani labda Baba kachanganyikiwa nilimuambia.

“Baba Mama mbona kila siku yuko hapa, ndiyo anakupikia, anakusafisha, anakufanyia kila kitu? Inamaana umesahau?” Nilidhani Baba akili zimanza kupotea lakinia litabasamu na kuniambia “Hapana mwanangu, sikusahau leo kuwa Mama yako hayupo, nilisahau kipindi namuoa kuwa hayupo. Niliendekeza ndugu na kuwajali, niliwapa kila kitu huku Mama yako nikifungia ndani, nilikua nikimpiga kwa maneno tu ya ndugu zangu.

Alivumilia kila kitu kwakua hakua na pakwenda lakini leo yeye ndiyo yuko na mimi na ananihudumia kwa kila kitu wakati mimi sina pakwenda. Ndugu zangu wana maisha mazuri lakini wapo na familia zao wanakuja kunisalimia wakati Mama yako ananiogesha na kunilisha. Nyie wanangu mpo huko mna maisha yenu, siwalaumu lakini ukweli nikuwa mimi si jukumu lenu hata kuja kunisalimia mnapangiana zamu.

Lakini Mama yako hana cha zamu, akilala akiamka yuko na mimi, akigeuka ni mimi, akila ni mimi, akipumua ni mimi, nikijisaidia ni yeye, nikitapika niyeye, nikidondoka ni yeye. Wakati zamani nilikua namuambia kama umenichoka bado ondoka lakini leo siwezi hata kujisaidia bila yeye. Mwanangu wapende ndugu zako lakini kama hutaki kufa kwa unyonge kama mimi basi Mpende mke wako zaidi, huyo ndiyo Mungu akipanga utazeeka naye.

Ndugu watakuja kukusalimia tu na kukupa pole lakini wakubeba kinyesi chako ni mkeo. Mfanye abebe huku akikumbuka mema uliyomfanyia na si mateso uliyompa, mwanangu ukimnyanyasa mwanamke lazima utateseka tu, akitangulia kufa yeye utabaki na watoto wanaokuchukiaa kwakua ulimtesa Mama yao, hata kama hawakuona lakini utakua unaumia kila siku ukiwaona na ukitangulia wewe basi yeye ndiyo atakua karibu kukuhudumia, mheshimu sana mke wako.”

Baba alimaliza kuongea, akaniambia nimuache apumzike. Siku iliyofuata niliondoka kurudi mjini lakini sikufika, nilipigiwa simu kuwa Baba yangu kafariki dunia. Nilirudi kwenye msiba, ndugu zake walikuja na kulia tena sana. Lakini baada ya siku mbili wote walirudi kwao na familia zao, alibaki Mama tu, nilijikuta badala ya kulia natabasamu kwani Baba alinifundisha kuwa watakuja watalia na mwisho wa siku atabaki mkeo na wanao.

Comment, Shea uwezavyo

R.I.P WOTE WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom