1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo,
mwingine anaweza kuwa mama wa watoto
wako, lakini ukipata mwanamke ambae
atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao
na mama kwa familia, tafadhari mwanangu
usimuache huyo!
2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako
kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za
jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata
nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa
majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi
pamoja!
3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha
familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako,
usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama
utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa
sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa
familia!
4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu
na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na
mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha
mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu
mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi
fungu husika hata kama limetokana na
michango yenu wawili. wanawake wanajua sana
kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye
kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa
nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela
zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata
kama utakuwa umeishiwa!
5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo,
maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake
kwa muda mrefu sana na huacha kidonda
ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana
kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!
6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado
utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na
mke wako, sio muda mrefu utakuwa bacheol
tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke
na mume!
7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi
na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na
mashamba makubwa na mavuno yalikuwa
makubwa, lakini kwa sasa maisha
yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke
wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na
mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia
ukubwa wa familia yako!
8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao
nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza
kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini
kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini
ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana
pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike
kikubwa unachotakiwa kukifanya ni salamu
itakuw unatosha
9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza
kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia
hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui
mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na
kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae
aliweza kusimama imara wakati wote wa
mapito yenu magumu.
10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au
kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna
kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha
kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au
kutimiza wajibu wako.
11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au
kumlinganisha mke wako na mwanamke
mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia
sana na hajakufafanisha na mwanaume
mwingine yoyote huko nje na ndio maana
aliamua kuwa na wewe.
12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa
haki za wanawake, sawa,kama mwanamke
anasema ana haki sawa na wewe katika
nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani
kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu
timiza nusu yako na mwambie atimize nusu
iliyobaki.
13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa
bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana
kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo
bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa
muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na
wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na
ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo
ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.
14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule
kwa kuwa nilikuwa mjinga kama waze wengi
wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye
ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya
wanawake sasa kimefanya wanaume
waonekana ni watu wa kawaida sana na sio
muhimu kama zamani, Ukijaliwa watoto wape
elimu.
15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu,
wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa
siwezi kukudanganya, wengine waliongeza
urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua
na masikio lakini usisahau hawakuonyesha
maumbile yao nyeti hadharani kama sasa.
Hakikisha mkeo analijua hili!
16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna
hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye
maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu
wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba
usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa
kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama
gazeti kwa kila mtu.
17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa
cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa
kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua
cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie
mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na
uwezo wako kama ambavyo unahangaika
kutimiza ndoto zako.
18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na
mama yako, utu uzima una changamoto nyingi
sana na Mungu akikujalia utaziona muda
ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako
kama baba wa familia kumbuka pia bado
tunaishi na wewe ni mtoto wetu.
19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali,
Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui,
ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu
kila siku!
20.mwanangu.....................
Very wise and powerful message. Asante sana mletaji. Thanks.
21: mwanangu sio lazima uchangie kwa kuwuote hata kawaida ujumbe na shukrani zitafika tu,unajaza server