Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
36,447
Reaction score
110,234
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
 
Hapo inatakiwa uanze kumpigia mara kwa mara na sio salamu iwe ni kumjulia hali na kuulizia vitu mbalimbali mfano kuwaulizia ndugu zako,au watu fulani ambao yeye anaweza waelezea,hii itakuza conversation yenu...mtu akiwa hana stori au sio muongeaji just ask him or her questions hapo mtazidi kuongea mpaka mtakua mnapiga stori
 
Niwe natumia maswali zaidi ile yeye awe anaongea sana right? Thanks sana kiongozi
 
iko ivo mara nyingi hata mie wakati nasoma nje ya mkoa wangu mzee alikuwa akiona simu yangu anajua ni hela hapa inaita ikikata ni kutuma msg "kesho nenda stendi bahasha yako ntaituma" kitambo iyo hamna mpesa.

wazee wamekuwya makauzu sana hata kumshirikisha jambo ni ngumu, sema mzee wangu alibadirika baada ya mie kuanza mishe za porini. alikuwa lazima anitwangie simu kujua khali yangu ndo mwanzo wa stori nae hadi leo.
 
"Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe nilitemzoea zaidi duniani.
Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana afu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba ake anaingea nae mno kuliko sie."

Duh... We na huyo was Tanga mna wachumba??? Labda mzee Kuna vitu anahisi kwenu...
 
Hongera je ulianza vipi? Sidhani kama nishawahi kuongea na mzee zaidi ya dk 2. Ni simu tu ya shida basi. Wazazi wa kizazi kipya tubadirike kwakweli
 
Hili jambo hata mimi nilikuwa sina story na father nilianza kupiga nae story kidogo nilivyomaliza A'level.


Ilikuwa hata nikipiga simu ni salamu ya shikamoo kwisha ila nikatafuta mbinu mwenyewe kama kuulizia shughuli zake zinaenda vipi. Kuulizia ndugu na kumpa salamu na habari ya ndugu niliyoongea nao.

Japo huwa tunazungumza sana hadi leo ila likija kwa mama hapo naweza hadi kumaliza bundle.
 
Hamna wachumba.. sema tunampenda sana mama..Afu mm sikulelewa na mama na sijakaa nae sana mpaka leo. Nikipata muda kwenda home nakaa naongea nae sana ili kufidia..vile nikiondoka nimeondoka
 
Mimi bando la kuongea na mama halijawahi kutosha! Dk 70 zinaisha ila bado nataka tuendelee kuongea. Nipeni mbinu nirudishe uhusiano na mzee
 
Hongera je ulianza vipi? Sidhani kama nishawahi kuongea na mzee zaidi ya dk 2. Ni simu tu ya shida basi. Wazazi wa kizazi kipya tubadirike kwakweli
nilienda fanya kazi mkoa flani porini kias basi mzee alikuwa na hofu na maisha yangu (maana ile jamii ya kule wanapenda migogoro) akawa ananitwangia kujua maendelea yangu. basi na kumpa stori za huko ndio mawasiliano yakafufuka hadi leo.

siku izi nampa hadi 'habari mvunjiko' nkizipata huku yeye akiisikia kwenye tv ananitwangia pia kuniambia kumbe kweli.

juzi tulikuwa tunapiga stori ya jamaa aliye muua mpz wake, nikampa ya jamaa kenya kumuua mwenzake kisa kumbikumbi alishangaa sana nasubiri akiiona atanitwangia kushangaa zaidi
 
Nilishapitia hayo maisha, ni saikolojia zaidi. Anza kwa kumtumia vocha ya shilingi elf 5 kila mwezi utaona akipokea aidha anakutumia meseji kukushukuru au kukupigia kukushukuru.

Then wakati mwingine zungumza nae kuhusu uzoefu wake juu ya maisha ya kiume ukiomba ushauru namna ya kuwakabili wanawake, kupambana kuzalisha mali n.k. n.k.

Kuwa mdadisi wa kutaka kujua historia yenu babu zake na baba yako kama vile unataka kutengeneza family tree history...

Kila la kheri.
 
Title mwanangu hataki kuongea na mimi nifanyeje.

So ukishashauriwa utaenda kumpa ushauri mzee wako?

Kwanini umuite baba yako dingi? Sisi kumheshimu mzee wako inaanzia na wewe unavyomwasilisha kwetu, kama unamuwasilisha kama dingi na hujisikii kumuita baba mbele yetu pengine unataka tukuone mhuni sana basi kuna tatizo mahali.
 
Naomba msome vema mtaka Ushauri.Hili mnapaswa kulibeba na kujitathimini.Ukiona unapenda storm na mama yako zaidi si dhambi bali unauoga fulani na unahitaji kufarijiwa .Anayeongea na baba yake mara nyingi anaweza kukabiliana na maisha na si mwoga na kufanya shughuli Za maendeleo ni jambo la kawaida,pia katika familia anasimama kama baba .Msiwaogope baba mshirikishe hata ya kukosolewa ni vema
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Mimi na dogo hufanya mashindano ya kucheza muziki nyumbani ku bond. Pia hujadili mambo mengi kwa kumpa uhuru mkubwa sana. Na kwa sababu hiyo anaweza kujiamini sana, kuuliza maswali magumu na kuwa mtu mwenye utashi.

Maisha ya kumuogopa baba yanamfanya mtoto asiwe na uhuru, yanaua utashi, yanaleta sononeko na si mazuri kiujumla.
 
Historia ya babu anaijua bamkubwa..ndio hua naongea nae sana. Natamani angekua ndio baba maana ana stori hatari
 
Hili jambo hahah sisi kwetu tulikua kujiskia baba yupo nyumban hata kukohoa tabu akisafir sherehe tulikua ni salam tu labda sana sana akitaka akutume....ila sshv ss anatupigia SIM kila uchwao anasema tunamsusa daaa tumemzoea sana mama haipiti siku mbili sijamgongea SIM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…