Mwanangu anauliza; Kama dunia iliumbwa bila masaa (time zone), je punda na kuku nani kawafundisha kusoma majira hadi wawike?

Wale mliozaliwa masaki mkae msikilize tu!

Mwanangu asubuhi hii tukiwa njiani tunaelekea shule kaniuliza swali;

Ikiwa wanasayansi ndiyo waliotuletea Massa, (time zone-GMT) kwa kuweka sekunde,dakika hadi saa nzima kama tunavyosoma shule!

Je; kuku au punda walijuaje kuwika mda muafaka?

Kwa mliozaliwa mjini ni kwamba; Punda anaouwezo wa kuliaa/kubweka kila baada ya lisaaa limoja, na ukiangalia mda kwenye saa inakuwa kweli saa kamili!

Naombeni majibu yenu wadau; Maana dogo nimemwambia tutaongea jioni aniache kwanza asubuhi ninawahi kazini
View attachment 1219228
Unaposema muda muafaka unamaanisha nini? Maana navyoona Ukishasema muda muafaka, hapo tayari umeshakuja kwenye kipimo cha muda na wewe umesema muda muafaka kwavile tu unalinganisha kipimo cha muda na matukio ya wanyama. Kumbuka kabla ya kuwekwa kipimo cha muda watu walitumia jua tu kutofautisha nyakati
 
yaani punda analia kila inapotimia saa kamili, mfano, saa 12 kamili utamsikia poopiiiiiipoooooooooopiiiiiiiiiii.....
 
"Wanasayansi ndiyo waliotuletea masaa" ama kweli ni mtoto ungeuliza hili swali wewe mtu mzima ningekuona wewe haujitambui ila kwa kuwa ni mtoto ni haki yake .
 
Hili swali ni kielimu zaidi. Huyo dogo ana akili sana. Shuleni kwake hakuna mwalimu atakaejibu hili swali. Na ndio maana babaake amelileta kwa magreat thinker,au na nyie mmechemka?
daadeki hivi umesoma post yake vizuri labda na wewe uwe na akili sawa na huyo dogo hebu rudia kusoma post vizuri kisha ndo urudi ku comment
 
"Wanasayansi ndiyo waliotuletea masaa" ama kweli ni mtoto ungeuliza hili swali wewe mtu mzima ningekuona wewe haujitambui ila kwa kuwa ni mtoto ni haki yake .
we kweli popoma! sekunde zimetengenezwa na nani?
 
daadeki hivi umesoma post yake vizuri labda na wewe uwe na akili sawa na huyo dogo hebu rudia kusoma post vizuri kisha ndo urudi ku comment
wewe uliyeelewa tusaidie! achana na personal attack!
Toa jibu
 
yaani punda analia kila inapotimia saa kamili, mfano, saa 12 kamili utamsikia poopiiiiiipoooooooooopiiiiiiiiiii.....
Tunajua saa kamili baada ya kuwekwa kipimo cha muda. Unadhani hapo mwanzoni kipindi watu wanatumia jua kutofautisha nyakati waliweza kutambua ukamili huo? Baada ya mzungu kuweka kipimo cha muda yaani dakika, sekunde, na saa ndipo tumeweza kutambua ya kwamba punda analia kila inapotimia saa kamili. Hata punda mwenyewe hajijui kama analia baada ya muda gani kwasababu wao hawana elimu ya kipimo cha muda
 
Nimewahi kukutana na swali la kichokonozi kwa binti yangu akiwa standard 5, anamaliza form 4 mwaka hu. Ningekua ndio mimi nimuelizwa na dogo hivyo, this is what I could tell him:- Wakati wana sayansi wanatengeneza saa, waliangalia interval ya punda kubweka na jogoo kuwika, yaani lile jogoo la kwanza kuwika then wakaona waseme hiyo ni saa 10 alfajiri na interval ya saa hadi saa 1 wakaweka kwa interval ya kubweka kwa punda huku pia wakihusisha na utosi wa jua, hadi mwisho jogoo alipowika tena siku ya pili alfajiri then wakapata hizo saa 24 kwa siku, kumbuka mambo haya ya ugunduzi wa saa hayakufanywa siku moja au mwezi mmoja, walifanya kwa muda kidogo. Hope utakua umemtoa wasi wasi. NIna hakika huyu dogo kama sio mwenda ile inaitwa sunday school basi atakua anasoma madrasa baada ya shule but asilimia kubwa huyu ni mtoto wa Sunday school.
 
daadeki hivi umesoma post yake vizuri labda na wewe uwe na akili sawa na huyo dogo hebu rudia kusoma post vizuri kisha ndo urudi ku comment
Hata kabla hajauliza hilo swali,mimi pia nilishawahi kujiuliza hicho hicho kitu alichouliza. Vinginevyo usilifikirie kama unavyolichukulia wewe kijujuu. Hili swali lipo kifirosofi zaidi. Hili swali lina mchanganuo wa kutosha tu. Kuna elimu ya kutosha hapo. Kwa wewe sikulaumu,unaweza ukawa na mambo mawili unayo. 1. Unakaa masaki,huna uzoefu na punda wala jogoo. 2. Ni nyie wa elimu hii ya siku hizi ya kurahisisha kila jambo,unaona linaweza kupatikana kwa ku-google
 
we kweli popoma! sekunde zimetengenezwa na nani?
Huyu mimi mwenyewe nimemuona kilaza namba 1. Hajifikirishi. Haoni hata wenzie wanajishughulisha angalau anadadavua kwa kusema wanasayansi
 
Kamjibu hivi- wanasayansi waliotengeneza saa,wamefuata vitu vya asili kama jua,giza,mwanga,wanyama kama punda,kuwika kwa jogoo,ni miongoni mwa vitu vilivyowaongoza kutengeneza muda (saa). Kwa hiyo hivyo vitu vya asili vilikuwepo kabla ya hizo saa.
 
Ni hoja fikirishi sababu jogoo huwika saa 9 alfajiri, Kisha saa 12 alfajiri, Saa saba mchana, Saa tisa Alasiri kisha saa 12 jioni then anafunga mahesabu.

Je umeshawahi kujiuliza anajuaje timing?

Tunazungumzia jogoo Pure wa kijijini si hawa wa kwenu ma bloiler wanawika hata usiku wa manane au wakiona unakula chipsi.
 
Kwani punda wamekwambia ni saa tisa au saa kumi? wao wanafuata majira na nyakati na si masaa yaliyowekwa na wanadamu
 
Vipi kuhusu changamoto ya mawingu, au kunapokuwa na mvua, unawezaje kubashiri nyakati ilihali jua linalotegemewa lijulishe nyakati halijatoka ipasavyo? Swali langu halijalenga kutofautisha usiku na mchana bali limelenga kutofautisha nyakati za hapa katikati kabla ya jua kuzama.
I think mawingu na mvua haviathiri sana mawio na machweo ya jua, tunakosa kuona muangaza tu wa jua au muangaza wake hupungua tu ila jua huwa linatoka na kuzama kama kawaida, na kwa hio nyakati zinaendelea kuwa kama kawaida. Mfano nilitoa wa ulaya mawio na machweo ya jua hubadilika sana na hivyo nyakati zinabadilika sana, na hivyo saa huwa zinatumika kwa shughuli za kimaisha tu kama kwenda kazini na kutoka.... ila hazilingani na nyakati tulizozowea sisi huku kwetu Tanzania.
 
Kamjibu hivi- wanasayansi waliotengeneza saa,wamefuata vitu vya asili kama jua,giza,mwanga,wanyama kama punda,kuwika kwa jogoo,ni miongoni mwa vitu vilivyowaongoza kutengeneza muda (saa). Kwa hiyo hivyo vitu vya asili vilikuwepo kabla ya hizo saa.
asante kwa wazo ila nisije mdanganya mwanangu tu
 
Kwani punda wamekwambia ni saa tisa au saa kumi? wao wanafuata majira na nyakati na si masaa yaliyowekwa na wanadamu
kwanini huyo punda analia after 60sec? tena exactly time kama ni saa 7 basi saa saba kamili, 8kamili
 
Africa ndio maana haiendelei toto unalilipia ada Lina kuja na maswali ya kuuliza jogoo kuwika na punda kulia badala ya kuuliza trekta au ndege zinatengenezwaje.Angekuwa mwanangu namwachisha shule aende akachunge punda na kuangalia mabanda ya kuku kuliko kuendelea kulipia ada toto kama hilo
 
Back
Top Bottom